Coastal Union vs Simba s.c. Live updates

Wazee wa dhulumat, madai ya ukweli yanaenda hadi fifa mbona ya Basena hatujayasikia? Tunajua Yanga Imeamuriwa na fifa iwalipe Njoroge na Papic, na Muhindi atajuta kuijua Yanga mwaka huu
Ya Moses Basena haya hapa chini

Basena aishitaki Simba CAF

Majuto Omary

ALIYEKUWA kocha mkuu wa Simba, Moses Basena ameliandikia barua Shirikisho la Soka Afrika (CAF) akidai klabu hiyo imlipe dola 72,000 (sawa na sh 112.3 milioni) kwa sababu ya kuvunja naye mkataba.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Uganda, Basena ambaye hivi sasa anaifundisha klabu ya Express ya nchini humo alisema kiasi hicho kinaweza kuongezeka kwa sababu hajaorodhesha gharama za madhara aliyoyapata baada ya klabu ya Simba kuvunja naye mkataba.

Basena alisema tayari ameishawaandikia barua CAF na wamemtaarifu watalifanyika kazi suala hilo.Alisema pia amelitaarifu Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) ili kusimamia suala hilo na kufungua kesi katika mahakama ya Tanzania kwa ajili ya kupata haki zake.

Basena alisema kwamba hajafurahia jinsi klabu ya Simba walivyolishughulikia suala la madai ya malipo yake huku akisema walimuambia watalimpa madai yake kupitia kwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed Mkwabi, lakini hawajafanya hivyo.

"Nina matumaini kwamba suala hili litamalizwa kwa amani, lakini natambua kuwa viongozi wa Simba walikuwa wakinichezea mchezo mchafu na mimi sikuwa nataka kuwashitaki CAF au kufungua kesi mahakamani, lakini nimechoka ahadi hewa ndiyo maana hivi nimeamua kutafuta njia nyingine za kupigania haki zangu,"alisema Basena.

Alisema kuwa haamini jinsi klabu ya Simba inavyolishughulikia suala la maslahi yake kwa sababu alifanya nao kazi vizuri, lakini anashangaa wamebadilika wakati aliiacha Simba ikiwa juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.Basena ambaye aliinoa Simba kwa miezi saba alisema kwamba klabu ya Simba haikumpa taarifa mapema ya kuvunja naye mkataba na kumchukua kocha anayeinoa Simba hivi sasa Milovan Cirkovic kutoka Serbia.

Tayari Kamati ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) inayoshughulikia Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji imesema haikuwa na mkataba wa Basena uliosajiliwa TFF kama kanuni na taratibu zinavyotaka kwa hiyo Simba na Basena ndiyo watakaolimaliza suala hilo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Alex Mgongolwa, kocha Basena alifanya kazi nchini kinyume cha sheria na alikuwa hana kibali cha kufanya kazi nchini.

Mgongolwa alisema Basena na Simba walikuwa wameingia mkataba bila kufuata sheria.

Simba walivunja mkataba na kocha Basena baada ya kocha huyo kushindwa kuipatia Simba vyeti vyake vya ukocha kama walivyokubaliana. Hata hivyo Basena alipeleka vyeti vyake Simba baadaye wakati tayari Simba ilikuwa imeishaamua kuachana naye na kumchukua kocha Milovan.

Baada ya uongozi wa Simba kupata vyeti vya kocha Basena ulisema kocha huyo aliwadanganya kwa sababu awali aliwaambia kuwa ana shahada ya ukocha, lakini vyeti alivyowapatia Simba vinaonyesha ana diploma.

Msemaji wa FUFA, Rogers Mulindwa akilizungumzia suala hilo alithibitisha kuwa ni kweli Basena amewapa taarifa za madai yake na kuwataarifu CAF.

Mulindwa alisema FUFA inamuunga mkono Basena na tayari kocha Basena amefungua kesi katika mahakama kuu ya Uganda.

Naye Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa hawana taarifa za Basena kuishitaki Simba katika Shirikisho la Soka Afrika CAF wala mahakamani ila watalishughulikia suala hilo kabla halijafika mbali kwani walikuwa na mkataba na Basena ambao ni baina yao Simba na kocha huyo.

Basena aishitaki Simba CAF
 
Ya Moses Basena haya hapa chini

Basena aishitaki Simba CAF
Tuesday, 16 October 2012 11:48

CAF wamesemaje sasa kuhusu hayo madai maana FIFA tumewasikia walichosema kuhusu madai ya Njoroge na Papic, na unakijua!!
 
Back
Top Bottom