Is it really a good investment idea to build another University in Dar. Why not find another region? Dar is overpopulated, unless building it in areas such as Kibaha. Lakini really Dar? This would be a great investment, but should not be built in Dar at all.Duh hivi ndio maana nasema kuwa lazima tuwe makini sana na harakati za Kampeni hizi
Kwanza lazima waboreshe vyuo tulivyokuwa navyo na kabla ya kuanza kwa chuo hiki. Kuna vyuo vya umma kibao na pia kuna haja ya kukarabati chuo kikuu cha Dar maana inatia hata aibu kwa Taifa
Kwa nini wasijenge Tabora? Kuna eneo kubwa tu pale na hospital kubwa ya Mkoa wa Kitete. Walau Tabora nayo itakuwa na income fulani kwani wanafunzi ni purchasing Power. Tabora hamna madini, mgodi, kiwanda wala babu yake nani. Pamejichokea na kukondeana kama kijibwa cha Darfur.....
Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar
Na Jackson Odoyo
RAIS Jakaya Kikwete ametangaza azma ya serikali kujenga Chuo Kikuu cha Afya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wananchi jana katika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee wakati wa kuzindua Mpango kabambe wa kuboresha huduma ya afya nchini, alisema Chuo hicho, kitaongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini.
Alisema mpango huo, lazima uende sambamba na mikakati thabiti ya kuboresha huduma hiyo nchini.
"Maandalizi ya ujenzi wa Chuo Kikuu katika maeneo ya Mloganzira jijini Dar es Salaam
yamekamilika na kitaanza hivi karibuni ili kuongeza idadi ya Madaktari. "Hivi sasa tunatoa madaktari 200 kwa mwaka, baada ya kuanzishwa kwa chuo hicho tutajitahidi angalu tufikie idadi ya madaktari 1,000 kwa mwaka,"alisema Rais Kikwete
wadau, hii mloganzira iko pande zipi hapa dar
Kwa nini wasijenge Tabora? Kuna eneo kubwa tu pale na hospital kubwa ya Mkoa wa Kitete. Walau Tabora nayo itakuwa na income fulani kwani wanafunzi ni purchasing Power. Tabora hamna madini, mgodi, kiwanda wala babu yake nani. Pamejichokea na kukondeana kama kijibwa cha Darfur.....
Kwanza lazima waboreshe vyuo tulivyokuwa navyo na kabla ya kuanza kwa chuo hiki. Kuna vyuo vya umma kibao na pia kuna haja ya kukarabati chuo kikuu cha Dar maana inatia hata aibu kwa Taifa
Kwa tetesi changu UDOM mwaka huu pekee watakuwa wanafunzi 20,000 pamoja na fani nyingine na pia wanafunzi wanaosoma udkatari watakuwa kama 100 hivi kwasababu hiyo ni bora kuboresha vyuo vingine kwanza, maana hata hivi vya binafsi vinaweza kuchukua kwa muda wanafunzi wengine, na pia mimi naona kuna haja ya kuboresha kwanza vyuo vingine kwa miundombinu kwanza na kuanza vingine, tutakuwa tunafanya vitu nusunusu, sijaona watu kama wanachukulia kwa uzito chuo cha Sokoine university. Mimi nasema tuboreshe kwanza hivi tulivyokuwa navyo kuliko kuanza kujenga vingine na kuweza, hata kama tupo nyuma, Kwani Uganda wana vyuo vingapi?? Mbona wanatoa madaktari wengi kuliko Tanzania?? Jamani tume makini sana na kuanzisha vyuo. Sijakataa kuanzisha vyuo ni kitu kizuri ni lazima mikakati iwepo pia ili kujenga jamii bora zaidi na kutoa wahitimu bora zaidi na vifaa vya kufundishiaHivi chuo kikuu cha Dodoma kinatarajiwa kuchukua wanafunzi wangapi? na hicho cha Afya kitatarajiwa kuchukuwa wanafunzi wa ngapi?
Sijakataa kuanzisha vyuo vingine ni kitu kizuri sana kwa Taifa letu, lakini isije kutokea na kusahau kushughulikia vyuo vingine ambavyo tunavyo tayari. wewe mwenyewe shaidi, sijajua kuwa chuo cha Dodoma, au UDSM wamepewa bajeti shilingi ngapi?? na hapa ndipo unaweza kujua kitu nasema nini?? Kuna uwezekano huo mkubwa na kutazama na rasilimali zote kupeleka sehemu moja tu. hii itakuwa ni Hatari sanaMkuu Sikonge, hapo ndipo haswa kwenye point... Unajua Dar tayari ipo imejaa lukuki na hakuna mipango yoyote siku za usoni kujaribu kupunguza msongamano, then wanakuja na hili!?!!? ni kweli kwa nini wasipeleke mikoa ya mangaribi manake angalia kuna KCMC (kaskazini mashariki), Bugando (Kaskazini na mangaribi) kisha kusini hakuna chuo kikubwa cha afya... sasa hii kuongeza lijichuo jingine Dar ni kuzidisha msongamano kwenye kibiriti kilichojaa.... nikiulizwa nitasema wakijenge (Tabora - central to west) au hata ikiwezekana kipelekwe Mbeya au japo Iringa tujue moja.... jamani Tanzania hii yetu itajengekaje wakati maendeleo tunayavutia kule ambapo tumerithishwa na wakoloni, ina maana sisi hatutaweza kujenga from scratch.... may be ni kweli manke kikubwa tulichowahi ongelea kuanzisha/kujenga ilikuwa CDA (Makao Makuu Dodoma, now more than 30 years and counting)....
Mkuu Josh M, naomba kwa hili nipingane kidogo na wewe... Kwa uelewa wangu na kutembelea karibu asilimia kubwa ya Tanzania, nimegundua kuwa Tanzania tupo nyuma sana katika fani ya elimu na afya.... Hatuna madaktari wa kutosha na vifo vingi maeneo ya vijijini vinatokana na kukosa tiba/ushauri mbadala wakati muafaka... kuongoze vyuo vya afya kutapelekea kuwa na madaktari wengi na hii inaweza kutusaidia kupunguza vifo na kuokoa jamii kubwa ya waTanzania..... hivyo hata kama kuna vyuo vikuu 1000, sioni tatizo kama uwezo upo kujenga vyuo vya afya na ualimu...
naomba kuwakilisha...
Is it really a good investment idea to build another University in Dar. Why not find another region? Dar is overpopulated, unless building it in areas such as Kibaha. Lakini really Dar? This would be a great investment, but should not be built in Dar at all.