GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Kwanza nianze kwa kusema kuwa najua Mimi ni Mtu mdogo sana kuweza kuwaamulieni CMG nini cha kufanya ILA natambua kwa jinsi CMG mlivyo Watu wema, makini na wastaarabu sana na ambao huwa mnapenda mno kutusikiliza sisi Wadau wenu naamini hili ombi langu Mimi GENTAMYCINE pamoja na Wadau wengine watakaokuja kuchangia mtatusikiliza.
Natambua kwa sasa Mtangazaji mahiri kabisa wa Michezo wa Clouds Media Group ( Clouds fm na tv ) Kamarada wetu Alex Luambano amesimamishwa Kazi kwa kosa la kumtangaza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul C. Makonda katika hafla fulani kitendo ambacho nimeambiwa kuwa kiliwakera sana si tu Mabosi zake bali hata akina TEF na MOAT ambao walipitisha maazimio ya kutopewa coverage ya aina yoyote kwa Mkuu huyo wa Mkoa.
Clouds Media Group binafsi kwa ninavyomjua Alex Luambano sidhani kama kweli alifanya kile kitendo kwa makusudi au kwa kujipendekeza kwa RC Makonda bali ninadhani kuwa siku ile alipitiwa tu na isitoshe hata nyie mliopo nae hapo mjengoni mnajua kuwa Alex Luambano hana record mbaya yoyote ile.
Mimi nikiwa kama Mdau wenu mkubwa sana wa Vipindi vyenu vya Michezo Clouds fm na tv niseme tu kuwa kutokuwepo katika Kipindi kwa Kamarada wetu Alex Luambano kiukweli tunakosa ladha fulani kwani Luambano ana ' mvuto ' wa aina yake hasa awapo katika Kipindi na kiukweli uwepo wake ukichanganya na ' Chemistry ' nzuri ya Makamarada wengine akina Shafii Dauda, Issa Maeda, Yahaya Mohammed, Edgar Kibwana, Fatuma Likwata na Mbwiga Mbwiguke hukifanya Kipindi cha Michezo kuwa kizuri na kichangamfu mno.
Tunajua kuwa Alex Luambano kweli amekosea kwa alichokifanya ila tunawaombeni Clouds Media Group na hapa ninapoandika huu uzi nimepiga magoti kabisa huku nikitiririka hivi kwa ku type na machozi ya kumuombea Msamaha Kamarada wetu huyo na pia tunaomba nyie Clouds pia mkamwombee msamaha kwa akina TEF na MOAT ili kwa ujumla wenu muweze kumsamehe kwani alikengeuka tu na hakukusudia.
Natanguliza shukurani zangu kwenu Uongozi mzima wa Clouds Media Group na naamini kuwa mtasikiliza hili ombi langu ILA naomba radhi pia kama nitakuwa nimekosea kwa kusema Mtangazaji wenu Alex Luambano amesimamishwa Kazi na kumbe ikawa siyo kweli kwani sometimes Watanzania huwa tunalishana sana matango pori humu Mitandaoni.
Boss Kusaga, Boss Ruge na Boss Sheba chonde chonde tunawaombeni mumsamehe Alex Luambano kwani tunamkumbuka na tunamuhitaji mno tumsikia akiwa anatangaza katika Vipindi vya Michezo vya Vituo vyenu hapo.
Mwenyezi Mungu awabariki sana Clouds Media Group wote, awapiganie, awalinde na azidi kuwaweka juu Kitasnia na nyie mtabaki kuwa Radio na Tv yangu pendwa muda wote na ninawakubali mno ila mkimsamehe Mtangazaji Alex Luambano nitawakubali kwa kutukuka kabisa.
Akhsanteni na naomba kuwasilisha.