Cold war (chadema vs ccm) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cold war (chadema vs ccm)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Oct 29, 2010.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  VITA BARIDI-COLD WAR(CHADEMA vs CCM)

  Ni Jumapili ya terehe 24/10/2010 saa 5 asubuhi niko mezani najiandaa kuandika makala ya kueleza maoni yangu kuhusu mdahalo uliofanyika jumamosi ya tarehe 23/10/10 katika ukumbi wa Movenpick hotel saa 1.00 jion hadi saa 3.00 na Kurushwa moja kwa moja na kituo cha televishen TIV ukimhusu Dr.Wilbroad Slaa (rais mtarajiwa wa Tanzania)
  Kabla sijashika kalamu na kuanza kuandika ninakumbuka kuwa nina wajibu mzito wa kuwakumbusha watanzania kuwa Dr.Slaa ndiye Rais anayeweza kukidhi haja za watanzania walio wengi, na Chadema ndio chama pekee chenye uwezo wa kutufikisha kwenye nchi ya Ahadi
  Wajibu huu nilijipa rasmi, mara baada ya Dr Slaa kutangazwa na chama chake kuwa ndiye mgombea urais mwaka 2010. Tangu wakati huo hadi sasa nimeshatuma sms kwa watu takribani 9800 (ninaowajua na nisiowajua). Kila siku lazima nibuni ujumbe mpya wa kunadi CHADEMA (kwa kusoma ilani yao au kwa kusikiliza sera zao majukwaani na kwenye vyombo vya habari.
  Sifanyi kazi hii kwa kuwa ni mwanachama wa CHADEMA, wala kwa kuwa ni kiongozi wa chama; Hasha! Nafanya sehemu yangu kama raia wa kawaida kabisa wa Tanzania ninayetaka mabadiliko. Nina hakika kabisa sio mwenyekiti wa shina (chadema tunaita msingi), wala katibu wa chama wa kata anayejua kazi ninayoifanya, ila nina hakika Watanzania wanajua. Maana sifanyi hivi kuwaridhisha viongozi wa chama bali kuwakomboa Watanzania. Simaanishi napuuza viongozi wa chama; HASHA, naheshimu Watanzania. Kwa maana viongozi wa CHADEMA ni muhimu ila Watanzania ni muhimu zaidi.
  Wakati nikitafakari nikagundua kuwa wangekuwepo watu 4500 wenye mawazo kama yangu (ya kueneza sera za chama kupitia ujumbe wa simu), hadi kufikia jana ujumbe huo ungekwishawafikia Watanzania miliono 44.1, idadi ambayo inazidi jumla ya watanzania wote, maana takwimu zinaonesha idadi ya watanzania inakadiriwa kuwa milioni 40. Kumbe baadhi ya watu wangepata ujumbe zaidi ya mara moja.
  Ila hoja yangu leo si kujadili ujumbe wa simu naotuma maana , bali nimelazimika kuutaja maana mojawapo ya ujumbe nazotuma ndio zimeibua vita hivi baridi.
  Nikiwa mezani kabla sijaanza kuandika kuhusu mdahalo wa Dr.Slaa, naanza kwa kuhubiri HABARI NJEMA kwa Watanzania kupitia ujumbe wa simu. Ujumbe unafika na response zinatokea. Ujumbe niliotuma siku hiyo ulikuwa ni nukuu ya majibu ya Dr., Slaa aliyotoa kuhusu sera ya CHADEMA ya elimu ya bure.ujumbe ulisema “ni upuuzi rais kupanda ndege kwenda kunywa chai na Obama halafu aseme elimu ya Bure haiwezekani. Elimu ya bure inawezekana kama rais akiamua kula mhogo ikulu lakini watoto wetu waende shule”
  Baada ya ujumbe huo rafiki yangu mmoja ambaye yeye ni CCM typical akanijibu na ndipo vita hivi vya maandishi vilipoanza. Ilikuwa hivi;
  CCM: Dr.Slaa ni mropokaji,mgomvi, na anatukana vyombo vya ulinzi na usalama. Anataka damu imwagike ili mradi tu aingie ikulu. Tumkatae kuigeuza nchi yetu Somalia. (sms hii iliwahi kutumwa kwa Watanzania kupitia namba zisizojulikana; hivyo alichofanya yeye ni ku-forward.)
  CHADEMA: Huo ni utapiamlo wa fikra, sijaelewa ccm mnabishana na kipi kati ya HOJA au MTOA HOJA. Unapoeleza Dr.Slaa ni mropokaji eleza ameropoka nini, wapi na lini. Na kama amewatukana (ccm), mmechukua hatua gani? Kama ni kupinga pingeni hoja zake sio kuzusha mambo ya uongo. Hamuthubutu kumpinga Dr.Slaa maana nmajua anachoongea ni ukweli mtupu (facts).
  CCM:Nilimsikiliza siku moja nikiwa Moshi, akasema atafuta kodi zote na mimi kama mchumi sikubaliani nae maana hata Marekani, China na mataifa mengine makubwa yanatoza kodi, maana vyanzo vingine havitoshelezi. Sasa yeye akifuta kodi Tanzania si itakuwa ombaomba kwa kila nchi. Nchi hii inapaswa kuongozwa na mchumi kama Kikwete.
  CHADEMA:Sina hakika kama umekurupuka au hukumsikiliza Dr.Slaa kwa makini. Na hilo halinishangazi maana hata viongozi wengi wa chama chenu ni wavivu wa kufikiri. Huwa wana kawaida ya kusikiliza hoja kijuujuu then wanaanza kubishana bila kuelewa. Wewe kama msomi unapaswa usikilize hoja kwa makini kabla hujaamua kubishana. Kubisha HOJA usiyoielewa vyema ni kuibua VIOJA.
  Kuhusu kauli ya Dr.Slaa, hakusema atafuta kodi zote (nakala ya hotuba hiyo ninayo), bali alisema atafuta baadhi ya kodi zinazomwumiza mtanzania na ambazo hazina maslahi makuba kwa taifa. Kwa mfano kodi ya pembejeo za kilimo, na kodi katika zana za ujenzi. Na baada ya kufuta kodi hizo ataelekeza nguvu kwenye kodi zenye maslahi makubwa kwa taifa, ikiwa ni pamoja na kodi katika migodi ya madini.
  Haiwezekani kodi ya VAT katika vifaa vya ujenzi iwe 18%, ushuru wa mazao uwe zaidi ya 10% ya anachokipata mkulima maskini wa Namtumbo, halafu kodi kwa mabepari wanaochimba madini iwe 3%, then umsifu eti rais ni mchumi, aina hiyo ya uchumi hata kuzimu haipo.
  CCM: (kimya)
  CHADEMA:Alichokisema Dr.Slaa (rais anaesubiri kuapishwa) ni kuwa atapitia upya mikataba yote ya uwekezaji, hususani katika sekta ya madini na kufix upya utaratibu wa kodi. Ghana wawekezaji wa madini wanalipa serikalini 40% ya faida wanayoipata. Hapa kwetu serikali inaambulia 3% na wawekezaji kubeba 97%. Hiyo ndio serikali ya rais unayemsifia mchumi ambaye sina hakika kama fikra zake zinamtosha yeye peke yake (licha ya kuwatosha watanzania), maana naamini hata konda wa daladala za Pugu hawezi kukubaliana na upuuzi wa sisi wazawa kupata 3% na wageni kubeba 97%.
  Zana za kilimo kutoka nje ya nchi zinatozwa kodi kubwa, hali inayopelekea wakulima kushindwa kumudu gharama, na kuishia kulima kilimo kisicho na tija cha jembe la mkono. Halafu at the same time serikali bila haya inahubiri KILIMO KWANZA. Huu ni wendawazimu na mgando wa mawazo. Sasa wewe kama mchumi (rafiki yangu huyo amesoma uchumi), nieleze kodi unayosema isifutwe kwa kuwa inaendeleza nchi ni hii ya kuwanyonya wakulima maskini wa Tanzani na kuendekeza mabepari?
  CCM: (Badala ya kujibu swali akakimbia hoja na kuibua Vioja) akasema: mimi namsubiri rais wangu Kikwete aingie madarakani halafu tuone huyo mlalamikaji atafanyaje. Kwanza hawezi kuongoza nchii maana ana maneno mengi kuliko vitendo.
  CHADEMA: Kwanza hujajibu swali la msingi bali umekurupuka na kutoa hoja mufilisi, ambayo haina mashiko. Nimeekuuliza wewe kama mchumi, pamoja na rais wako (anayemaliza muda wake) ambaye unadai ni mchumi pia, niambieni nchi hii itaendelea kwa kutegemea vijisent vya wakulima maskini wa Mpanda na Peramiho? Kiongozi bora siku zote anatafuta njia za kumsaidia mwananchi wake na si njia ya kumnyonya.
  Dr.Slaa atafuta kodi zote zinazomwumiza mwananchi na kutilia mkazo kwenye vyanzo vingine vya mapato bila kumwumiza mwananchi.
  Ama kuhusu hoja ya Dr.Slaa kuwa na maneno mengi kuliko vitendo, nadhani wewe kama msomi you have to talk facts. Eleza hayo manenoi ni yapi na kwanini unadhani hawezi kufanya vitendo.
  Labda kwa kukusaidia ni kuwa Dr.Slaa (rais mteule wa Tanzania) anachohubiri ni sera. Na kwa kawaida SERA duniani piopote ni maneno. Sera zikifanyiwa utekelezaji ndipo zinakuwa vitendo. Kwa maana hiyo ili sera ziwe vitendo zinapaswa kufanyiwa utekelezaji.
  Dr.Slaa kwa sasa hawezi kuziweka sera zake kwenye vitendo maana yuko nje ya dola. Lakini siku chache zijazo utaziona sera hizo zikiwa kwenye vitendo, maana bado siku saba ashinde uchaguzi, na hazitazidi siku 14 kabla hajaapishwa. Kwa hiyo kama unataka kuona maneno ya Dr.Slaa yakibadilika kuwa vitendo MPE KURA YAKO, then within two weeks you will prove that Dr.Slaa is the man of action.
  CCM: (kimya)
  CHADEMA: Mbona kimya? Waingereza husema silence means YES. Kwa hiyo asante kwa kuwa umekubali kumpa kura Dr.Slaa. Mchague Dr.Slaa na wabunge makini wa CHADEMA kwa MABADILIKO YA KWELI na UHURU WA KWELI.
  Na huo ndio ukawa mwisho wa vita vyetu baridi (vita vya maneno) vilivyodumu kwa takribani saa moja. Sitaki kuwa mwamuzi (judge), maana hiyo ni kazi ya wasomaji, ila nadhani CHADEMA ilishinda.
   
Loading...