Confused or divided Government?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Hoja ya Katiba Mpya
  • Waziri anayehusika / Mwanasheria Mkuu wa Serikali - Nchi haiko tayari kwa sasa na hatuna uwezo, na isitoshe iliyopo inatosha tu kufanyiwa malekebisho
  • Rais - Umefika wakati muafaka katiba ibadirishwe ili itufikishe kwenye miaka mingine 50 ijayo
Hoja ya kulipwa ama kutolipwa Dowans
  • Waziri aneyehusika / Mwanasheria Mkuu wa Serikali - Ni lazima tulipe na hakuna jinsi tunaweza kukwepa kulipa
  • Rais - Lazima tulipe, halafu baadaye - hili deni ni kubwa mno lazima tutafute namna ya kulipunguza ama kulifuta kabisa.. Wanaohusika watafute jinsi ya kulipunguza deni hili au kuepusha taifa lisilipe
Wavamizi wa hifadhi ya barabara
  • Waziri anayehusika - wote waliovamia hifadhi ya barabara lazima waondoke kwa gharama zao na wakishindwa serikali itawabomolea na kuwalazimisha kulipia gharama zitakazotumiwa na serikali katika bomoa bomoa hiyo
  • Waziri Mkuu - inabidi isitishwe kwanza
  • Rais - Bomoa bomoa iko pale pale lakini muangalie namna (ili kusudi watu wetu wa karibu wasiathirike ila walala hoi hao hakuna shida). Kwa maneno mengine Rais anataka watendaji wake wapindishe sheria ikibidi....
My take:
The President is not very clear, or lacks definitiness of purpose and authority in his statements thus ending up confusing everybody on what he actually stands for!
 
Has he ever stand on anything? He is just a flag it goes with tune of the wind,unfortunately that is our presidaa mr mkwere
 
Mwanzoni mwa Anguko la Uchumi Duniani (Economic Crunch):

Rais: Matatizo yanayosababishwa na anguko la uchumi hayatatuhusu wala kutugusa. Uchumi wetu hauko linked na uchumi wa nchi za magharibi

Baadaye:

Rais: Tunakabiriwa na hali ngumu ya kimaisha kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa dunia!
 
Raisi- " Pia muwalipe wote wanaostahili kulipwa fidia na msiwalipe wale wasiostahiki na msiangalie unafuu wa serekali pekee"

Waziri wa fedha- "Serekali haiwezi kupunguza kodi ili mwananchi apate unafuu"

Sasa kama raisi anasema serekali isipewe unafuu inakuwaje waziri wake wa fedha hataki serekali ibebe mzigo wa kodi kwa niaba ya wananchi?
 
Watanzania tunafanywa mazuzu sana na hawa watawala uchwara!kauli zao huwa za kuwazia matumbo yao tuu!
 
Mwanzoni mwa Anguko la Uchumi Duniani (Economic Crunch):

Rais: Matatizo yanayosababishwa na anguko la uchumi hayatatuhusu wala kutugusa. Uchumi wetu hauko linked na uchumi wa nchi za magharibi

Baadaye:

Rais: Tunakabiriwa na hali ngumu ya kimaisha kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa dunia!

Tehehehe!
 
No society can surely be flourishing and happy, of which the far greater part of the members are poor and miserable-ADAM SMITH (A pioneer Political economist)
 
It doesn't rely on strong argument that based on scientific researches and evidnences. I do believe that they say according to their information, knowledge and capacitity at that particular time. They do not focus far in future. That why they always keep on contradicting themselves daily like
'Hatuguswi na aguko la uchumi la dunia' oohh "tunakabiliwa na hali ngumu ya uchumi kutoka na aguko la uchumi la dunia"

They should be visionist
 
the problem with our president wants to b loved by everyone..! mr kikwete only a mad man appeals to everyone...! lets knw ur stand on important issues facing our nation..!

THE SHILLING IS PLUNGING THAN EVER B4....! and u think we like looking at ur smiling face..? think twice..! i wish wananchi had courage like the pipo of Egypt,Tunisia and Libya.

" kumchagua tena kikwete ni janga la kitaifa" Dr wilbrod slaa
 
Japo wameaminiwa ustawi wa taifa, wanachofanya ni kila mtu anakula kamuhogo kake na kuangalia paji la uso wake pekee
 
Mtu ukitaka kuelewa serikali yetu hivi sasa ilivyo hadi kwa watendaji ni sawa na picha za Simba na Yanga za miaka hiyo ambapo unakuta kundi fulani la wachezaji ama hutii Dewji tu au Marehemu Abbas Gulamali, Tarimba, George Mpondela, au Rage kwa kutegemeana na nani aliyemuingiza mle.

Utii wa utumishi serikalini ni mparaganyiko kwa kwenda mbalee tena wengine ni hujuma ya juu kwa juu nyumba kudondoka yenyewe kwa mchu wa kutafuna chuma ambao ndio wengi zaidi waliomo huko.

Mambo si mseto tena serikalini, mambo ni mparaganyiko mtupu tangu ngazi ya kata hadi Magogoni; kula mmoja keshaanza kupiga darubini mbele kwa uhakika wa mabadiliko makubwa yanayoendelea kucheleweshwa na CHADEMA kutokea.
 
Duh mkuu uko deep! Hapo umesema kweli tupu
 
Back
Top Bottom