harakat
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 2,887
- 1,350
Rais wa CWT, Makamu wa Rais wa CWT, Katibu Mkuu CWT na Mweka Hazina wa Taifa wa CWT. Ninapenda kuwajulisha kuwa nimepokea barua mbili kwa njia ya baruapepe kutoka Tamisemi.
Barua ya Kwanza imetoka kwa Katibu Mkuu wa Tamisemi iliyokiri serikali kupokea hoja saba za CWT zilizowasilishwa tare he 21 Februari katika kikao kilichoitisha na Mhe Simbachawene Mbunge na Waziri wa Nchi Tamisemi.
Barua ya pili imeandikwa na kusainiwa na Mhe Simbachawene Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi na kunakilishwa kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mhe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao hicho kimetujulisha kuwa kutakuwa na kikao cha Pili cha mazungumzo kati ya serikali na CWT tarehe 16 Machi saa 4 Dodoma ili serikali itoe mrejesho wa hoja saba za Chama.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2016) kabla ya Chama cha wafanyakazi kutumia Sheria yoyote ya kazi lazima ihakikishe kuwa majadiliano na mwajiri yameshindikana kupata suluhisho la matatizo ya wafanyakazi.
Kifungu hicho pia kinapaswa kusomwa na Kifungu cha 26 cha Sheria ya Majadiliano ya Pamoja kwenye Utumishi wa Umma. Kwa kuzingatia vifungu hivyo vya Sheria nilivyovitaja hapo juu, CWT haiwezi kutangaza mgogoro na serikali tarehe.1. 3.2017 kama ilivyoamuliwa na Baraza kwa kuwa mazungumzo na mwajiri hayajakwama na hatujui tutakachopewa na mwajiri kwenye kikao kijacho.
Tamko la Baraza la Taifa la kutangaza mgogoro linaweza kutekelezwa ikiwa mazungumzo ya tarehe 16.3.2017 hayatakuwa na tija. Kwa sasa ninashauri kuwa kwa tarehe 1.3.2017 Rais wa CWT awajulishe walimu kuwa tunasubiri kikao cha tarehe 16. 3.2017 kabla ya kuamua kutangaza mgogoro au la.
Madai ya walimu yakitekelezwa na mwajiri hakutakuwa na sababu ya kutangaza mgogoro na mwajiri. Maelezo haya ni ushauri wangu wa kitaalamu ambayo nimeona niitoe kwa kuwa barua zimetumwa kwenye baruapepe yangu na nimezisoma na kukiri kuzipokea.
Pia nimezingatia kuwa Rais anaweza kuulizwa maswali kwa leo au kesho ili atakachosema iendane na matakwa ya Sheria.
Ni mimi Mwl Ezekiah T Oluoch Naibu Katibu Mkuu leo tarehe 28.2.2017 saa 12:15 jioni