Lyimo
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,826
- 2,017
Nimestushwa na taarifa ya serikali kutaka kujenga chuo kikuu kingine cha Kilimo katika mkoa wa Katavi, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira la leo. Sababu ya mstuko huo ni hali mbaya ya vyuo vyetu vya kilimo vilivyopo ambayo vinashindwa kijikidhi na kutoa huduma stahiki kutokana na bajeti finyu inayopokea kutoka serikalini. Chuo kikuu kilichopo (SUA) bado kinahitaji kujitanua na hakijajitosheleza wataalamu, hivyo ni heri serikali ingeongeza nguvu kwenye chuo hicho kama inajali zaidi wakulima. Kwa miaka ya karibuni sasa kumekuwa na mfumuko wa vyuo vikuu Tanzania jambo lililopelekea hata kushusha viwango vya kuingia kwenye vyuo hivyo, jambo ambalo lilibarikiwa na Tume ya vyuo Vikuu (TCU). Mfumuko huu utasababisha kutozalisha wataalamu waendeshaji/ watendaji wenye ngazi ya Diploma na Cerificates ambao ni wanahitajika sana kutokana na mahitaji ya Taifa. Bado wataalamu wa Kilimo hawatoshelezi Kata zote nchini, licha kimfumo kila kijiji kinahitaji bwana shamba na bwana mifugo ambao vijiji vingi sana hawana, hivyo hata kupata maelekezo/ushauri wa kitaalamu haiwezekani. Sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kina katika kuwekeza kwenye mahitaji ya wataalamu wa kilimo nchini.
Vyuo vya Kilimo na Utafiti vya serikali ninavyovikumbuka kwa uchache, (wachangiaji mtanisaidia kuongezea vingine vingi):
- Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro;
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Uyole Mbeya
- Chuo cha maendeleo ya Mifugo Tengeru (LITI-Tengeru) Arusha
- Tengeru Horticultural Reasearch and Trainning (HORTI).- Arusha
- Chuo cha kilimo na Utafiti Kilombero (KATRIN) Morogoro
- Chuo cha Kilimo taaluma ya umwagiliaji Igurusi - Mbeya
- Chuo cha kilimo na Utafiti Ilonga (MATI Ilonga) Morogoro
- Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro (KATC) - Kilimanjaro
- Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Mlingo
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Morogoro (LITI Morogoro) Morogoro
- Chuo Cha Utafiti wa Kilimo Cha Ukiriguru
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Buhuri (LITI Buhuri) Tanga
- Chuo cha Maendeleo ya Kilimo Inyala Mbeya
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) Arusha
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Mpwapwa (LITI Mpwapwa) - Mpwapwa
- Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele Mtwara
- Chuo cha utafiti wa Kilimo Tumbi Kibaha
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Mlingano Tanga
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Tumbe Tabora
- Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa magonjwa ya wanyama (ADRI) DSM
- Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Madaba - Songea
Vyuo hivi vingeweza kutumika vizuri kufundisha wataalamu na hata wakulima ili kuweza kuendesha kilimo chenye tija. Tukumbuke kuwa, wananchi wengi maskini Tanzania ni wakulima, hivyo tukiacha hivi vyuo vijiendeshe kibiashara kama vyuo vya uhasibu ama IT ambavyo wahitimu wake ni rahisi kuajiriwa mijini. Vilevile mazingira bora ya watumishi wa vijijini yanahitajika ili kuwavutia wataalamu kufanya kazi vijijini. Kama serikali haitaweka kipaumbele kwenye kuboresha miundombinu vijijini na kuelimisha wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija ni dhahiri kuwa wimbi la vijana kukimbilia mijini halitakoma. Serikali ilitakiwa kuvisaidia kwa hali na mali vyuo hivi vilivyotawanyika nchi nzima japo vina wataalamu wachache bado. Sioni mantiki ya kukimbilia Kujenga chuo kikuu cha Kilimo Katavi wakati wahadhiri/watafiti hawapo wa kutosha nchini (SUA haijajitosheleza bado). Vilevile kwa Tanzania ya leo bado ni ndoto kuwa na mabwana shama wenye taaluma ya degree, hivyo ni vema tukaweka mkazo kwanza kwenye hivi vyuo vya diploma na certificate. Wakati utafika ambapo tutakuwa na hitaji la vyuo vikuu baada ya kujitosheleza kwenye hii ngazi ya kati kimahitaji. Swala la Chuo kikuu Katavi ni la haraka mno na linaonekana lina maslahi kisiasa zaidi kuliko kutoa huduma ya elimu, ushauri na utafiti kwa wananchi.