Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chaipinga TCU, Chasema Hakijadahili wanafunzi wasio na sifa

Naisoma360

JF-Expert Member
Jan 23, 2015
821
491
UDSM.jpg

SIKU moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania (NACTE).

Taarifa ya UDSM Kwa upande wake, UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga aliliambia gazeti hili jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.

“Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tulivyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:

“Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki”, alisema Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.
Alisema kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.

Alisema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.

“Yawezekana kuna taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga.

Chanzo: Habari Leo
 
jambo zuri ni kuwa tcu imesema hao wa2 inaowashuku wapeleke vyeti so badae itajulikana tu.
 

Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) .

UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.

“Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:

“Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki”, alisema

Profesa Luoga alisema uhakiki ambao umefanywa na TCU na kutoa idadi ya wanafunzi 224 wanaosoma chuoni hapo, kuhakikisha wanawasilisha ushahidi wa nyaraka zao, wanaufanyia kazi, kwani kuna uwezekano tume hiyo haina taarifa kuhusu programu zinazoendeshwa na chuo hicho.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.

Alisema kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.

Alisema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.

“Yawezekana kuna taarifa ambazo hazijakaa sawa, tumepokea taarifa ya TCU sisi kama chuo ni jukumu letu kuitekeleza,” alieleza Profesa Luoga.
 
UDSM si sehemu ya vilaza!
Wajitafakari upya hao Tcu ikiwezekana Ndalichako ajiuzulu
 
Mbona taarifa inajieleza, UDSM yawezekana wanachukuwa watu wasiokuwa na ufaulu wa kiwango cha NECTA ambacho wahakiki wametumia kuhakiki wanafunzi na then kuwa Upgrade. UDSM inatakiwa kutoa justification ya authenticity ya program zao katika kukuza sifa za hao watu kuwa university materials.
 
tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga.
Daudi angefanyia maujanja yake udsm angenyang'anywa digrii yake.
 
Drama hizi zitaisha lini, la madawa naona sasa linapoteza mvuto, sasa TCU nao wameanza kweli tutafika ile nchi ya ahadi aliyetuahidi MUSA; nchi ya V-WONDER kweli?? Na hapo bunge alijaanza vikao, another drama on the way.
 
Huyu mama ndalichako yeye kila leo anakuja na vikorombezo vyake mara gpa mara diploma yaani ili mradi kuwavuruga watanzania ona sasa leo mnaanza kushikana mashati nyi wenyewe haki mungu hii nchi yetu sijui imepatwa na nini kila leo series zinakuja mpya unashindwa ipi uanza nayo kuangalia.
 
Niliwahi kwenda bodi ya mikopo nikifatilia mkopo...nikawatajia chuo ninachotokea wakaniuliza hivi hicho chuo ni cha serikali au binafsi....??? Nilishtuka sana taasisi inayohusika na elimu haina taarifa ya vyuo.... Hii ni Tanzania... Kazi yao ni kupokea maagizo tu.
 
Back
Top Bottom