CIA report: Israel will fall in 20 years


See also: Fearing a One-State Solution, Israel’s President Serves Pabulum to Washington

Source: CIA Report

 

Sababu mojawapo kubwa ya kuanzishwa kwa taifa la Israel ni HOLOCAUST...Fuatilia Historia.
 
Israel ni taifa teule la MUNGU, kwahiyo halitakaa lisambaratike hata siku moja mpka mwisho wa dunia. MUNGU ndo everything kwao na sote twajua hakuna lisilowezekana kwa MUNGU. Mafanikio mengi waliyo nayo Wamarekani leo ni kwa sababu ya urafiki wao mzuri na Israel. Kama Wamarekani wakiamua kuitosa Israel, MUNGU ajua namna ya kuwalisha (Waisrael ) na huo ndo utakuwa mwisho wa Marekani kuwa super power.
 
Marekani imebarikiwa kwa sababu inawaunga mkono Israeli? Hivi maana ya baraka au kubarikiwa ni nini? Kuwa tajiri hata kama unaiba au kudhulumu wengine ni baraka? Kutumia nguvu za kijeshi kuua watu wasio na hatia na hata kuwa polisi wa dunia ni baraka hizo? Tusemeje basi kuporomoka kwa uchumi kwa nchi iliyobarikiwa? Madorf yule Myahudi alihesabiwa mvua 150 tuseme alibarikiwa kwa sababu alikuwa na fedha nyingi alizowaibia Wayahudi wenzake? Nasita kukubali theologia nyepesi kwamba mtu akiwa maskini basi amelaaniwa hata kama amenyonywa na kuibiwa, na kwamba kila anayeonekana kuwa navyo vingi basi amebarikiwa hata kama amewaibia na kuwanyonya wengine.
 
Last edited:

Hmmm, Uchumi wa Israel ni wa ngapi kwa ukubwa duniani? Hizo billion 3 wanazopewa kila mwaka ni kwa ajili ya defense walisign contract mwaka jana na ni contract ya miaka 10.
 

Eeeh! Kumbe... eeeh! Mi nilifikiria taifa teule lililo mkiri na kumkubali yesu kuwa ndio mwokozi wao... kumbe kwa mujibu wa ukikristo ukiwa myahudi huna haja ya kuwa mkiristo... U'super power wa kuuwa wasio na hatia...lol eti na mungu anaukubali...lol! Maskini Red Indians native Americans... Hakuna wa kuwatetea na dhurma na uonevu mliofanyiwa... Marekani imekwenda kuwakumbatia taifa teule la mungu ili kufutiwa madhambi... yuk!
 
teh. teh. teh

hapa watu wengine wanachangia kiimani imani. matokeo yake wanafumbia macho mambo ya ovyo ya wazi wazi na badala yake wanakuwa bize kikweli kweli kusifia tu. kama vile hawaoni. kama vile hawasikii. kama vile hawasomi kwenye vyombo vya habari.

sisi binadamu ni dhaifu sana. na ni wabinafsi sana. lakin naamini kabisa dunia inaweza kuwa sehemu salama zaid ya kuishi kwa kila binadamu - awe mweusi, mzungu, mwarabu, mhind, mchina etc. bila kuwa na ulazima wa kuua, kudhulumu binadam wengine. kwasababu huo ni ufisad kwa binadamu
waungaji mkono ufisad dhidi ya binadam siwez kushangaa kusikia wanawaona kama mashujaa watuhumiwa wetu wa ufisad hapa tz

iam calling for peace every where
 
Baada ya kusoma posts nyingi zinazochangiwa kuhusu Israel, naona kuna mchanganyiko (confusion) mkubwa kuhusu dhana ya neno Israel. Kutokana na kuelewa kwangu kwa posts nyingi ni kuwa kuna baadhi ya watu kutokana na imani zao, hawawezi kutenganisha Israel ya Biblia (taifa/watu) na Israel kama serikali (government/administration). Hivyo ni vitu viwili tofauti. Kwa ufahamisho tu ni kwamba hata wale Wayahudi wenye siasa kali (ultra orthodox Jews) hawakubaliani na wala kuitambua serikali ya Israel na mfumo wake kama ilivyo sasa kuwa inawakilisha taifa la Israel. Middle East Online
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…