CIA Report. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CIA Report.

Discussion in 'International Forum' started by Francis Baraka, May 15, 2010.

 1. F

  Francis Baraka Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Jamani wana jamii naomba tuchambue nini maana ya report iliyotolewa na CIA juu ya ukuaji ama ongezeko la watu kwa kiasi kikubwa huku kundi tegemezi likionekana tatizo kwa uhai wa taifa letu ukizingatia idadi ya wenye kuzalisha inaonekana ni ndogo kuliko wahitaji.
  Binafsi sina uhakika na takwimu zilizotolewa na CIA ila JE,nini hasa wanachotutaka?na kama ni kutushauri tu,je ushauri wao uko sahihi?
  Wanajamii tafadhali tusibeze hili,naomba tujaribu kufanya upembezi staha ili hili liwe wazi kwetu sote.
   
 2. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Topic nzuri Francis, ila mi naomba uweke link ya hiyo report hapa ili wenye interest tuipitie kwanza kabla ya kuanza kuichambua
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hiyo ripoti i wapi??
  Kama suala la kuongezeka kwa kasi kwa watu ambayo hawaendani na hali halisi ya huduma za jamii, na hivyo kuongezeka kwa wategemezi, kwa jamii zetu wa Afrika nadhani vyanzo vipo wazi.

  Mtu asikudanaye kuwa sisi tunaweza kufuata mifumo ya Ulaya na Marekani ya kupunguza idadi ya watu kupitia uzazi wa mpango. Rasilimali tulizo nazo kama tungezitumia vizuri, bado tunahitaji zaidi wa mara tatu ya watu tuliopo sana. Kuna ardhi kubwa tu ya kuishi na kufanya shughuli zinazotuwezesha kuishi tofauti na huko Ulaya na Marekani. Tuna rasilimali nyini tu za asili ambazo ndizo hizo sasa unaona kutokana na ubovu wa uongozi wetu, tumeshindwa kuzitumia kusaidia huduma za jamii kama elimu, afya, maji safi na kadhalika.

  Unaweza kuona kwa jisni gani ambavyo kutokana na watu wengi katika jamii kushindwa kupata huduma bora za kijamii na pia elimu wanaamua kuwa wategemezi kwa kuhama toka pale walipo kutafuta ndugu zao ambao angalau wana hali nzuri (kati ya hao masikini).

  Kwa nchi za kiafrika, ongezeko la watu lina mahusiano makubwa sana na umasikini wa kujitakia ambao unaletwa na uongozi mbovu. Mtu kama ana shamba lake anaweza kulima lakini akizalisha hapati soko la mazao yake, sasa huyo mtu kakosa nini, kuna haja gani tena mtu ambaye anaweza kujimudu kumzuia kuzaa watoto kiasi atakachoweza??.

  Kule China na Japan ambapo kuna watu wengi, maisha yanaonekana angalau ni mazuri kulinganisha na kwetu lakini unasitaajabu hao Wachina wanakimbilia katika nchi zetu na wanapata maeneo mazuri tu ya kuishi na kufanya shughuli za kijamii kwa raha kabisa wakati ambapo sisi wenyewe wazawa tunalazimishana kupunguza idadi ya watu. Wazungu wanakuja Afrika na kupata maeneo makubwa tu ya kuishi na kufanya shughuhuli za kiuchumi wakati ambapo sisi tunaona hatuna maeneo ya kuishi...

  Utegemezi wetu ni mfumo unaochochewa zaidi na uongozi, kama kule Lindi, Songea, Sumbawanga nk kungekuwa na mazingira mazuri ya kufanya shughuli za kiuchumi na pia huduma bora za jamii, nadhani ni watu wachache sana wangekuwa na fikra za kuhangaika kumtafuta ndugu zoa wanaoishi katika mijia afadhali kama Dar es Salaam, Arusha au Mwanza ili akaishi nae.

  Kama kungekuwa na mfumo bora wa Elimu wa kuwezesha wazazi kusomesha watoto wao wote pasipo shinda, nani angesumbuka kumtafuta kaka, dada, shangazi au mjomba ili akamsomeshe au kumtafutia kazi?? Kwa utawala huo mbovu, sasa utegemezi umekuwa ni tabia miongoni mwetu.

  Waweza pia kuona kuwa matatizo ya kiuchumi na kukosa huduma bora za kijamii yanaongeza vifo kutokana na magonjwa yanayotibika kama malaria au yale yasiyotibika kama UKIMWI na kuacha yatima ambao wanaongeza tabaka la watu tegemezi.
   
 4. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
 5. paradox

  paradox Senior Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So I read the whole thing from that link, na all I can say is ni kitu gani umeona hapo ambacho kimekushtua?? I mean the CIA databases have facts on every country in the world, search for it and you will get, I don't think there can be any underlying objectives in something an organization does so routinely, it updates it's databases annually so most of the facts they write are might be accurate (perhaps a few discrepancies might exist), I don't think they would put up false information on purpose though, what for??? seriously dude.
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wanaponivunjaga mbavu hawa jamaa ni pale wanaposema ati, Tz wakristo ni 30% na waislam ni 35%, indiginious ni 35%...wakati tz hatujawahi kufanya sensa ya kidini, na hata kama tungekuwa tumefanya, watu wasio na dini si wengi hivyo. ukienda kwenye saiklopidia zingine, wanakwambia Tz wakristo ni 45% waislam ni 30%, waliobaki kama asimilia 20% ni wasionadini...asilimia 5% ni wahindu,budha etc. sasa sijui tumwamini nani, na tangu nimesoma hii factbook yao mwaka 2004 tulipokuwa tunabishana na mtu kuhusu mambo fulani, kitu iko palepale, wanakopi na kupaste...hawana maana kwa kifupi.
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  CIA ni mabingwa wa overt and covert operations.
  Hii ni pamoja na kufalsify data kwa manufaa yao.
  You can only believe them at your own peril
  Success yao ni wewe kuwaamini na kuji subscribe to their suggestive thinking.
  In short WAMEKUPATA mzee!!
   
Loading...