Chuo Kikuu (UDSM) Kufunguliwa na Masharti mapya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo Kikuu (UDSM) Kufunguliwa na Masharti mapya!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mafuchila, Jan 15, 2009.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Date::1/14/2009
  Daruso yafutwa, sheria mpya UDSM zatangazwa
  Latifa Karugila na Hussein Kauli

  CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeweka masharti magumu ya kudhibiti usajili wa wanafunzi waliodahiliwa upya kuingia chuoni hapo kuanzia Januari 19, mwaka huu.

  Vile vile, kimetangaza rasmi kufutwa kwa sheria za chuo zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Daruso).

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Makamu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Makenya Maboko, ilionyesha kuwa wanafunzi wote watakaotimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo, watapewa vitambulisho vipya pamoja na taratibu za namna ya kuishi chuoni hapo.

  Profesa Maboko alieleza kwenye taarifa hiyo kuwa, mwanafunzi atakayekutwa ndani ya chuo bila ya kuvaa kitambulisho atakuwa amesababisha uvunjifu wa amani na utulivu, hivyo atachukuliwa hatua za kisheria juu ya kitendo hicho.

  "Wanafunzi watakaokuwa wamevaa vitambulisho hivyo ndio watakaoruhusiwa kuingia darasani," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Ili kutekeleza masharti hayo, Profesa Maboko alisisitiza kuwa kila mwanafunzi atakayekamilisha taratibu za usajili atapaswa kupatiwa kitambulisho kipya, vinginevyo hatatambuliwa kama mwanafunzi aliyetimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo.

  Akizungumzia kuhusu Serikali ya Wanafunzi wa UDSM (Daruso), Profesa Maboko alisema taasisi zote za wanafunzi zilizokuwa zikitambuliwa na sheria ya chuo ya mwaka 2007, kabla ya kusimamishwa kwao, hazitatambuliwa tena.

  Alisema taasisi hizo zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho.

  "Taasisi mpya za wanafunzi zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho," aliongeza Profesa Maboko.

  Wanafunzi waliosajiliwa upya watatakiwa kuripoti chuoni hapo kuanzia Januari 19 hadi 22, mwaka huu, kwa utaratibu maalumu uliotolewa na chuo.
  Source: Mwananchi 15/01/2009
   
  Last edited by a moderator: Jan 16, 2009
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Divide and rule!

  Sijui ni kwa nini wanadhani tatizo ni Daruso. Hali hii inasikitisha na hasa kwa sababu inatokea kwenye vyuo vikuu ambapo katika hali ya kawaida tusingetegemea maprofesa hawa kukubali kutumiwa na wanasiasa.
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kazi ipo kwani Vyuo vya elimu ya juu kuongozwa na watu wenye ushabiki wa vyama vya siasa madhara yake ndio hayo,watanzania masikini wana nafasi gani ya kusomesha watoto wao katika mazingira kama hayo.Kazi kwenu wadau kuiokoa jamii kielimu.
   
 4. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu Makamu wa Taaluma anajua maana ya taaluma?

  Wanafunzi wa chuo kikuu bado wanaongozwa kama kondoo?

  Chuo kikuu inategemea hawa wanafunzi wakimaliza masomo yao watakuwa wana-confidence yeyote na ushindani katika hii globalization?

  This is pathetic kwa uamuzi uliotolewa na CHUO KIKUU. It is time for other facult members to speak against this.
   
 5. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Kuvaa Vitabulisho......?!!!!!!
  Wadau naomba kufahamishwa ili swala la vitamblisho.
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kosa lingine ni letu wazazi. Vijana wanagoma wakiangalia uwezo wa sisi wazazi wao. Sisi tunakaa kimya kana kwamba hayatuhusu. Tunawasaliti vijana na kwa kufanya hivyo tunajisaliti wenyewe. Tunapaswa kupaza sauti zetu na kumuuliza JK, mbona watoto wa maskini wanakosa elimu wakati ulisema haitatokea hivyo?

  Tujiulize pia, hivi watoto wote wanaotaka mkopo wakipewa asilimia 100 kuna shida yoyote? La msingi ni kuwabana walipe, period. Ni kama nataka kulima, naenda benki kukopa, benki inanipa hela za kulimia tu na inasema za kuipanda na kupalilia nijitegemee wakati sina uwezo huo. Je nikilima tu huo mkopo utarudi? Si bora wanikoppeshe hadi gharama za kuvuna na kuuza ili hayo mauzo ndiyo nilipe mkopo?. Serikali tumia akili.

  Tatizo linakuwa gumu kwani JK, mkuu wa nchi alitoa msimamo wake mapema sana juu ya suala la sera ya uchangiaji kuwa haitabadilishwa. Ni kosa kubwa kwa rais kutoa misimamo kama hiyo kwani wewe ndiye mkuu kabisa, Sasa tuone kama hatakula matapishi yake.
  Akisema sera ibaki hivyohivyo - kala matapishi yake maana watoto wa maskini hawatasoma. akisema ibadilishwe - kala matapishi yake maana alishasema haitabadilishwa. KAZI KWELIKWELI.
   
 7. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kosa lingine ni letu wazazi. Vijana wanagoma wakiangalia uwezo wa sisi wazazi wao. Sisi tunakaa kimya kana kwamba hayatuhusu. Tunawasaliti vijana na kwa kufanya hivyo tunajisaliti wenyewe. Tunapaswa kupaza sauti zetu na kumuuliza JK, mbona watoto wa maskini wanakosa elimu wakati ulisema haitatokea hivyo?

  Tujiulize pia, hivi watoto wote wanaotaka mkopo wakipewa asilimia 100 kuna shida yoyote? La msingi ni kuwabana walipe, period. Ni kama nataka kulima, naenda benki kukopa, benki inanipa hela za kulimia tu na inasema za kuipanda na kupalilia nijitegemee wakati sina uwezo huo. Je nikilima tu huo mkopo utarudi? Si bora wanikoppeshe hadi gharama za kuvuna na kuuza ili hayo mauzo ndiyo nilipe mkopo?. Serikali tumia akili.

  Tatizo linakuwa gumu kwani JK, mkuu wa nchi alitoa msimamo wake mapema sana juu ya suala la sera ya uchangiaji kuwa haitabadilishwa. Ni kosa kubwa kwa rais kutoa misimamo kama hiyo kwani wewe ndiye mkuu kabisa, Sasa tuone kama hatakula matapishi yake.
  Akisema sera ibaki hivyohivyo - kala matapishi yake maana watoto wa maskini hawatasoma. akisema ibadilishwe - kala matapishi yake maana alishasema haitabadilishwa. KAZI KWELIKWELI.
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,842
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Mkuu tupo pamoja hapa. Unajua! wanafunzi wakigoma vyombo vya habari vinakuwa vya kwanza kuwabeza eti hawajui hata sababu wanayogomea, mara wanatumiwa na wanasiasa, tena ohh walafi nk. Hata katuni za akina kipanya utakuta zinawabeza eti wanaomba nyongeza wakati wananchi wengine wako hoi. Tena, hata hapa JF wapo wengi tu. Tuliopita pale mlimani tunajua issue ilivyo na namna 'wazazi' walivyotutosa kutuunga mkono na kuendelea kusikiliza propaganda za Serikali.

  Sasa unapofuta DARUSO unataka nini kama siyo kuongeza matatizo? katika ulimwengu wa leo huwezi kutawala bila kuwashirikisha unaowatawala. DARUSO imekuwa ikisolve matatizo mengi ya wanafunzi na kuwawakilisha wanafunzi katika vikao mbalimbali vya chuo kuanzia senete. Hivi utakuja tu kuwaambia wanafunzi kadhaa wamedisco au supp. bila mwakilishi wao kuhusika seneti?!!! damn!

  Halafu eti mwanafunzi wa chuo kikuu atembee chuoni akiwa amevaa kitambulisho! what a shame!

  'wazazi' = wananchi.
   
 9. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,030
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  1. sasa watanzania tunawaiga Makaburu na sera yao ya apartheid kwani wabantu ktk maeneo yaliyotengwa ( reserved bantuland) walitakiwa kuvaa vitambulisho.
  2. Kuna tatizo gani kama mtu ataingia darasani halafu asifanye mtihani? Siono haja ya watu kuonyesha vitambulisho ndio aingie darasani.
  3. "PhD holders are people who are very deep in the ocean but at a very shalow water to the extent that their backs are seen". Usomo wao uko wapi ktk masuala madogo kama haya?
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mh!

  Wazazi wengi wanaona kama vile
  "Elimu ya chuo kikuu ni huruma ya serikali ya CCM tu au sivyo watoto wao wamngeishia huko madongo."
  Sijui ni lini kondoo sisi tutatambua uwezo wetu wa kutumia pembe na kwato zetu vizuri na kuacha kuendelea kulia baaa! baaa! kila siku?
   
 11. Kiumbemzito

  Kiumbemzito Member

  #11
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  watu wameanza kuzeeka akili,DARUSO sio chanzo cha vurugu au migomo!
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kama wanafunzi wa chuo kikuu wanabehave kama watoto wa sekondari basi ni sahihi kuwawekea sheria kama watoto wa sekondari walio kwenye umri wa baleghe. Hawa wanafunzi wamekuwa aibu tupu na migomo yao isiyokuwa na kichwa wala miguu. Hongera uongozi kwa jitihada za kubuni mbinu za kujenga taifa lenye nidhamu, busara na fikra wajibifu.
   
 13. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa hivi wataambiwa wavae uniform za green vest za kijani.
   
 14. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haya bwana hiyo Ndio Tanzania yetu
  Hivi hawa viongozi wanaanzia wapi kuifuta Daruso, Viongozi wengi wa hapa Tanzania pamoja na kufanya mauzauza kibao kwenye serikali yetu, ila wameanzia huko kwenye serikali ya DAruso

  Pia ikumbukwe kuwa hata wale waliokuwa na uchungu na nchi yetu (Baba wa Taifa) alikuwa akitambua mchango wa Daruso na ndio maana hakuwahi kutamka kuhusu kuifuta Daruso pamoja na migomo yote iliyokuwa ukitokea enzi hizo

  Haya yote ni matunda ya serikali ya CCM, na hili pia kikwete atakuwa kalipitisha mwenyewe maana najua kabisa DARUSO ilikuwa inamaana kubwa sana hapa Nchini na ilikuwa ikitambulika kisheria, sasa mambo kama haya kama yanafanyika tu bila utaratibu ni maajabu.

  Haya bwana, ngoja tuone wasomi bila utaratibu wao wenyewe inakuwa vipi?
   
 15. U

  Usimwogope New Member

  #15
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa sasanakuwa sijui wapi tunaenda maana siku mojo hawa wanachuo watatakiwa kuwa na sale za chuo.
   
 16. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #16
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Do
  Do
  Do
  Do
  Do
  DO
   
 17. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  What a shame in this country; this country bwana "IMELAANIWA", wazazi wamelaaniwa; ukiwauliza wazazi wanasema safi; safi wakati watoto wamekosa nafasi ya kusoma chuo? umaskini mwingine unatengenezwa huo; what a crap is this country; heri niondoke tu maana maisha ya walio wengi nchini hayana maana; yana vikwako kila kona kuanzia hospital, ofisini, na sasa vyuoni; Eti unatawala watu kwa hofu; haisaidii; maprofessa uchwara sasa ndio hao sio aliokuwa anaongelea Mkapa enzi hizo
   
 18. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Siyo taifa lenye nidhamu bali la wanafiki na la kuwaabudu wenye madaraka.
   
 19. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  DARUSO BUNGE LAO Vipi, wakae chini na watoe tamko kama wasomi.

  Naomba C.V ya mbunge mmoja anaitwa MISS YOHANA ROGASIANI MARTINI. Yuko mwaka wa tatu Ualimu Psychology.

  Asanteni
   
 20. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani sio kila wakati tuwe watu wa kutoa lawama tu pasipo na sababu za msingi, chuo kuamua kuifuta daruso mimi naona wapo sahihi kabisa maana hiyo daruso ilishapoteza mwelekeo wake na ikabakia kuanzisha migomo isiyokuwa na msingi, WHY nimesema hivi:-

  Hebu nambieni shuo kimetoa masharti kwa mwanafunzi anayetaka kurejea chuoni ni lazima ajaze forms za kuomba kudahiliwa upya na awe ameambatanisha risiti za ada na awe amemaliza ada yote then azitume kwa registre kabla ya tar 2 january 2009,, wapo waliotimiza haya masharti na wapo wengine walijaza forms na kutokulipa ada wakitegemea chuo watalegeza masharti na watarudi bila kumalizia ada kama ilivyokuwa huko nyuma kwenye migomo mingine, chuo kwa kuwaonea huruma wakawaongezea muda wale ambao walisubmit forms bila kumaliza ada wakawapa mpaka tar 15 january 2009 then tar 16 up 2 17 jan watatoa batch ya pili ya majina ya wale walioweza kufikisha sifa za kurudishwa chuoni, sasa kilichotokea ni kwamba chuo wamekuwa na msimamo mmoja tu kuwa atakayemaliza ada ndiye atakayeruhusiwa kurudi chuo, na asiye maliza basi huyo hataki kusoma. na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wameweza kwenda kulipa ada ili waweze kurejeshwa chuoni, sasa haya yaliyopelekea chuo kuamua kuifuta DARUSO ni kwamba:- Juzi tu hapa huyu raisi wa wanafunzi somebody Machibya ameenda kufanya pressconference kuutangazia uma wa wanafunzi wote kuwa ifikapo tarehe 19 January 2009 wanafunzi wote waripoti chuoni wawe wamemaliza ada au hawajamaliza ada waende chuoni na wataingia darasani kama kawaida, sasa hebu niambie wewe ambaye unalaumu why DARUSO imefutwa hii ni kutafuta haki au kutafuta choko choko zisizo na msingi kwa serikali?? Wewe ni nani mpaka utake kutengua maamuzi ya wakuu wako ambao wanakufundisha hapo chuoni na utake kutengua maamuzi ya serikalli? kanini usingekuwa mpole tu? na alipoulizwa kama yeye amelipa au la akasema kwa kujiamini kabisa kuwa hajalipa na hatalipa na chuoni atarudi tu sasa hii ni haki?? wanafunzi wenzako 8000 wameenda kulipa ada wewe unautangazia uma kuwa hutalipa ada na chuoni utarudi tu who are you?? Chuoni kila mtu alienda kwa wakati wake na usia alipewa na wazazi wake na anapofuikuzwa anaondoka peke yake kurudi kwa wazazi wake peke yake hakuna solidarity tena zaidi ya kujawa na hofu utaenda kujibu nini kwa mzazi wako ambaye ni mkulima. Sasa chuo ndo kimeshaamua hivyo no way hakuna DARUSO mpaka hapo itakapotungwa sheria mpya na si daruso tu hakuna society yoyote ya wanafunzi inayotambulika kwa sasa mpaka hapo chuo kitakapotoa utaratibu mpya na kutangaza kwenye gazeti la serikali out off that unajitafutia kuumia tu,, mbaya zaidi nasikia kwamba wamevunjiwa sehemu yao pale nje walipokuwa wanakaanga chips na bar yao walikuwa wanasubiriwa wamalize stock ya vinywaji vilivyopo the waifunge kabisa na ofisi zao walishaambiwa watoe wanachokiona ni chao watafute sehemu nyingine si kwenye majengo ya chuo.

  Na pressconference aliyoifanya huyu raisi wa DARUSO ndo imepelekea chuo kutoa maamuzi ya kuwataka wanafunzi wavae kitambulisho watakachopewa upya maana inspection inaanzai getini, unafika pale unaangalia jina lako lipo unaruhusiwa kuingia ndani ya chuo kwa ajili ya registration na unatakiwa kukiacha pale kitambulisho chako cha zamani,, ukiangalia hii yote ni kutaka kuwabana wale ambao wamegoma kulipa ada na wanataka kuja kusoma bure na ndo hao hao waanzisha migomo isiyokuwa na msingi, hebu tufikirie kwanza kabla ya kulalama tu kuna ncho ambayop inatoa elimu bure kwa sasa hivi? ukinambia sweedn, Finland, Norwey nitakucheka maana hao wanakusomesha lakini joto ya jiwe utakuja kuiona huko mbele ukishamaliza shule na umepata kazi so SERA YA UCHANGIAJI KATIKA ELIMU NA AFYA NI LAZIMA na tena nashangaa kwa nini tunakomalia elimu tu na tusikomalie afya iwe free....

  Ni hayo tu waungwana si vyema tukaegamia upande mmoja tu kila wakati, madogo wanachemka na ni lazima kaka zao hapa JF tuwaelekeze maana nasi tulipita hapo
   
Loading...