Kitotonya
Senior Member
- Dec 9, 2011
- 188
- 60
kwanza kabisa napenda kutanguliza shukrani kwa wana jf kutokana na jinsi ninavyo nufaika,hasa pale ninapotaka msaada.
kiukweli kwa sasa vijana wengi hasa wanao maliza la saba na form four ukiwauliza unataka fani gani hawaishi kukuambia mi nataka udereva.wanasahau kwamba udereva kwa sasa sio dili kwa maana watu wengi ni madereva na wengi wanaishia kuendesha daladala na vibajaji. lakini pia wanasahau kuna uopareta wa magreda na sindilia pamoja na vijiko vya kuchotea vifusi.sasa wana jf nimemshauri rafiki yangu aende kusomea hayo maujuzi maana watu wake ni wachache.
swali je ni vyuo gani vinavyotoa hizo kozi na gharama yake ni shiling ngapi.
naomba kuwakilisha.

Chuo cha udereva wa mitambo ya ujenzi kipo Mbeya Tech kwa nchi nzima,
Chuo cha bandari kinajitahidi kwa mbali lakini hakikidhi matakwa ya wataamu wa mitambo ya ujenzi
Kwenye mkutano wa Makandarasi juzi tumeishauri serikali kuvipa uwezo vyuo vingine kama VETA nk viweze kutoa mafunzo hayo ili kusaidia tatozo la ukosefu wa wataalamu hawa!