Concise and overall assessment of 2015 election (Taswira kubwa ya uchambuzi wa uchaguzi 2015)

Asante kwa uchambuzi ambao umenipa insights nilizokua sijazifikiria sana,hususan kuibuka kwa taswira ya "ukanda", kwa sababu ya ugeni wangu kwenye mambo ya siasa . Pamoja na hili, naona ungeboresha tathmini yako kwa kuangalia components zote za zoezi lote. Hizi ni kwa haraka haraka attributes za wapiga kura, wapigiwa kura, usimamizi wa uchaguzi,sheria na muktadha mzima ambamo uchaguzi huu umefanywa, na zinginezo. Matokeo ya tathmini ya hivi itatuwezesha kutambua maeneo mengi, kama si yote, yanayohitaji marekebisho.
Nakushukuru kwa kuona umuhimu wa uchambuzi huu katika kuandaa taifa letu la baadaye. Sasa tuungane kumwomba Dr Slaa aanzishe chama kitakachosaidia nchi yetu kurudisha umoja wa kitaifa na kendeleza vita dhidi ya ufisadi. Niatalifanyia kazi ombi lako la kuangalia nyanja nyingine za taswira za uchaguzi wa mwaka huu. Niliamua kujikita katika taswira tatu ambazo niliziona kuwa kubwa na zitasaidia watu kama Slaa na Wariona kutusaidia kuifanya nchi yetu iwe bora na yenye demokrasia ya kweli siyo ya usanii.
 
Mbowe ana viashiria vyote vya udikiteta. Anachotak yeye ndani ya chama ndiyo sera ya chama. Kama unahitaji kukumbuka inaweza kukuaidia kujua jinsi alivyoshughulikia mgogoro wake na Zito Zuberi Kabwe. Watu ninaowajua na nisiowajua walimsihi sana Mbowe asimfukuze Zito, lakini aliziba mawe masikio yake. Akasema over his dead body. Yeye akiamini kuwa ule ndiyo uongozi imara. Uongozi usiozingatia ushauri bora kwa manufaa ya chama ni udikiteta. Katika kumwingiza Lowasa Chadema alifanya kwa utashi wake binafsi. Waliopinga uamui wake walilazima kukiacha chama na yeye akabaki akidhani, kwa akili yake anaimarisha chama. Kusikiliza ushauri ni jambo bora lakini kuujua ushauri wa busara kunahitaji busara pia. Kwa bahati mbaya watu wanaosikiliza ushauri wenye bura hujishusha, hajikwezi, Mbowe hajui kujishusha anajua kujikweza. Superiority complex huwapata hasa watu inferiors kwa sababu wanataka kufidia mapungufu yao. Mbowe anapungukiwa. Ana elimu ndogo. Kila anayemshauri hasa akimzidi kiwango cha elimu anajenga defence machenisim
Mkuu wali usikasirike, unajua majadiliano yanahitaji utulivu wa moyo. Athari ya Dr. Slaa kusalitiwa na Mbowe ipo. Sababu ni Slaa kutaka chama kiendelee na misingi yake ya kupiga vita ufisadi huku Mbowe akifikiria njia ya mkato ambayo hana uhakika nayo. Tujadili tu ndugo Tanzania ni yetu sote. Hata kama matokeo yanaumiza lakini bado majibu ya uhakika kwa maswali magumu yanahitajika.
 
Huu uchaguzi huwezi kuuchambua kwa matokeo feki ya NEC utajikaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Hata voter turnout ilikuwa more than 90% wao wanadai 67%. Uongo wa mchana kweupeeee
Nimeanza kwa kusema kuwa kama tukichukulia kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki. Hata katika mazingira ya kuchakachua, msokumo wa kikanda unaonekana.
 
Back
Top Bottom