Chumba cha uwanja wa ndege terminal 3 cha waka moto

mahenda255

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2018
Posts
515
Reaction score
702
Dar es Salaam. Chumba kimojawapo cha ofisi kilichopo katika jengo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jengo la Terminal 3, kimeungua kwa moto ambao bado chanzo hakijajulikana.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto JNIA, Maria Kulaya ameiambia Mwananchi leo Jumapili Machi 24, 2019 kuwa tukio hilo lilitokea jana jioni baada ya moto huo kuzuka ghafla katika chumba cha ofisi hiyo kinachotumiwa na wakandarasi
Kulaya amesema ingawa haukuwa na madhara kwa kuwa jeshi hilo liliwahi baada ya kupewa taarifa, lakini baadhi ya vifaa na nyaraka zilizokuwemo kwenye chumba hicho zimeteketezwa na moto huo.
“Kamishna Jeneral wa Zimamoto, Tobias Andengenye alitembelea leo hapa na tayari tumeshaanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huu. Tutoa taarifa rasmi baada ya kukamilika kwa mchakato huu,”amesema.

Source: Mwananchi
 
Picha tafadhali tunaweza kujua hata chanzo chake kwa picha tuionapo
 
Yaleyale! Tutaishia kusema "yasiyojulikana".
 
Hayatuhusu hayo tuko kupambana na akina Mbowe, Lissu, Matiko, Zitto, Maalim n.k maana hawa ndio kipaumbele chetu
 
lolote litakalotokea msisahau kuhusu Taifa leo
 
Back
Top Bottom