Chuo Kikuu Huria cha Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Magobe T, Nov 23, 2008.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Nilifurahi sana Chuo Kikuu Huria kilipoanzishwa hapa nchini. Nafurahi sana pia kuona kuwa Watanzania wengi wamejiunga na chuo hiki kiasi kwamba kama kisingekuwapo basi watu wengi wangekosa nafasi ya kujiendeleza hasa kwa kiwango cha elimu ya chuo kikuu. Kuna wanafunzi wa rika zote: vijana sana, vijana wa kati, middle age na wazee. Hii ni nzuri!

  Kinachonisikitisha ni huduma duni na ukosefu wa ufanisi mzuri katika kutunza data na kuhakiki kazi za wanafunzi. Hii inakatisha tamaa sana! Halafu pia naona wanaotoa huduma ni kama watu wamechoka vile. Yaani, baadhi wanaonekana kama wamelazimishwa - hawana motisha! Sijui malipo ndiyo madogo au ni tabia tu ya utendaji kazi.

  Ukiuluza kitu unajibiwa kimkato sana na kama hujaelewa unaambiwa unapoteza muda kwa vile wengine ambao wako nyuma yako nao wanangojea huduma kama wewe. Na mara nyingi hao wanaosema hivyo huwa wana kauli ambayo ni 'arrogant'. Na hata hao wanaowasema 'wengine' kama watauliza wafafanuliwe kitu, utasikia kama ugomvi tena.

  Kwa hiyo, utakuta kwamba kuliko kwenda kuuliza kitu unaamua kufanya jinsi unavyoona wewe na wakati mwingine unaweza kupatia au kukosea. Hivi hatuna njia ya kuboresha huduma katika Regional Centres zetu na hata pale Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria, Kinondoni?

  Tuchangie namna ya kuboresha huduma Chuo Kikuu Huria ili kiweze kutoa huduma nzuri zaidi. Mimi naona huduma zake ni kama level ya sekondari - yaani, ukiwa maeneo yale hupati challenge ya kukufanya uone kama ni level ya chuo kikuu hasa kwenye Regional Centres na hata pale Makao Makuu. Je, niko 'prejudiced' au na nyinyi mnaona hivyo?
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,798
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  ni wakati mwafaka wa marekebisho sasa. Mabadiliko mapya ya mwaka huu yanatutia tumbo joto. Kila mahali kwenye mkanganyiko wa matokeo unaambiwa itabidi urudie upya, chuo kitasomwa miaka 10 kwa digrii ya kwanza!
   
Loading...