Clouds FM msiishie tu kuuza Instrumental ya Jet Man

Clouds FM msiishie tu kuuza Instrumental ya Jet Man

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,692
Reaction score
2,098
Wadau,

Jetman ni producer na msanii wa dancehall anayeishi Mwanza aliyewahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na vibao mbalimbali. Msanii huyu anasumbuliwa na maradhi ya mgongo kwa miaka mitano sasa na sasa anahitaji msaada kutoka kwa wadau ili aweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Tshs milioni 12 zinahitajika ili aende India kupata matibabu. Pia wamekadiria kama Tshs Millionj 8 zitatumika kwenye Nauli hivyo kufanya Jumla ya Tshs Million 20 kuhitajika kwa ajili ya matibabu yake haya.

Michango kwa ajili ya matibabu haya imeshaanza kuchangwa ambapo ni Fedha taslimu pamoja na uuzwaji wa Instrumental iliyotengenezwa na Jetman mwenyewe inayoratibiwa na Clouds FM. Pengine Clouds wana nia nzuri ya kuchangisha fedha hizi ila naona kama wangeweza kujiongeza zaidi kuliko kuishia tu kuchanga kwa kuuza instrumental.

Mfano mimi kama Shakir naweza kununua hiyo Instrumental kwa hiyo Tshs 100,000/= lakini nikishainunua naipeleka wapi?? Hizo vocal nitaingiza tu nyumbani mwenyewe mwenyewe halafu inaishia tu hewani?? Kwanini basi kwa kua THT ndio waratibu wa hili zoezi na wanayo studio wasitusikilize sisi wanunuzi wa instrumental tukatengeneza nyimbo kwenye studio yao??

Nilidhani pengine kila anaenunua hiyo instrumental akipata nafasi ya kurecord wimbo wake kwa instrumental hiyo kisha Clouds FM wakatenga muda wakazipiga hewani ingekua poa zaidi?? Sio lazima watumie muda mrefu sana kuzihariri maana wanunuzi wengi sisi sio waimbaji, hivyo hatufanyi mziki biashara kua ni lazima utoke bomba. Hata Waziri wa Sanaa ambae nae amenunua hiyo instrumental Bw. Nape Nnauye sio mwimbaji, lakini tukijisikia tulivyoimba inaleta hamasa zaidi.

Ni ushauri tu wangu tu kwa Clouds FM, kila mwenye Tshs 100,000/= yake msiishie tu kumpa instrumental yake kwenye flash au memory card kisha mchezo uishie hapo, bali muingizeni studio zenu arecord wimbo wake na muupige kwenye mojawapo ya vipindi vyenu. Hii itavutia watu wengi zaidi kujitokeza.

Ni hayo tu,
Nawe pia wanaweza kuchangia kupitia 0757 62 62 07.
Jina ni GODFREY KUSOLWA
 
Back
Top Bottom