SI KWELI CNN wametangaza kupatikana kwa Polepole

SI KWELI CNN wametangaza kupatikana kwa Polepole

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu

Kuna hii Taarifa nimeikuta katika mtandao wa Facebook inaeleza kuwa CNN wamechapishwa kwamba Polepole amefariki.

Polepole.jpg
 
Tunachokijua
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye ambaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba. Usiku wa kuamkia Oktoba 06, 2025 Polepole alivamiwa na kutekwa katika makazi yake na kupelekwa kusikojulikana.

Madai

Kupitia mtandao wa Facebook mtumiaji mmoja amechapisha taarifa Januari 08, 2025 ikiwa imeambatana na 'link' ya Youtube ikieleza kuwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole amepatikana amekufa na CNN imeanika mauaji hayo huku akisafirishwa Ikulu.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia kwa kina Taarifa hiyo na kujirirdhisha kuwa si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya utafutaji wa maneno muhimu umebaini kuwa hakuna chanzo chcoche cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo. Aidha chombo cha habari cha CNN kilichotajwa pia katika Taarifa hiyo hawajachapisha Taarifa yoyote kumuhusu Humphery Polepole hivi karibuni.

Kiungo (link) iliyoambatanishwa katika taarifa hiyo ambayo ni ya Youtube ukiibonyeza inakuja video tofauti inayomuonesha mwanaharakati Mange akiongelea masuala tofauti na hakuna mahali panapoeleza uthibitisho wa kufariki kwa Polepole.

Hivyo hii ni aina ya Upotoshaji wa kichwa dhidi ya maudhui, kichwa cha habari kinaeleza tofauti na kili kilichopo kwenye link ya Youtube iliyoambatanishwa.

Kwa mujibu wa jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam mara ya mwisho walito taarifa Oktoba 06, 2025 wakieleza kuwa wanafuatilia taarifa za Polepole kutekwa hivyo hakuna taarifa mpya hadi sasa kumuhusu.
Back
Top Bottom