Chuo cha marubani kujengwa Tanzania

Chuo cha marubani kujengwa Tanzania

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
SERIKALI ya China kwa kushirikiana na Afrika Kusini, zimetoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha marubani nchini, ikiwa ni juhudi za kumuunga mkono Rais John Magufuli. Kauli hiyo ilitolewa jijini Arusha na Mkuu wa Chuo cha Usarishaji nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa ambaye amesema nchi hizo zimeona jitihada za serikali kwenye kuimarisha usari wa anga nchini na kuwa ni vyema wakatoa fedha hizo ili kujenga chuo hicho katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Profesa Mganilwa amesema mbali ya kutoa pesa, pia nchi hizo zimeahidi kutoa wataalamu wa kufundisha wanafunzi katika kozi ya urubani na kila mwaka marubani 20 wanatarajiwa kuhitimu chuoni hapo. Alisema katika ukanda wa Afrika, Tanzania itakuwa nchi ya pili yenye Chuo Kikuu cha Urubani, ukiacha Afrika Kusini.

Alisema kuwa wafadhili wakubwa, wameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kukiendeleza chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kutoa wataalamu wa ufundishaji. Mkuu huyo alisema tayari serikali imeshatenga pesa kwa ajili ya ununuzi wa ndege tano za mafunzo kwa wanafunzi, watakaojiunga katika chuo hicho na kinachosubiriwa kwa sasa ni kuanza kwa ujenzi wa chuo hicho huko KIA.

“Maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo hicho yako tayari, pesa za nchi za China na Afrika Kusini ipo, serikali imeshatenga pia ununuzi wa ndege za mafunzo na eneo la ujenzi wa chuo liko tayari na kinachosubiri ni kuanza kwa ujenzi tu,” alisema Profesa Mganilwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni (KADCO) inayoendesha KIA, Christopher Mukoma alisema kuwa serikali imekiria jambo jema kwa faida ya nchi na katika kuunga mkono jitihada hizo za serikali katika kukuza usari wa anga, tayari wameshakabidhi hekta 60 kwa NIT kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.

Mukoma alisema kuwa KADCO, imeunga mkono jitihada za serikali katika kuimarisha usari wa anga na ndio maana imetoa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu cha marubani, ambacho kinakuwa cha pili Afrika. Alisema kuanzishwa kwa chuo hicho KIA, kuna vitu vingi vya ufundishaji.

Meneja wa Ufundi na Uendeshaji (KADCO), Mathew Ndossi alisema kuwa serikali ilichelewa kuanzisha Chuo Kikuu cha marubani. Alisema kuwa kuanzishwa kwa chuo hicho ni ukombozi kwa Watanzania na kunaimarisha zaidi usari wa anga. Ndosi alitaka chuo hicho kukamilika katika muda muafaka ili serikali iweze kuibua marubani wa uhakika kwa ajili ya kuendesha ndege za hapa nchini.

Meneja wa Umiliki na Mazingira wa KADCO, Hamis Tembele alisema KIA ina eneo la hekta 109 lililo wazi, lakini wametoa kwa NIT hekta 60 kwa ajili ya ujenzi wa chuo na pia wametoa hanga kwa ajili ya madarasa na karakana
 
Back
Top Bottom