Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 881
..nani atakwenda Pemba?
..Wapemba wenyewe kina Salim Salim na Maalimu Sefu wamejibanza mjini.
..wacha kijengwe Arusha ni mji wa kimataifa huo.
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!
Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!
Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?
Tumefanikiwa kupata nafasi ili chuo hiki kiwe Tanzania. Lakini for some unknown reasons WATAWALA na washauri wao wameamua kiwe ARUSHA!
Swali kwa nini kisijengwe Pemba hiki chuo ?..if not KIGOMA for that matter?
Kama alivyosema GT..hiki Chuo ingebidi kijengwe hata Kigoma! Hivi nyinyi mnafikiri kule siyo Tanzania? au watu wanafurahi tuu wakipewa eneo la kutoza ushuru..responsibility inaishia hapo?
Yaani kuna mikoa imetengwa bongo mpaka inasikitisha..
..jamani hiki ni chuo kikuu cha Afrika cha kimataifa.
..kingekuwa kinajengwa na serikali ya Tanzania basi tungekuwa na uwezo wa kuulizana kwanini hakijengwi Kigoma,Sumbawanga,Rufiji,Mafia etc.
..binafsi nadhani kilichozingatiwa hapo ni kuangalia eneo lenye miundombinu ya ku-support chuo kikuu. Arusha tayari miundombinu ya namna hiyo ipo mfano uwanja ndege, mawasiliano ya uhakika, mji wenye hadhi etc etc.
..sehemu kama Kigoma hata Watanzania wenyewe tunapakimbia. kuna maeneo kama Rufiji ambayo mtumishi wa serikali akihamishiwa anaamua kuacha kazi kabisa.
..sasa hawa wasomi/wahadhiri wa kimataifa ambao watafanya kazi kwenye chuo cha Mandela tuna uhakika kweli watavumilia kukaa eneo kama Kigoma, au Rufiji, au Mafia, au Sumbawanga, au Pemba?
..mngependekeza chuo kijengwa Mwanza kidogo ningewaelewa.
Masanja,
..nakubaliana na wewe kwamba kuna maeneo serikali imeyatelekeza.
..cha kusikitisha zaidi hata wananchi wa maeneo hayo nao kama wameunga tela la serikali ktk kuyatelekeza maeneo walikuzaliwa na kukulia.
..iliwahi kuletwa hoja hapa ikizungumzia utendaji wa Zitto Kabwe jimboni kwake.
..wana jamii forums wengi waliizima hoja hiyo wakisema Zitto halazimiki kuweka juhudi zozote zile kuchochea maendeleo ya Kigoma.
..sasa kama Zitto hana uchungu wowote na Kigoma mnategemea JK, Pinda, Masanja,jokaKuu etc ndiyo wawe na uchungu na Kigoma?
..hebu fikiria mkoa wa Kagera pamoja na kuonekana "nshomile sana" waliitana na kuchangishana 1.5 bilion kwa ajili ya elimu.
..umesikia wabunge toka Kigoma waki-organise mkutano wowote ule kuchangisha kwa ajili ya maendeleo ya Kigoma? na mikutano ya namna hiyo siyo lazima uite wana Kigoma peke yake.
MpendaTz said:Kukijenga chuo kule ndiyo ingelikuwa kichocheo cha serikali kuweka infrastructure stahili taratibu kwani ndivyo mikoa yote mikubwa ilivyoanza. Nyerere ndivyo alivyokuwa anashauri mara kwa mara, nakumbuka Mbeya cement ilikuwa kidogo isijengwe kule, kama sikosei ilikuwa phase two ya Tanga Cement
MpendaTz,
..i see your point.
..lakini huoni kwamba hiki chuo kinajengwa Arusha kwasababu miundombinu imeshatangulia pale?
..binafsi naamini tayari vipo vichocheo vingi tu vya kupeleka miundombinu Kigoma. kichocheo namba moja ni zao la michikichi, kichochoe kingine ni ziwa Tanganyika na mazao yake, hifadhi ya Sokwe ya Gombe, pamoja na soko/biashara na Jamhuri ya Congo.
..kama Watanzania wenyewe hatutaiinua na kuijenga Kigoma,Sumbawanga,Rufiji,Mafia,Kilwa, tusitegemee watu wa nje kama Mandela kuja kutufanyia kazi hiyo.
..binafsi sikubaliani na utaratibu wa Mwalimu Nyerere kuweka mbele siasa ktk maamuzi ya kiuchumi. utaratibu huo ndiyo uliopelekea kiwanda cha kukata almasi kikajengwa Iringa wakati almasi inapatikana Mwadui.
..