respect wa boda
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 4,556
- 3,838
Mwanasiasa mashuhuri Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.
Mfanyabiashara huyo na Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii.
Muungano wa vyama kadha vya upinzani uliamua kumuidhinisha Katumbi kuwa mgombea mwezi Machi.
Katumbi aliidhinishwa na muungano wa vyama vya upinzani Machi
Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo ni za uongo.
Moise Katumbi anaweza kuwa rais DR Congo?
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.
Chanzo: BBC
Maoni yangu: Nauona mwanzo wa kuporomoka kwa Tajiri huyo wa Congo au kama sivyo basi Katumbi ni pandikizi la Joseph Kabila ndani ya Upinzani. Mbinu kama hiyo Kabila aweza kuwa ameokopi toka Tanzania kwa uchaguzi wa Oct mwaka jana.
BACK TANGANYIKA