Chungu na tamu za bajeti yetu 2021/22

Kagosi DJ

Member
May 5, 2020
19
69
Habari wana JF, Ni matumaini yangu tu, wazima wa afya tele, ashukuliwe MUNGU kwa kutupa hii nafasi.

Naomba leo tuongee kuhusu BAJETI yetu ya mwaka 2021/22. Ambayo ndio kwanza haijamaliza siku 30 tangu utekelezaji wake uanze.

Makadirio ya mapato na mipango ya matumizi ya mapato yatakayo patikana kwa manufaa ya wananchi katika kipindi Fulani, Hito haswaa ndiyo maana halisi ya bajeti. Serikali inaweka mikakati ya jinsi ya kupata fedha na Kisha jinsi ya kuzitumia fedha hizo. Kwa nchi yetu BAJETI huwa ya kipindi Cha mwaka mmoja!

BAJETI ya mwaka 2021/22 inakadiliwa kukusanya na kutumia jumla ya Trilioni 36.33. Ambapo jumla ya Trilioni 26.03 zitatokana na makusanyo ya ndani, sawa na 71.7%. wadau wa maendeleo na wanatarajiwa kuchangia msaada wa jumla ya trilioni 2.96 sawa na asilimia 8.1 ya BAJETI yote.

NI ZIPI CHUNGU ZA BAJETI HII?

1. KUHUDUMIA DENI LA TAIFA

Pamoja na kuwa deni la taifa bado ni himilivu lakini ukubwa wake unadumaza maendeleo ya Taifa. Asilimia 29% ya bajeti inatumika Kulipa deni la taifa. Huu ni mzigo mzito kwa taifa ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe. Uwiano wa fedha zinazo tumika Kulipa deni na zile zinazo tumika katika maendeleo ni mdogo Sana yaani Ni asilimia 29% kwa 37% jitihada za dhati ziendelee kuchukuliwa kupunguza utegemezi ili angalau mapato yaanze kutumika kuwanufaisha zaidi wananchi. Ni Jambo jema kwamba bajeti ya mwaka huu imepunguza utegemezi kwa asilimia 3% lakini haitoshi. Bado serikali inatarajia misaada na mikopo ya masharti nafuu wa zaidi ya shilingi trilioni 2.96, sawa na asilimia 8.1% ya bajeti yote. Hiyo Ni kwa wahisani wa nje pekee.

2. KUDUMAZA SEKTA YA KILIMO
Sekta ya kilimo inatoa mchango mkubwa kuliko sekta nyingine yoyote katika pato la taifa, zaidi ya asilimia 26.9% ya pato la taifa inatokana na kilimo zaidi ya asilimia 80% ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo.

Kwenye Bajeti ya mwaka 2021/22 kunabaadhi ya tozo zinaweza kudumaza zaidi ukuaji wa sekta hi ambayo kiujumla inakua kwa asilimia 4.9% ukuaji huu sio mzuri kabisa.

Utozaji wa ada ya huduma ya umwagiliaji ambayo ni asilimia 5% ya mavuno ya mwaka. Serikali inapaswa kutoa huduma hii kwa ada nafuu zaidi ikiwezekana iwe bure kabisa. Sekta hii hivi Sasa inahitaji kutengenezewa mazingira yanayo wavutia zaidi wawekezaji kuliko kuanza kuiongezea tozo na Kodi zisizo za lazima. Hii inaweza kupelekea kushuka kwa mchango wake kwenye pato la taifa.

Pili serikali inampango wa Kutoza Kodi ya Zuio kwa kiwango cha asilimia mbili 2% kwenye malipo yanayohusisha mauzo ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Hii inadumaza zaidi sekta hi kuliko kuikomaza ili ilete manufaa zaidi Kwa Taifa.

3. KUDUMAZA MAENDELEO YA WATU NA USTAWI WA JAMII
Waziri wa fedha alihainisha kuwa Dhima kuu ya Bajeti hii ni “KUJENGA UCHUMI SHINDANI NA VIWANDA KWA MAENDELEO YA WATU” lakini utekerezaji wake haswaa haupo katika dhima husika kwa sababu zifuatazo:

(i) kuwepo kwa tozo na Kodi kandamizi zinazo weza kudumaza ushindani wa taifa katika soko la kimataifa, Kama vile kurekebisha sheria ya petrol sura 392. Ili kuongeza tozo ya mafuta ya taa kutoka shilingi 150 hadi shilingi 250. Pia Kuongeza shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli. Mafuta ni nishati muhimu kwa uchumi kupandisha Ushuru kutapelekea kupanda kwa gharama za uendeshaji wa uzalishaji jivyo kupandisha bei za bidhaa zinazo zarishwa nchini Ni dhahili kwamba bidhaa za ndani zitashindwa kushindana katika soko la kimataifa na hata kushindwa kupata soko la uhakika ndani ya nchi.

(ii)marekebisho katika Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki, Sura 306. kutoza shilingi 10 hadi 10,000 kwa kila muamala wa kutuma au kutoa fedha, hi inaongeza mzigo kwa watumiaji na itasababisha watumiaji wa huduma hii kutafuta njia mbadalaa hivyo serikali itakosa VAT iliyopatikana awali. Na hakuna ubora wa maisha katika gharama kubwa ya huduma za muhimu za kijamii.

Pia kutoza kiasi cha shilingi 10 hadi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu, kutadumaza malengo ya Taifa ya kufikia asilimia 80% ya watumiaji wa internet kutoka 49% iliyopo Sasa. Mabadiliko haya zitaongeza gharama za mawasiliano nchini. Pia kunauwezekano wa mabadiliko haya kuleta kikwazo kwa wananchi kufikia haki ya kujieleza na haki ya kupata taarifa kama ilivyoainishwa katika ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

4. BAJETI KUTO KUGUSIA UGONJWA WA UVIKO -19
moja ya Jambo linaloisumbua dunia hivi sasa Ni jinsi ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19. Ni Jambo la ajabu kwamba bajeti yetu haijaonesha jitihada zitakazo tumika kupambana na tatizo hili kubwa, licha ya serikali kukili kwamba ugonjwa huu bado upo. Hii itaifanya Bajeti kukumbana na 'suprises' ambazo zingeweza kutatuliwa mapema.

Bajeti imeainisha kwamba Wizara ya Fedha na Mipango imeanza majadiliano na IMF ya mkopo wa dharura (Rapid Credit Facility - RCF) wa dola za Marekani milioni 571. Hivyo watu bado wanaathirika na madhara ya ugonjwa huu lakini serikali haijatenga pesa yoyote ya ndani kushughurikia tatizo tunaendelea kusubili mazungimzo tupate mkopo.

UPANDE WA TAMU ZA BAJETI

1. KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI NCHINI

Bajeti imepunguza Kodi ya mapato ya ajira kutoka 9% hadi 8% na Kufuta tozo ya asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa kwa ajili ya
kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention Fee) kwa wanufaika pia, Kutenga jumla ya shilingi bilioni 449 kwa ajili ya kuwapandisha vyeo watumishi 92,619. Kwa mwaka huu wa fedha, Serikali kupunguza muda wa miaka 12 hadi 6 wa watumishi wa Jeshi la Polisi kupata mafao yatokanayo na utumishi wao. hii itapunguza ugumu wa maisha kwa wafanyakazi tofauti na ilivokua awali.

3. MSAMAHA WA KODI NA TOZO MBALIMBALI
Serikali imetoa msamaha wa Kodi kwenye maeneo mbali mbali ikiwemo. Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye Nyasi Bandia, kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye simu janja za mkononi (smart phones), Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za bima ya mifugo na Kufuta tozo ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi kwa hospitali zinazomilikiwa na taasisi za kidini. Kupunguza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi (Gaming tax on Winnings) kutoka asilimia 20% hadi asilimia 15%. hizi ni baadhi tu ya tozo na Kodi zilizo ondolewa.

4. KUBORESHA MIUNDOMBINU NA UTOAJI WA HUDUMA ZA JAMII
Bajeti ya mwaka 2021/22 imejikita katika kuboresha huduma za jamii Kama vile shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya miradi ya
reli ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa, shilingi trilioni 2.08 kwa ajili ya miradi ya barabara, ujenzi wa madaraja, na viwanja vya ndege, shilingi trilioni 2.34 kwa ajili yamiradi ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme ikiwemo mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere; shilingi bilioni 589.4 kwa ajili ya miradi ya maji mijini na vijijini; shilingi bilioni233.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Hii itaongeza ubora wa maisha kwa wananchi na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kijamii.

HITIMISHO,
Kwanza ningependa kuwashauri watanzania wenzangu kulipa Kodi bila udanganyifu wala kukwepa, maana uchumi wa nchi yetu unatutegemea sisi wananchi. Pili serikali itengeneze mazingira rafiki kwa watu Kulipa Kodi kwa hiyali yao. Usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi yanayo onekana wazi na yenye lengo la kuwanufaisha wananchi yanaweza kuongeza hamasa kwa wananchi Kulipa Kodi zaidi na hii inaweza kuongeza umoja wa kitaifa katika kupambana na changamoto za pamoja Kama Taifa.
Basi kazi iendelee!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom