CIA: Korea Kaskazini inakaribia kuwa hatari kwa Marekani

CIA: Korea Kaskazini inakaribia kuwa hatari kwa Marekani

Cogito ergo_sum

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
1,648
Reaction score
2,930
Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA Mike Pompeo ametahadharisha kwamba Korea Kaskazini inakaribia sana kuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kombora la nyuklia.

Amesisitiza kwamba taifa hilo bado linapendeleza zaidi kutumia diplomasia na vikwazo lakini amesema kwamba bado wanatafakari uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi.

Korea Kaskazini imekuwa ikidai kwamba tayari ina uwezo wa kuishambulia Marekani.

Pompeo ameambia mkutano wa Wakfu wa Uhifadhi wa Demokrasia mjini Washington kwamba "Korea Kaskazini sasa imekaribia sana kuwa na uwezo ambao kwa mujibu wa mtazamo wa kisera wa Marekani tunafaa kufanya vitendo vyetu tukizingatia kwamba wako karibu sana kufikisha lengo hilo."

"Wanapiga hatua sana, na sasa ni kufikiria tu jinsi ya kuwazuia kufika hatua ya mwisho."

Ameonya kuwa ya Pyongyang imepiga hatua sana katika teknolojia yake ya makombora kiasi kwamba ni vigumu kwa majasusi wa Marekani kujua ni lini hasa watafanikiwa.

"Iwapo unazungumza kuhusu miezi kadha uwezo wetu wa kufahamu hilo kwa kina kwa sasa hauna maana kwa kiasi fulani," amesema.

Wikendi iliyopita, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alisisitiza kwamba Rais Donald Trump angependa kutatua mzozo wake na Korea Kaskazini kupitia demokrasia.

Hiyo ni baada ya Bw Trump kumwambia hadharani kwamba asipoteze muda akitafuta mazungumzo na Kim
 
Naona CIA wanaanza kuleta movie yao ya kutaka mtu apigwe kama wakati ule wa Saddam dhidi ya ushahidi wa kupikwa wa General Collin Powell U.N.
 
Zamani tunakuwa kwenye madisco vumbi ilikuwa hivi anatumwa dogo kuja upande mwingine anaanza kuwachokoza kwa maksudi tu bila sababu sasa mkoe uone timwili lake yeye katumwa kama chambo na wababe ninapoona hili suala la N korea na Usa Kim anatumwa tu kumchokoza Usa ila na yeye ni mjanja alishasoma mchezo siku nyingi hapo ni kupigana biti tu hakuna vita wala nini
 
exactly, wamarekani wajanja wakitaka kukupiga lazima wasingizie kwamba una silaha za Hatari, unatishia usalama wa dunia na bla bla nyingine
Naona CIA wanaanza kuleta movie yao ya kutaka mtu apigwe kama wakati ule wa Saddam dhidi ya ushahidi wa kupikwa wa General Collin Powell U.N.
 
exactly, wamarekani wajanja wakitaka kukupiga lazima wasingizie kwamba una silaha za Hatari, unatishia usalama wa dunia na bla bla nyingine
North Korea hizo silaha zipo dhahiri na kila MTU anajua hakuna blah blah hapo
 
Back
Top Bottom