Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimeo, Jul 1, 2009.

 1. K

  Kimeo Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar

  Na Jackson Odoyo

  RAIS Jakaya Kikwete ametangaza azma ya serikali kujenga Chuo Kikuu cha Afya jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Wananchi jana katika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee wakati wa kuzindua Mpango kabambe wa kuboresha huduma ya afya nchini, alisema Chuo hicho, kitaongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini.

  Alisema mpango huo, lazima uende sambamba na mikakati thabiti ya kuboresha huduma hiyo nchini.

  "Maandalizi ya ujenzi wa Chuo Kikuu katika maeneo ya Mloganzira jijini Dar es Salaam
  yamekamilika na kitaanza hivi karibuni ili kuongeza idadi ya Madaktari. "Hivi sasa tunatoa madaktari 200 kwa mwaka, baada ya kuanzishwa kwa chuo hicho tutajitahidi angalu tufikie idadi ya madaktari 1,000 kwa mwaka,"alisema Rais Kikwete


  wadau, hii mloganzira iko pande zipi hapa dar
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Maeneo ya Kwembe?
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh hivi ndio maana nasema kuwa lazima tuwe makini sana na harakati za Kampeni hizi
   
 4. k

  kilandu Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is it really a good investment idea to build another University in Dar. Why not find another region? Dar is overpopulated, unless building it in areas such as Kibaha. Lakini really Dar? This would be a great investment, but should not be built in Dar at all.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili kilikuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu na wakazi kuhusu kiwanja huko kwembe miaka mingi,kwa sbabu kwa sasa Muhimbili hapatoi fursa bora ya kimafunzo kwa vijana wanaojiunga na fani za afya,wafamasia wauuguzi madaktari na maabara kwa hiyo uliokuwepo toka enzi za mzee Ben
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wasijenge Tabora? Kuna eneo kubwa tu pale na hospital kubwa ya Mkoa wa Kitete. Walau Tabora nayo itakuwa na income fulani kwani wanafunzi ni purchasing Power. Tabora hamna madini, mgodi, kiwanda wala babu yake nani. Pamejichokea na kukondeana kama kijibwa cha Darfur.....
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanza lazima waboreshe vyuo tulivyokuwa navyo na kabla ya kuanza kwa chuo hiki. Kuna vyuo vya umma kibao na pia kuna haja ya kukarabati chuo kikuu cha Dar maana inatia hata aibu kwa Taifa
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  kuna kushindana kwa wakubwa wetu,kila mmoja anataka atakapoondoka madarakani waseme alijenga hiki ama kile,you get my point?
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Faida ni kwetu sisi, lakini pale muhimbili ndugu zangu inatia aibu sana na hata pale UDSM/ Sasa vipi tena Dodoma university??
   
 10. Kijini

  Kijini Member

  #10
  Jul 1, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni bora kuboresha vyuo vilivyopo na huduma katika hospitali zilizopo kwanza, Tz ukiumwa omba iwe kitu kidogo na rahisi kutambulika vinginevyo, utakutana na madaktari wanaokisia kisia tu na hakuna vipimo vya kutosha katika maabara zetu. Mazoea ya kusema ni kazi ya Mungu pia yanaturudisha nyuma wakati asilimia kubwa ya matatizo ya kiafya yanaletwa na watu wasiofanya kazi zao kiufanisi na huduma duni.
   
 11. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unachosema ni kweli, lakini utasikilizwa ndugu yangu labda aseme Obama au Gordon
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha ha Sikonge,

  Tabora kuna fisadi papa Rostam Azizi. Yeye pekee anachota pesa za serikali zenye uwezo wa kujenga university kama nne hivi (zenye hadhi ya Muhimbili).

  Itabidi kwanza Tabora muwaombe msamaha watanzania kwa kuchagua wabunge f......g - fisadi papa (Rostam) na spika aliyesaidia kupitisha kwa speed zake za kizembe bajeti mbofu mbofu ya mwaka huu (mzee wa vimada - six).
   
 13. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwa taarifa ni kwamba hicho chuo kinachotaka kujengwa sio kipya ila itakuwa ni Main Campus ya Chuo Kikuu cha Muhimbili. Wazo ya kuazisha hiyo campus ilikuwapo hata kabla ya wazo la kikwete la kuanzisha chuo kikuu cha Dodoma.

  Kikwete anachofanya sasa hivi ni kuupigia chapuo mpango wa serikali yake wa kupanua na kuboresha huduma za afya (Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi MMAM). Mpango huu Utahitaji wataalamu wengi sana wa afya hivyo inabidi vyuo vya afya viwezeshwe ili kuweza kufanikisha mapango huo.
   
 14. K

  Kaingilila Member

  #14
  Jul 1, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivyo vyuo vinavyojengwa wahadhiri wanatoka wapi? Na mbona viongozi wetu wanapenda vyuo vingi vidogo vidogo ambavyo havina ufanisi? Kwa sababu ninachojua vyuo vingi hapa kwetu ukiacha upungufu wa vitendea kazi na majengo mabovu. Kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri kiasi kwamba wahadhiri walewale wanafundisha vyuo zaidi ya viwili au vitatu. Hii inachangia kuwa na wataalam wababaishaji wanapohitimu masomo yao. Matokeo yake vifo na magonjwa yanazidi kuongezeka baada ya kupungua.
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,495
  Trophy Points: 280
  Mloganzila ni kijiji kilichopo maeneo ya kibamba CCM, wilaya ya kisarawe. Ukifika kibamba CCM ukitokea mjini unaingia kushoto, kama Km3-4 hivi kama sikosei.
   
 16. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Sikonge, hapo ndipo haswa kwenye point... Unajua Dar tayari ipo imejaa lukuki na hakuna mipango yoyote siku za usoni kujaribu kupunguza msongamano, then wanakuja na hili!?!!? ni kweli kwa nini wasipeleke mikoa ya mangaribi manake angalia kuna KCMC (kaskazini mashariki), Bugando (Kaskazini na mangaribi) kisha kusini hakuna chuo kikubwa cha afya... sasa hii kuongeza lijichuo jingine Dar ni kuzidisha msongamano kwenye kibiriti kilichojaa.... nikiulizwa nitasema wakijenge (Tabora - central to west) au hata ikiwezekana kipelekwe Mbeya au japo Iringa tujue moja.... jamani Tanzania hii yetu itajengekaje wakati maendeleo tunayavutia kule ambapo tumerithishwa na wakoloni, ina maana sisi hatutaweza kujenga from scratch.... may be ni kweli manke kikubwa tulichowahi ongelea kuanzisha/kujenga ilikuwa CDA (Makao Makuu Dodoma, now more than 30 years and counting)....


  Mkuu Josh M, naomba kwa hili nipingane kidogo na wewe... Kwa uelewa wangu na kutembelea karibu asilimia kubwa ya Tanzania, nimegundua kuwa Tanzania tupo nyuma sana katika fani ya elimu na afya.... Hatuna madaktari wa kutosha na vifo vingi maeneo ya vijijini vinatokana na kukosa tiba/ushauri mbadala wakati muafaka... kuongoze vyuo vya afya kutapelekea kuwa na madaktari wengi na hii inaweza kutusaidia kupunguza vifo na kuokoa jamii kubwa ya waTanzania..... hivyo hata kama kuna vyuo vikuu 1000, sioni tatizo kama uwezo upo kujenga vyuo vya afya na ualimu...

  naomba kuwakilisha...
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi chuo kikuu cha Dodoma kinatarajiwa kuchukua wanafunzi wangapi? na hicho cha Afya kitatarajiwa kuchukuwa wanafunzi wa ngapi?
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa tetesi changu UDOM mwaka huu pekee watakuwa wanafunzi 20,000 pamoja na fani nyingine na pia wanafunzi wanaosoma udkatari watakuwa kama 100 hivi kwasababu hiyo ni bora kuboresha vyuo vingine kwanza, maana hata hivi vya binafsi vinaweza kuchukua kwa muda wanafunzi wengine, na pia mimi naona kuna haja ya kuboresha kwanza vyuo vingine kwa miundombinu kwanza na kuanza vingine, tutakuwa tunafanya vitu nusunusu, sijaona watu kama wanachukulia kwa uzito chuo cha Sokoine university. Mimi nasema tuboreshe kwanza hivi tulivyokuwa navyo kuliko kuanza kujenga vingine na kuweza, hata kama tupo nyuma, Kwani Uganda wana vyuo vingapi?? Mbona wanatoa madaktari wengi kuliko Tanzania?? Jamani tume makini sana na kuanzisha vyuo. Sijakataa kuanzisha vyuo ni kitu kizuri ni lazima mikakati iwepo pia ili kujenga jamii bora zaidi na kutoa wahitimu bora zaidi na vifaa vya kufundishia
   
 19. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sijakataa kuanzisha vyuo vingine ni kitu kizuri sana kwa Taifa letu, lakini isije kutokea na kusahau kushughulikia vyuo vingine ambavyo tunavyo tayari. wewe mwenyewe shaidi, sijajua kuwa chuo cha Dodoma, au UDSM wamepewa bajeti shilingi ngapi?? na hapa ndipo unaweza kujua kitu nasema nini?? Kuna uwezekano huo mkubwa na kutazama na rasilimali zote kupeleka sehemu moja tu. hii itakuwa ni Hatari sana
   
 20. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kilandu,
  Bado tuna uhaba wa wahadhiri katika nchi yetu hasa katika hizi fani za sayansi utabibu ukiwa mojawapo. Inawezekana wanafanya hivyo ili walimu walioko Muhimbili waweze pia kufundisha katika chuo hicho tofauti na kikipelekwa Iringa na kwingineko ambako inaweza ikawa ni tatizo kupata walimu wa kutosha. Huo ni mtazamo wangu.
   
Loading...