Chuo au Kureseat? Ushauri kwa Waliopata D Moja Form Four

Sahel 234

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
23
Reaction score
45
Wakuu habari, naomba ushauri. Kijana wangu amemaliza kidato cha nne mwaka 2023 akichukua combination za arts, lakini amepata D moja tu (Kiswahili). Je, katika hali hii anaweza kupata nafasi ya kujiunga na chuo bila kureseat? Kama haiwezekani, ni vituo gani vinajulikana kwa kufaulisha vizuri wanaorudia mitihani?
 
Vyuo vya kati wanahitaji D's nne(4) Ili waweze kukupa nafasi ila kwanini asiende veta tu kupata ujuzi mkuu?
 
Ni kweli VETA ni sehemu nzuri ya kupata ujuzi, lakini kwa upande wake bado ana malengo ya kuendelea zaidi kielimu — kuanzia ngazi ya cheti, kisha diploma na hatimaye chuo kikuu. Ndio maana nilitaka kufahamu kama kuna vyuo vya kati vinavyokubali wanafunzi wenye matokeo ya chini ya vigezo vya kawaida (chini ya D nne), ili angalau aanze huko na kuendelea hatua kwa hatua.
 
Mimi kama NACTE naahidi sitokubali ajiunge na chuo cha kati vilivyosajiliwa chini yangu kwa sababu anatakiwa awe na D nne.
 
Wakuu habari, naomba ushauri. Kijana wangu amemaliza kidato cha nne mwaka 2023 akichukua combination za arts, lakini amepata D moja tu (Kiswahili). Je, katika hali hii anaweza kupata nafasi ya kujiunga na chuo bila kureseat? Kama haiwezekani, ni vituo gani vinajulikana kwa kufaulisha vizuri wanaorudia mitihani?
Vyuo vingi angalau d nne tena masomo yasiwe ya dini.kwa huyo wako hapo usichoshe akili sana huyo angeenda veta au afanye mambo mengine mbali na elimu tuu

Kwa sababu inaonesha kama hayupo seriously nakitabu lakn kama nyuma alokuwa anafanya vizuri basi kurisiti pia inaweza kuwa chaguo bora.

Lakn angalizo kabla hujafanya hayo maamuzi ya kurisiti hakikisha umechunguza ufaulu wake wanyuma.

Kama wew ni mzazi unaefatilia mwenendo wa mtoto wako akiwa shuleni basi itakuwa unajua kila kitu
 
Back
Top Bottom