Chuo cha Mipango kupanuliwa zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo cha Mipango kupanuliwa zaidi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 24, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SERIKALI imesema itajenga jengo la ghorofa nane la taaluma katika Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) na kusaidia ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya chuo hicho.

  Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa na waziri wa fedha Mustafa Mkulo wakati wa mahafali ya 24 ya chuo hicho na kubainisha kwamba serikali inatambua umuhimu wa chuo hicho hivyo zipo kila sababu za kuhakisha chuo hicho kinakua zaidi.

  Alisema hicho ni chuo pekee kinachotoa wataalam mbalimbali wa kada ya mipango hapa nchini ambapo mpaka hivi sasa kimeshatoa zaidi ya wataalamu 3,000.

  Waziri Mkulo alisema serikali kupiti Wizara ya Fedha na Uchumi, itagharamia na kumaliza ujenzi wa jengo la ghorofa nane linalojengwa eneo la Miyuji mjini hapa ambayo ni sehemu ya upanuzi wa chuo hicho.

  Aidha waziri huyo alisema serikali itahakikisha wahitimu wanaomaliza chuoni hapo wanapatiwa ajira moja kwa moja ili waondokane na adha ya kutafuta ajira baada ya kuhitimu masomo yao.

  Mkulo aliwatunuku jumla ya wahitimu 712 waliomaliza masomo yao katika ngazi mbalimbali ikiwemo cheti, stashahada, shahada, shahada ya uzamili, Shahada ya Maendeleo ya Mikoa na Rasilimali Watu.
   
Loading...