Computer yangu Intel inagoma ku-display

Computer yangu Intel inagoma ku-display

Nzowa Godat

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2011
Posts
2,785
Reaction score
824
Nina computer aina ya intel ni hii mitumnba ya computers 4 Africa, inafunguka ndani kwa ndani lakini monitor inakataa ku-display, yaani imepoteza stability kabisa. Naomba msaada namna ya kuirudisha katika hali yake.
 
je una hakika kwamba inafunguka ndani kwa ndani?
umejuaje?. imetoa mlio wa windows startup?

je taa LED ya hdd inaonesha activity -BUSY?. Au haioneshi chochote?

je? unapobonyeza button ya ON. monitor haishtuki hata kidogo?
 
Ndiyo inafunguka mlio unasikika na ukizima umeme kwenye monitor na kuunganisha tena ina-display na kuzimika tena ghafla.
 
Ndiyo inafunguka mlio unasikika na ukizima umeme kwenye monitor na kuunganisha tena ina-display na kuzimika tena ghafla.

hiyo computer ina OUTPUT ngapi za video? kama ina output zaidi ya moja. jaribu nyingine.

je wakati unapozima na kuwasha monitor inapowaka hai display maneno yoyote kama vile resolution is out of range or not optimal?

jaribu monitor nyingine.
jaribu cable nyingine.
jaribu ku chezesha waya kwenye hiyo port ya vga/divi kwa upande wa cpu naupande wa monitor.
kama monitor ina input zaidi ya moja. hakikisha ume set intput husika.

kama resolution is out of range itabidi utafute monitor ya chogo ili kubadili settings.
 
Nashukuru ngoja nijaribu kutokana na maelekezo yako then nitatoa taarifa.
 
Kwenye monitor yenye kisogo inafunguka bila shida. Basi tatizo halipo kwenye cpu, asante sana.
 
Back
Top Bottom