Nimesikia muda si mrefu mnapiga wimbo wa "Tanzania Tanzania Nakupenda Kwa Moyo Wote" . Hongereni sana kwa kutuelewa[emoji122][emoji122][emoji122], inaonyesha wazi kabisa Boss Ruge huwa unapitia JF na usikute ukawa JF member kwani kwa akili kubwa uliyonayo sidhani kama utakosa kuwa member JF [emoji106].
Ombi langu kama itawezekana hata kuanzia jumatatu achana na wimbo Taifa, piga wimbo wetu huu wa Tanzania Tanzania, lakini waimbaji hakikisha wanauimba "kizalendo" zaidi na sio "kisanii" zaidi, ina maana waonyeshe kwa kutumia sauti zao kweli Tanzania tunaipenda, wasirembee sana kwani wimbo huu wa kizalendo hauhitaji kuremba , huu wimbo unatukumbusha kwanini tuitwe watanzania!!
Kwanini tunapaswa kuwa wazalendo, kwanini tuipende nchi yetu. Tanzania Nchi Tamu sana!!!
Hongera sana Chief Ruge.