Observer2010
Senior Member
- Oct 29, 2010
- 195
- 44
Japokuwa najua ni redio ya kidaku zaidi, ila ni vyema Clouds FM kuwa makini wanapotoa habari zenye umuhimu na maslahi ya Taifa.
Najua kuna mambo mengi tu wanayamislead, ila hapa nitatolea mfano mambo mawili waliyotokea hivi karibuni,
1. Wakati wa mabomu ya Gongo la Mboto, Clouds fm wakatangazia umma ya kuwa Mabomu yanalipuka katika kambi ya Mkuranga.
2. Ilipotokea ajali ya 5 Star maeneo ya Morogoro, clouds fm wakangazia umma kuwa ajali imetokea maeneo ya Kibaha.
My concern ni kuwa kama hawana uhakika wa tukio si waseme watalitolea maelezo ya kina watakapopata uthibitisho wa habari. Huu ni ukiukwaji wa taratibu na taaluma ya uhandishi wa habari.
:smow::smow::smow::smow::smow:
Hii ni redio ya umma pamoja na udaku wao lakini wanatakiwa wawe serious. Kuna wakati wanachemka hadi kupitiliza mtu unajiuliza hawa jamaa wanajua wanachokifanya kweli. Huwa siwasikilizi ila redio yangu ni ya kizamani kwa hiyo wakati natafuta station nyingine huwa napitia frequency zao basi naweza kusikiliza by the way. Lakini kuna kile kipindi cha jumapili kinaitwa njia panda, hicho huwa nasikiliza.
Hii ni redio ya umma pamoja na udaku wao lakini wanatakiwa wawe serious. Kuna wakati wanachemka hadi kupitiliza mtu unajiuliza hawa jamaa wanajua wanachokifanya kweli. Huwa siwasikilizi ila redio yangu ni ya kizamani kwa hiyo wakati natafuta station nyingine huwa napitia frequency zao basi naweza kusikiliza by the way. Lakini kuna kile kipindi cha jumapili kinaitwa njia panda, hicho huwa nasikiliza.
May be alikuwa anamaanisha " the peoples station"...radio ya watu..Kwa ufupi sio clouds peke yenye mapungufu kwenye kutoa taarifa radio nyingi tu za bongo ila tatizo la Clouds inasikilizwa na wengi kasoro hizo ndogo ambazo zinarekebisha ishu kubwa ilikuwa ni taarifa ya ajali iliyotokea huenda mtoa habari wa mwanzo Muimbaji wa taarab mwanahawa Ali huenda alikuwa ameweweseka nakusema vingineKwenye blue ni Kweli?? Hivi inatanagza kutoka Mkoa gani,Mimi nipo TZ lakini mbona siijui.Inapatikana masafa gani na wapi au ni zile redio zilizojaa dar zinazoishia Kibaha.
we unawasikiza wa nn wkt unajua hawako makini? dont waste your time kuwasikiza.
Email address zao ni eti pb@cloudsfm.co na wanatangaza kila siku wakati inatakiwa kuwa pb@cloudsfm.co.tz
Email address zao ni eti pb@cloudsfm.co na wanatangaza kila siku wakati inatakiwa kuwa pb@cloudsfm.co.tz
Huwezi pata hiyo website ni ya zamani. wamebadili na wana website kiboko sana ambayo umeikanusha kwa makosa ambayo ni www.cloudsfm.co hivyo basi ukitaka kuwasiliana na vipindi kama leotena una address leotena@cloudsfm.co Hawa watu to be fair wana vipindi vizuri ukiondoa Jahazi ya sasa ikiwa na Kibonde na wanawake 2 wanaocheka cheka - wote watatu wana hulka ya kujipendekeza na kupindisha ukweli. Wasikilize Dinnah na Gea utafurahi na vpindi vingine ukitoa Jahazi ya sasa.
Power breakfast sio mbaya sana, ila kuna kipindi siku hizi kinaitwa amplifaya (amplifier), hiki ni cha dogo mmoja anaitwa mirlad ayo aliyahama kutoka radio one, ndani yake kuna kipengele kinaitwa 'habari bila wasiwasi na wasiwasi mwabulambo' hicho ukisiliza lazima utapike, jamaa anaboa hakuna mfano, habari zinazopaswa kuwa za kusikitisha yeye anazisoma kama anashangilia vile na lugha ya mtaani inayotia kinyaa, jaribuni kusikiliza kuanzia saa 12 jioni mpaka saa tatu usiku, halafu kipondi chenyewe nadhani hawakufanya utafiti wa kutosha, kuna wakati wanaishiwa habari basi wanafululiza mziki mapak unasahau ni kipindi gani.
Redio ya umma si tbc zamani rtd na uhuru jamani? Hii ni radio ya watu binafsi sio ya umma (serikali).