Jamani wana jamii naomba tuchambue nini maana ya report iliyotolewa na CIA juu ya ukuaji ama ongezeko la watu kwa kiasi kikubwa huku kundi tegemezi likionekana tatizo kwa uhai wa taifa letu ukizingatia idadi ya wenye kuzalisha inaonekana ni ndogo kuliko wahitaji.
Binafsi sina uhakika na takwimu zilizotolewa na CIA ila JE,nini hasa wanachotutaka?na kama ni kutushauri tu,je ushauri wao uko sahihi?
Wanajamii tafadhali tusibeze hili,naomba tujaribu kufanya upembezi staha ili hili liwe wazi kwetu sote.
Hiyo ripoti i wapi??
Kama suala la kuongezeka kwa kasi kwa watu ambayo hawaendani na hali halisi ya huduma za jamii, na hivyo kuongezeka kwa wategemezi, kwa jamii zetu wa Afrika nadhani vyanzo vipo wazi.
Mtu asikudanaye kuwa sisi tunaweza kufuata mifumo ya Ulaya na Marekani ya kupunguza idadi ya watu kupitia uzazi wa mpango. Rasilimali tulizo nazo kama tungezitumia vizuri, bado tunahitaji zaidi wa mara tatu ya watu tuliopo sana. Kuna ardhi kubwa tu ya kuishi na kufanya shughuli zinazotuwezesha kuishi tofauti na huko Ulaya na Marekani. Tuna rasilimali nyini tu za asili ambazo ndizo hizo sasa unaona kutokana na ubovu wa uongozi wetu, tumeshindwa kuzitumia kusaidia huduma za jamii kama elimu, afya, maji safi na kadhalika.
Unaweza kuona kwa jisni gani ambavyo kutokana na watu wengi katika jamii kushindwa kupata huduma bora za kijamii na pia elimu wanaamua kuwa wategemezi kwa kuhama toka pale walipo kutafuta ndugu zao ambao angalau wana hali nzuri (kati ya hao masikini).
Kwa nchi za kiafrika, ongezeko la watu lina mahusiano makubwa sana na umasikini wa kujitakia ambao unaletwa na uongozi mbovu. Mtu kama ana shamba lake anaweza kulima lakini akizalisha hapati soko la mazao yake, sasa huyo mtu kakosa nini, kuna haja gani tena mtu ambaye anaweza kujimudu kumzuia kuzaa watoto kiasi atakachoweza??.
Kule China na Japan ambapo kuna watu wengi, maisha yanaonekana angalau ni mazuri kulinganisha na kwetu lakini unasitaajabu hao Wachina wanakimbilia katika nchi zetu na wanapata maeneo mazuri tu ya kuishi na kufanya shughuli za kijamii kwa raha kabisa wakati ambapo sisi wenyewe wazawa tunalazimishana kupunguza idadi ya watu. Wazungu wanakuja Afrika na kupata maeneo makubwa tu ya kuishi na kufanya shughuhuli za kiuchumi wakati ambapo sisi tunaona hatuna maeneo ya kuishi...
Utegemezi wetu ni mfumo unaochochewa zaidi na uongozi, kama kule Lindi, Songea, Sumbawanga nk kungekuwa na mazingira mazuri ya kufanya shughuli za kiuchumi na pia huduma bora za jamii, nadhani ni watu wachache sana wangekuwa na fikra za kuhangaika kumtafuta ndugu zoa wanaoishi katika mijia afadhali kama Dar es Salaam, Arusha au Mwanza ili akaishi nae.
Kama kungekuwa na mfumo bora wa Elimu wa kuwezesha wazazi kusomesha watoto wao wote pasipo shinda, nani angesumbuka kumtafuta kaka, dada, shangazi au mjomba ili akamsomeshe au kumtafutia kazi?? Kwa utawala huo mbovu, sasa utegemezi umekuwa ni tabia miongoni mwetu.
Waweza pia kuona kuwa matatizo ya kiuchumi na kukosa huduma bora za kijamii yanaongeza vifo kutokana na magonjwa yanayotibika kama malaria au yale yasiyotibika kama UKIMWI na kuacha yatima ambao wanaongeza tabaka la watu tegemezi.