Chuo Kikuu kina wenyewe bwana

Chuo Kikuu kina wenyewe bwana

Chura

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,425
Reaction score
2,528
Kila mtanzania anaongea lake na kulia kivyake huyu analia ajila zimefungiwa , yule analia kafoji vyeti, Wanunuzi wanalia pesa hakuna , wafanyabiashara wanalia wateja hakuna, huyu analalamika hakuna posho yule analia mwanaye haendi chuo vilio ni vingi kwa kweli,Na wengine wanasubiri kulia kile kilio cha jela ya mafisadi, ila asilimia kubwa ya watu niliongea nao wanonyesha kusoneneshwa na vigezo vya udahili vyuo mwaka huu kwa hofu kwamba wanafunzi wengi watatoswa hasahasa kwa wale wenye diploma wanatakiwa wawe na kuanzia GPA ya 3.5 kwa mnaosoma au mlio soma vyuo vikuu hususani kwa kozi za sayansi mtajua kupata GPA ya upper second kupanda juu ilivyo ishu kwa maana hiyo ni watanzania wachache sana watadahiliwa kwenda vyuo vikuu wakitokea ngazi ya stashahada kwa hiyo wale dada zetu wa IFM na CBE waliokuwa wanasoma kwa mashauzi mguu kwenye sofa kwa kigezo kwamba wenyewe hawasomei sifa eti wanasoma kufauru yani wale waliokuwa wanasoma kutafuta GPA ya pass 2.0 sasa imekula kwao.Pia kwa wale wazee walioteleza kidogo wenye GPA zakuanzia 3.0 mpaka 3.4 nawapa pole wasikate tamaa MUNGU yupo. Division Four plus zile Three ambazo marks hazifikii uzito wa 4 hawa wote Shahada wataisikia kwenye maono.

Swala zima la matokeo linaendana na sera za ajira za serikali husika ukiona nafasi ya elimu inatolewa au inatengenezwa kwa watu wachache ujue basi mfumo wa ajira hauruhusu ajira kwa watu wengi. Wanasiasa walipokuwa wanasema vijana ni bomu linalosubiri kulipuka sijui nyie mliwaelewaje???
kwa kukusaidia Jiulize kati ya hawa vijana wawili ni yupi bomu la kurusha kwa mkono (grenade) na ni yupi Bomu la nyuklia (atomic bomb) Kijana wa kwanza ni yule aliyemtaani bila ajira asiye na elimu kubwa yani la saba, form four ,form six na stashahada, Kijana wa pili ni yule aliye mtaani bila ajira mwenye elimu kuanzia Shahada, masters na PHd . Wote hawa ni mabomu yanayosubiri kulipuka ila ukishajua ni bomu lipi lina madhara zaidi likilipuka basi hutashangaa napokwambia wengi hawataenda chuo kikuu

Tujitahidi kuhudhuria sana semina za ujasiliamali tujikite huko ila hii dhana ya kusoma ili uajiliwe mwisho wa siku utajikuta kwenye wahanga wa kuisoma namba
Poleni wote mliokumbwa na hii kasumba MUNGU yupo

"Mchagua hovyo akitendewa hovyo asiseme hovyo" Jenerali Ulimwengu.
 
Mkuu umeshauri, umelalamika, umepiga vijembe, umenung'unika nk. Big up Mkuu. Mm nasubiri mabomu yaanze kulipuka.
 
Back
Top Bottom