Chuo cha hali ya hewa

thegreen

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
369
Reaction score
172
habarini wakuu, jamani sijui kama ndo kinavyoitwa au la. ila ningependa kufahamishwa kwa anaejua mahali chuo kinachofundisha fani hii. labda anisaidie kwa kuniambia kipo wapi kwa hapa Dar es salaam pia matawi yake yako mikoa ipi. ni matumaini yangu nimeeleweka, asanteni na naomba kuwasilisha
 
Watu wa jangwani na msimbazi chuo hiki hautaki ata kukisikia kutokana na dhahama iliyotukumba karibuni....
 
Watu wa jangwani na msimbazi chuo hiki hautaki ata kukisikia kutokana na dhahama iliyotukumba karibuni....

ni kitu gani kimewakumba jamani. tafadhali naomba utufahamishe na sie mkuu.
 
ni kitu gani kimewakumba jamani. tafadhali naomba utufahamishe na sie mkuu.

Mfano jana huyo mtu alikuwepo huko kwenye hali ya hewa sijui alijisahau kidogo maana koki zilimwaga maji si kitoto!
 

Hiyo course inatolewa pale WDMI maarufu kama chuo cha maji near COET
 
kipo kigoma,nadhan ukiajiriwa ndo unapelekwa pale kwa udhamini wa TMA..
 
Chuo cha usimamizi wa maji (wdmi) kozi inaitwa hydrology and meteology diploma miaka 3. Nipo hapo ila nasoma kozi tofauti
 
Kwa sasa utaratibu ni kwamba ajira zinatangazwa, na unaomba kama kawaida lakini kwa masharti ya kujiunga na kozi ya hali ya hewa kigoma. Hii ni kwa wale waliosoma combinations za PCM na PGM tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…