chumvini na miale ya nyuklia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chumvini na miale ya nyuklia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 18, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Chumvi hivi sasa imekuwa bonge la dili nchini China kufuatia uvumi kwamba chumvi yenye madini ya Iodine ni dawa ya kuzuia miale ya nyuklia, uvumi huo ulisababisha maelfu ya watu wavamie kwenye maduka madogo na makubwa kununua chumvi kwa wingi.
  Uvumi uliosambaa kwa njia ya ujumbe wa simu sms umepelekea uhaba wa chumvi nchini China na kuifanya serikali ya China iingilie kati na kuanzisha kampeni ya kuwatoa watu wasiwasi.

  Uvumi ulianza kwa taarifa kwamba madini ya Iodine yaliyopo kwenye chumvi yanasaidia kuzuia madhara ya miale ya nyuklia ambayo huenda ikaifikia China kufuatia kulipuka kwa kinu cha nishati ya nyuklia kwenye mji wa Fukushima nchini Japan.

  Uvumi ulisambaa kwamba mtu anapotumia kiasi kikubwa cha chumvi yenye madini ya Iodine basi mwili wake utaweza kujizuia na madhara ya miale ya nyuklia.

  Taarifa zaidi zilisambaa kuwa chumvi toka China ambayo hutokana na maji ya chumvi ya baharini haitakuwa salama kiafya kutokana na bahari kuchafuliwa na miale ya nyuklia toka Japan.

  Hali hiyo ilipelekea mamia ya watu wavamie maduka kugombania kununua kiasi kikubwa sana cha paketi za chumvi kama akiba ya kujilinda na miale ya nyuklia.

  Ndani ya muda mfupi, kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa chumvi nchini China kiasi cha serikali ya China kuanzisha kampeni ya kuwaonya watu wasinunue na wala wasitumie kiasi kikubwa sana cha chumvi kuliko kawaida.

  Angalia VIDEO chini kuona jinsi Wachina walivyokuwa wakigombania chumvi jana.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...