Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,353
Kikosi cha Coastal Union Wagosi wa Kaya kitaondoka jijini Tanga Moshi kwa ajili ya kuweka kambi ya siku kadhaa kabla ya kukutana na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao jijini Arusha.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi Nassor Ahmed Binslum, timu imeamua kuelekea Moshi kutokana na hali ya hewa ya Mji huo kufanana na ya Arusha hivyo itasaidia wachezaji kuzoea hali ya baridi.
Kitu kingine alichozungumza Binslum ambapo walishauriana na kocha mkuu wa Wagosi, Hemed Morocco ni kuwafanya wachezaji kutoka nje ya mkoa wa Tanga kwani tangu walipoanza kukaa kambini hawajawahi kucheza nje ya mkoa huo mbali ya kufanya vizuri kwenye mechi zote za majaribio kitaifa na kimataifa.
Zaidi: COASTAL UNION: Kikosi cha Coastal Union kuweka kambi mjini Moshi.