Mchekeshaji Mchopanga na Nyota ya Rais Zelensky wa Ukraine

Maabara4

Member
Dec 14, 2020
75
117
Kutoka WhatsApp Group nimepata hili.

=====

Kadri ya Rais Lovodymyry Zelensky wa Ukraine na Uteuzi wa Comedian Michopanga (Juma Chikako kuwa DC Rorya

Wakati vijana wengi wakikosoa bila hoja, kwa misukumo ya ukada wa vyama na agenda binafsi za kuonesha Rais Mhe SSH siyo makini..

Wote wanaohoji juu ya Mchopanga, eti kuwa comedian anapungukiwa sifa. Naomba mchukie habari ya Rais wa nchi ya Ukraine Mhe Zelensky. Huyu alikua comedian mkubwa huko lakini alipogombea urais aliaminiwa na kushinda uchaguzi kwa hoja zake siyo kwa brand ya vichekesho vyake.

Hivyo nashangaa vijana wa Tanzania baada ya kusherekea vijana wenzetu kuaminiwa tunaanza kuangamizana.

Jamani vijana tupendane, tuwape nafasi waoneshe vipaji na uwezo wao. Kisha wahukumiwe kwa utendaji wao.

Mwisho.

Mungu wabariki wateule wote katika majukumu yao. Wazingatie utawala Bora na sheria za nchi. Watende haki kwa Watanzania wote.
 
Kwa hiyo unataka kusema Chopa Mchopange kwa sababu ya uchekeshaji wake, mama Samia akamuona anafaa kuwa DC wa Rorya?
Ni dharau kiasi gani hii kwa wananchi wa Rorya?

Kuna namna fulani hili taifa limeharibiwa akili na CCM kiasi cha kuona watanzania wote ni kama mataahira.
 
Aisee Nchi imekua rahisi sana yaani usipowaza Urais unakua sio binadamu aliyekamilika.
 
Kwa hiyo unataka kusema Chopa Mchopange kwa sababu ya uchekeshaji wake, mama Samia akamuona anafaa kuwa DC wa Rorya?
Ni dharau kiasi gani hii kwa wananchi wa Rorya?

Kuna namna fulani hili taifa limeharibiwa akili na CCM kiasi cha kuona watanzania wote ni kama mataahira.
Aliratibu ziara za kampeni zote na mama ...nafasi 1 wagombea 3...Wema Mchopanga na Steve sasa akapita Mchopanga .....kulipa fadhila zileee
 
Kutoka WhatsApp Group nimepata hili.

=====

Kadri ya Rais Lovodymyry Zelensky wa Ukraine na Uteuzi wa Comedian Michopanga (Juma Chikako kuwa DC Rorya

Wakati vijana wengi wakikosoa bila hoja, kwa misukumo ya ukada wa vyama na agenda binafsi za kuonesha Rais Mhe SSH siyo makini..

Wote wanaohoji juu ya Mchopanga, eti kuwa comedian anapungukiwa sifa. Naomba mchukie habari ya Rais wa nchi ya Ukraine Mhe Zelensky. Huyu alikua comedian mkubwa huko lakini alipogombea urais aliaminiwa na kushinda uchaguzi kwa hoja zake siyo kwa brand ya vichekesho vyake.

Hivyo nashangaa vijana wa Tanzania baada ya kusherekea vijana wenzetu kuaminiwa tunaanza kuangamizana.

Jamani vijana tupendane, tuwape nafasi waoneshe vipaji na uwezo wao. Kisha wahukumiwe kwa utendaji wao.

Mwisho.

Mungu wabariki wateule wote katika majukumu yao. Wazingatie utawala Bora na sheria za nchi. Watende haki kwa Watanzania wote.
Acha upumbavu wa kupindisha hoja. Kwani watu wanahoji kwa sababu ni ''comedian''? Watu wanaohoji ni sifa gani aliyonayo zaidi ya ''uchekeshaji'' mpaka akachaguliwa.
 
Bavicha mna wivu na haters sana
Magufuli alipokuwa anaharibu nchi CCM mliogopa kusema chochote mpaka akawageuza mbele nyuma. Sisi tumehoji, tunahoji na tutahoji kila pale kiongozi anapofanya sivyo kwa sababu tunajua athari zake. Na wala sisi siyo Bavicha wala wanasiasa.
 
Kamanda meza Panadol na maji baridi. CCM bado itaitawala sana nchi hii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom