Clouds Tv na TCRA nani mwenye mamlaka?

Baba Wawili 2012

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
413
335
Habari wana Jamvi,

Binafsi naona kuna haja ya kuangalia prorgram za Clouds TV na kama mamlaka zinazopaswa kusimamia ustawi na maadili ya watu wake wanafanya kazi zao kwa ufanisi. Mimi naona kama TCRA aina meno ya kutosha kusimamia media hizi na kuwapa onyo au karipio ambalo halitafanya wamiliki au watangazaji kurudia rudia aina ya makosa yenye kumomonyoa maadili au yenye kuudhi au kuumiza kundi fulani katika jamii.

TCRA yapaswa kufanya maamuzi yenye kuakikisha hawa wenye media wanapotenda kosa alipaswi kurudiwa maana inaoynyesha kutojali kama hii clouds media iko juu ya sheria.

Nina matukio mawili yalionifanya nije na uzi huu:
  • Ukiondoa program ile waliomuoji shoga ikatikisa nchini... na adhabu ikatolewa, ilionekana kama adhabu ni yellow kadi na mchezo unaendelea. Hivi karibuni walikuwa na kipindi cha maagizo ...kinarushwa mapema sana cha mausiano...muda wa kipind hiki ni kati ya saa mbili hivi mapema sana nafikiri (wenye kujua muda wanaweza kuweka sawa) kilinighfirisha mbele ya familia yangu sebuleni wakizungumzia umuhimu wa shanga za kiononi za mwanamke wakati wa mapenzi.......ilikuwa igizo fulani mdada anajaribu kumshwishi kijana kuwa amkubalie mke wake atumie shanga....sikubalikiwa na kile kipind huku na nikiwa na watoto wangu wadogo hapo sebulen na mama mkwe. nilipotezea na nilitamani nije niandike humu.
  • Sasa hii ya jana ndio imenitoa shimoni kuja humu, kipindi kina jina lakini kinaongozwa na sudi brown cha Shilawdu (shirika la wambea duniani) walirusha habari na video ya kupigwa katika fumanizi la ngono na mke wa mtu. Kijana anaeitwa Abubakari mzuri alionyeshwa katika video akipigwa na mpaka kuumizwa na damu katika tukio hilo linasemekana ni fumanizi. Hapa ndio nataka kujua: Huu si udhalilishaji kwa huyu kijana, je media au chombo chochote cha habari kina haki ya kupoteza amani ya kiakili ya jamii au kikundi au familia fulani kwa mambo ambayo yalifanyika faraghani, hivi Clouds TV au TCRA wanajua ile video iliyoonwa nchi nzima kuwa hata watoto wa bwana Abubakari ambao hawajazaliwa watakuja kuiona? Hivi ndio malengo ya habari? Hivi Clouds TV awajui sheria ya nchi kuwa Body assault ni kosa la jinai, hata muarifu wa aina yeyote iko wazi kuna vyombo vya sheria vinahusika kumchukulia hatua, ikaweje video inarekodiwa mtu anapigwa mpaka dama na majereha yanatoka eti kwa sababu ya habari. Kile kipindi akifai nashauri kama ni lazima kiwepo basi kibaki katika audio/redio tu sio TV. Ni against social right ya watu na nchi yao. Abubakri akufumwa na mwanafunzi alifumaniwa na mke mtu, ambae ni mtu mzima na akili zake hakuna taarifa za kubakwa. Waliongea wakakubaliana kufanya yalio yao, iweje udhalilishaji ule ukawa na bia kiasi kile? Eti watoto shangazi ndio wakampige wafumaniwa ....hivi wale ni kabila gani, mtoto akampige bwana wa shangazi yake....?
  • TCRA lazima wa-act role yao katika mambo ya media hasa tv za bongo....maadili ni zero. Watoto wetu, watoto wenu ndio wanaoaribika.....sasa hivi ukifungia mtoto ndani na tv tu inatosha kumuharibu sio kama sisi zamani unaambiwa usiende kucheza kwa kina fulani wanatabia mbaya na usipoenda umepona.
  • TCRA angalieni vipi gani ninarushwa muda gani, Nyimbo za vichupi, mauno ya hatari, zinarushwa mchana kweupe...kwa ujumla kuna tv huwezi kuweka kama uko na mtoto au wakwe mkiangalia hata iwe saa 4 asubuhi....nchi za wenzetu nyimbo, program zenye matukio yasiofaa kwa watoto huanza kurushwa saa 4 za usiku na kuendelea....
  • TCRA fanyeni kama DSTV kuna strictly program unaset katika tv kwa move au program aziko relevant na watoto....kwa loca tv zetu lazima yale maigizo, vipindi viwe na vielelezo kwa kuweka wazi umri upi unafaa kwa kipindi kipi..haya ndio maendeleo.....sio sheria za TCRA mpaka wananchi watoe povu wakati hata nynyi mnaona....CLOUDS TV inataji kuangaliwa kwa jicho la tatu....fanyeni evaluation ya vipindi kadhaa haviko kwenye njia bora ya vizazi vyetu vinavokuwa.
Samahani kwa kuandika kama nahubiri wadau nilijkuta nahemuka sana kwa tukio la jana..Fikiria kila mwanaume atakefumqniwa aanikwe kama wa jana na media zetu.
 
Kutembea na mke wa mtu, au kuanikwa kwenye media lipi ni jambo kikubwa?

Vijana wa kiume wanapenda mteremko sana, itapendeza kila kitu kiwe kwa uwazi hivyo hivyo ili wajue madhara ya kutembea na mke wa mtu.

Tena safi wangemfokoa kifurushi kabisa, maana bila hivyo vijana hawaelewi.
Mke wa mtu sumu, wao vijana wanasema, Eti geto ni maziwa, ngoja ukute mtindi.. Dawa ni kuwafokoa tu,

Na sasa hivi nataka nitengeneze ky ya bamia made in Tanzania kwa ajili yao.
 
Unaanzajeanzaje kuangalia shit kama hizo, hao wameshazowea kuonyesha mambo yao, nakusihi angalia vipindi vitakavyokufanya ujifunze na uburudike bila bugudha,TCRA wanajua kazi yao ila wanakuwa weak kuwapa onyo
 
Ila mleta mada kipindi cha Sudi brown kina kosa gani?

Kwa upande wa igizo la Mahusiano nakubaliana na wewe kabisa, wale wahusika kuna maneno huyatamka waziwazi bila kuzingatia mda wanaorusha kipindi chao.

Kwa upande wa kipindi cha Qwisaar na Soud mimi sioni tatizo kwani kinaanza saa tatu usiku hadi saa 5. Half pia hawakuonyesha sehemu yyte mbaya ktk ile clip zaid ya pale abuu alikokua akipigwa migumi

Lakini Hakuna sehemu wamemuonyesha yule mwanamke au hata abuu akiwa naked, nashindwa kuelewa pale ulikwazika kitu gani?
 
He he he! Mzee umepigwa somo la shanga wakati uko na mama mkwe! Hatari sana.
Huyu Naye Atakuwa Ni Wale Wale, Wewe Uko Sebuleni Na Watu Wa Heshima Unatune Clouds Tv Ni Ujinga.Mimi Mama Akiwa Home Hata 5 Select Amma Eatv Siangalii.Ni Tbc, Itv Na Tv1 Tu.Anyway Binafsi Sioni Tatizo Maana Shilawadu Inaanza Saa 3 Usiku Ni Sahihi Kabisa.Na Kuna Michannel Kibao Kwanini Unakomaa Tu Na Hiyo Tv,binadamu Kazi Kweli
 
Back
Top Bottom