Chunga sana maneno yako kwa wenzio

Nov 2, 2020
68
90
Maisha ni safari na hatua ndefu ambayo kila mmoja wetu anayo tafsiri mbali na hii niliyoitumia. Kwa muktadha huo,Kama binadam bado kuna mambo au vitu ambavyo vinatuunganisha kwa sauti moja, ikiwemo suala zima la hisia. Sio rahisi kuainisha hisia ni nini, Lakini zinawezekana kudhihirika kupitia matokeo yake kwenye maisha yetu.

Maneno ni moja kati ya vichocheo ambavyo vimekuwa na nafasi ya kujenga au kubomoa maisha ya wengi. Mfano ni kupitia majukwaa yetu tofauti humu, Kila mtu huwa na namna yake ya kufikisha au kutafuta mbadala katika yanayomsumbua. Lakini kwa bahati mbaya,Baadhi yetu tunapoona mtu ameleta kitu ambacho hakiendani na wewe tumekuwa na kawaida ya kutoa maneno au kauli ambazo kwa wakati huo, Hazina msaada kwa mlengwa au mleta mada.

Kumbuka, Kila unachochangia hapa kupitia maandishi yako,Kuna mtu kinamjenga au kinambomoa. Hivyo ni bora kuwa makini na maandishi yako,Kwani tumeshuhudia wengi wakitoa ushuhuda juu ya aidha ushauri alioupata humu ulivyomuongoza au ulivyompotosha.

Ijapokuwa kila mtu ana akili zake ,Lakini bado isiwe ni ruhusa ya kumuumiza mwenzako kisa una uhuru wa kutoa maoni. Bora kukaa kimya kabisa,Ubaki ukisoma thread za wengine huenda ukapata la kujifunza.

Youth Worker

Hardness,Teaches
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom