Chuo cha Ardhi na kauli mbiu ya Rais

MATEGUZYO

Member
Sep 5, 2019
44
17
CHUO CHA ARDHI MOROGORO KINAVYOTEKELEZA KWA VITENDO KAULI YA ‘HAPA KAZI TUU’

1582115468-dr.%20Adam.jpg


Imewekwa: 19th February, 2020

Chuo cha Ardhi Morogora kilianza mwaka 1987 kwa sheria ya Bunge Na. 3 ya Chuo cha Ardhi ya mwaka 1974, wakati huo kikiwa tawi la Chuo cha Ardhi kilichokuwa Dar es Salaam. Chuo hiki kilianzishwa kwa lengo la kutoa taaluma ya masuala mbalimbali ya Ardhi, kutoa huduma kwa jamii pamoja na kufanya tafiti mbalimbali.

Katika nyakati tofauti tofauti, Chuo kimekuwa kikifanya marekebisho katika kozi zake na mitaala kwa lengo la kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya soko kwa ujumla. Katika kutekeleza hili, chuo cha Ardhi Morogoro kila baada ya miaka ya miaka 3 hupitia mitaala yake na kuona wapi pa kurekebisha ili kutoa elimu na taaluma bora zaidi kwa wanafunzi ambao ndiyo wataalam wa masuala ya Ardhi kwa taifa la kesho

Chuo cha Ardhi Morogoro kinasimamiwa na Serikali na hivyo kina usajili kamili yaani (full registration) pamoja na ithibati kamili (full accredidation) ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Kwa maana hiyo, mara nyingi sana Chuo hupokea ushauri na maagizo kutoka NACTE namna nzuri ya kusimamia na kuboresha mitaala yake

Uongozi wa chuo cha Ardhi Morogoro unajivunia sana Chuo kuwa na usajili na ithibati kamili kwani, imesaidia sana kuongeza uwezo na kujipanua zaidi kwa kuongeza udahili wa wanafunzi wengi kadri miaka inavyosonga mbele na kupanua wigo wa kutoa kozi mbalimbali kulingana na mahitaji yaliyopo kwa jamii kitu ambacho kimekuwa na tija kubwa kwa Taifa. Hadi sasa Chuo kinatoa mafunzo katika fani za upimaji ardhi (Geomatics) pamoja na Mipango miji na vijiji (Urban and Reoginal Planning) kwa kutumia mitaala bora inayojikita zaidi katika utendaji kazi mahiri na weledi.

Katika awamu hii ya tano Chuo cha Ardhi Morogoro kimefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 150 hadi kufikia 500 pamoja na kununua vifaa bora na vya kisasa vya kujifunzia kama vile RTK GPS, Total Station na software za GIS za kila aina. Haya ni mafanikio makubwa kwa chuo hiki kwa sababu, siyo kwamba wanafunzi wanapata utaalam tuu bali wanajengewa uwezo wa kujiamini na kuwa wabunifu kiasi cha kufanya kazi popote pale

Katika mafunzo ya vitendo yaani (Field work), mwanafunzi haruhusiwi kwenda mwenyewe uwandani. Chuo mara nyingi hufanya mawasiliano na Halmashauri mbalimbali nchini kujua kama kuna miradi ya upimaji na upangaji ili kuwapeleka wanafunzi kwenye hiyo miradi kama sehemu ya mafunzo. Wanafunzi wanapokuwa uwandani, hufanya kazi zote za uwandani wakishirikiana na waalimu wao pamoja na wataalam kutoka katika Halshauri zinazotekeleza miradi husika.

Pamoja na haya yote, Chuo cha Ardhi Morogoro kinasimamia na kuendesha miradi mbalimbali nchini kama sehemu ya kutoa huduma kwa jamii na kuwajengea wanafunzi uwezo kwa vitendo. Mkuu wa Chuo pamoja na uongozi wameweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha wanafunzi wanatekeleza kwa vitendo yale wanayojifunza darasani. Lengo kubwa ni kuhakikisha chuo kinazalisha wataalam bora wanaozingatia weledi katika kutoa huduma bora kwenye jamii inayowazunguka.

Baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Chuo cha Ardhi Morogoro ni pamoja na urasimishaji wa makazi holela katika Mitaa 72, Kata 34 kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Iringa na Tabora. Mradi mwingine ni wa Upimaji na Upangaji katika mikoa ya Tanga, Simiyu, Bariadi na Kigoma ambao umekuwa na mafanikio makubwa kwa viwanja vingi kupangiwa matumizi na kupimwa.

Chuo cha Ardhi Morogoro kina majukumu mengi na mikakati mbalimbali imewekwa ili kutekeleza majukumu hayo. Chuo kimeandaa mpango mkakati maalumu katika utekelezaji wa majukumu yake ambao umejikita zaidi katika kuendelea kuongeza udahili wa wanafunzi, kuboresha masuala yote ya kitaaluma,kutoa nafasi kwa watumishi wake kujiendeleza kielimu ili kuongeza maarifa, kuendelea kuboresha na kupitia mitaala, kuanzisha kozi nyingine mpya katika fani mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wataalam wa masuala ya sekta ya Ardhi nchini.
 
Back
Top Bottom