Chunusi zinanikosesha mke

Chunusi zinanikosesha mke

King snr

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
1,165
Reaction score
1,474
Habarini wakuu,

Nilileta topic ambayo ni 'akiniona anajificha, atakuwa ananipenda au hisia zangu tu?' kutokana na ushauri wa wadau ikanbidi nikamtokee,nilijipanga mtoto wa kiume nikatupia niwezavyo nikaenda kwao.

Ile nafika tu wa kwanza kukutana nae ni mama ake basi nikajikaza kiume nikapiga nae stori mbili tatu nikamwambia niliyemfata basi yule mama alikuwa ananiheshimu pale mtaani alimwita mtoto wake bila kusita alafu mwenyewe akatoweka.

Ile amefika tu sikutaka kupoteza muda nilihofia asije akanikimbia kama tabia yake ilivyo nikamtemea madini pale nikahis kama kanielewa hivi, akasema nisubiri akaingia ndan akakaa mda mrefu kidogo nikahisi labda kanikimbia tena.

Mara nikamwona anakuja kanibebea bahasha ya kaki akanipa akasema nikaifungue kwetu,nikaondoka maswali mengi kichwani nikahisi labda kanipa zawadi.

Kufika nyumbani kufungua ile bahasha nakutana na kioo na dawa kwnye kopo flani hivi, nikajiulza vya nini hivi nikachukua kioo kujiangalia daah! Chunusi zimeshamiri usoni, kumbe kioo muhimu, sasa sijui ndo kanikataa au.?

Ushauri wenu




 
Chunusi pengine zinakukosesha ''wasichana'' na si mke. Mke huwa anatoka kwa MUNGU na si vinginevyo ....

KUMBUKA YAFUATAYO:::

Wasichana - Jinsia ya kike ambao hawajakomaa 'sana' kiakili, kifikra na kimtazamo
Wanawake - Jinsia ya kike ambao wamekomaa kiakili, kifikra na kimtazamo
Mke - 'Mwanamke' unayepewa na MUNGU kwa ajili ya kushiriki naye uhai.
 
you-serious-bro_zps0eef9b1a.jpg
 
Back
Top Bottom