Chukua muda wako kutazama hizi Movies Weekend hii

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,487
23,859
Nina furaha nimerudi tena uwanjani hapa ikiwa ni toleo langu la saba sasa kuhusu movies mbalimbali. Ni matumaini yangu mko salama. Sasa Weekend ndo' hiyooo inasogea, wengine hatuna mambo ya clubs wala drinking, tunafanyaje? Tunakaaa ndani kutazama movies.

Bila kupoteza muda, tutazame movies ambazo waweza kuzipatia muda na bundle lako pasipo kujutia. Na endapo ukizipenda, nimekuwekea link ya channel ya Telegram ambapo waweza zipakua for free!

Kabla ya kuendelea let me declare my interest, mimi ni mpenzi sana wa movies za kaliba ya 'mysteries', 'thrillers' na 'horrors'.

01. BROKEN
e85cc099749f364e7b4778b3f8b8ff00.jpg

Bwana Sang ni mwanaume afanyaye kazi kiwandani. Alishampoteza mkewe kwasababu ya saratani na hivyo basi anaishi peke yake na mtoto wake wa kike kwa jina Soo-jin.

Siku moja jioni, mvua ikiwa inanyesha, maisha yake yanabadilika kabisa. Anarudi nyumbani na kukuta binti yake hayupo na kama haitoshi hapokei hata simu yake.

Akiwa anadhani pengine atakuwa kwa marafiki zake na hivyo basi atarejea si muda sana, bwana Sang anaendelea na mambo yake bila shaka. Lakini habari inakuja geuka pale anapopokea simu toka polisi akihitajika kufika mochwari kuutambua mwili wa binti yake!

Binti alibakwa na kuuawa.

Tangu siku hiyo bwana Sang akawa anaenda polisi akitumai kusikia watuhumiwa wamekamatwa na haki imefuata mkondo wake lakini haikuwa vivyo, kila ajapo anajikuta anarudishwa nyumbani akiambulia tu ahadi!

Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.

Siku moja bwana Sang anakuja pokea ujumbe kwenye simu akijuzwa watu wawili walioshiriki kwenye mauaji ya binti yake, na zaidi anapewa mpaka anwani ya wapi watu hao wanapopatikana. Sasa bwana Sang anaamua sasa hivi kutokushirikisha polisi, achukue sheria mkononi.

Kutokana na hayo anajikuta akiwa anasakwa na polisi (fugitive) huku yeye akiwa anasaka haki!

Lakini katika namna ya ajabu kabisa, mpelelezi wa kesi hii ya mauaji ya mtoto anakuja baini kitu ambacho hata nawe kitakuacha mdomo wazi kwa duwazo!

Kila mpelelezi huyo anapopangilia shahidi zake kumbaini muuaji wa binti, Soo-jin, anajikuta zikimuelekea baba yake mzazi! Yaani bwana Sang!

Shusha pumzi..

02. THE YELLOW SEA

027ba31e7d1aafd3da69af238c85cf71(1).jpg

Bwana Nam ni mwanaume anayeendesha maisha yake kwa kuendesha taxi na pale anapokuwa hayupo kazini, basi hupenda kuhudhuria kwenye kumbi za kamari, matokeo yake anajikuta akiwa kwenye malimbikizo ya madeni makubwa yasiyolipika.

Mke wake anaelekea nchi nyingine, South Korea, kutafuta kazi akiahidi kutuma pesa nyumbani lakini muda unapita bwana Nam hapokei simu wala ujumbe wowote toka kwa mkewe. Anapata mashaka. Anafikiri huenda mkewe ameshapata bwana mwingine huko katika maisha mapya.

Kama hiyo haitoshi, anafukuzwa kazini na hata kale ka-pesa kake kadogo anakopata kanasombwa chote na wanaomdai tena huku ikiwa haitoshi kulipia hata robo ya deni!

Akiwa katika hali hiyo ya kuhitaji sana pesa, mkuu wa genge la wahuni na wahalifu anampatia kazi yenye pesa nono, dola alfu kumi za Marekani, punde tu atakapoitimiza. Ni kazi hatari sana. Lakini pia na pesa ni kubwa vilevile kiasi cha kumaliza matatizo yake yote.

Kazi hiyo ni kuingia ndani ya nchi ya South Korea kisha kumsaka na kumuua professor mmoja kwa njia ya kumgonga na gari!

Bwana Nam hana budi kuikubali. Anapewa kianzio cha dola mia tano, anazama nchini na kuanza kumfuatilia target wake huku pia akifanya jitihada za kumpata mkewe kwani naye yupo humohumo nchini alimokuja kufanya kazi yake dhalimu.

Sasa shida inakuja pale muda ulipofika wa Bwana Nam kufanya kazi, mambo ya ajabu yanatokea kiasi cha kushindwa kutimiza kazi alotumwa. Matokeo yake, polisi wanaanza kumsaka kama mtuhumiwa wa zoezi la mauaji!

Wakati huohuo na genge la wahalifu lililomtuma, na pia lenginewe, nayo yanamsaka kwa udi na uvumba yamtie mikononi!

Ukitazama filamu hii mpaka mwisho wake ndo' utajua ulikua hujui! …

Mke wa Nam yu wapi? Anafanya nini? Na Nini hatma ya Nam anayepambana na pande tatu tofauti?

03. RAMPANT

77f0d155b19249917b5c27f1aa72944d.jpg

Umeitazama na ukaipenda TRAIN TO BUSAN? Habari njema ni kwamba Part 2 yake imetoka kwa jina la PENINSULA: TRAIN TO BUSAN, humo mambo kama kawaida, ni kazi kazi!

Sasa mbali na hiyo, balaa likiwa limetokea town, kuna hii ambayo yenyewe version yake ni kipindi kile cha kale. Nchi ikiwa na utawala wa kifalme, ambapo humo kuna ugonjwa wa ajabu unazuka na kuwavaa watu na kuwafanya kuwa wanyama wenye kasi, nguvu na zaidi kiu ya damu! Wakiwa wanavamia na kuua watu nyakati za usiku.

Usiku si muda salama tena. Mbaya zaidi mpaka kwenye kasri ya mfalme.

Sasa humu, kisanga hiki kinamkabili bwana aitwaye Lee ambaye alikuwa mateka huko Uchina kwa takribani miaka 10. Bwana huyo ni mtoto wa mfalme lakini mwenye ujuzi mkubwa sana wa kupambana. Anaporejea nyumbani, anakuta hali si hali!

Nchi imechafuka. Hapakaliki.

Anaamua kubeba silaha kupambania usalama wa himaya ambayo sasa ipo mkononi mwa ndugu yake, wakipambana kufa na kupona dhidi ya jeshi la usiku kabla ya himaya nzima haijapotea.

04. THE MAN FROM NOWHERE

2def6d17d6443fe0af3e623c5b60394e.jpg

Maji yaliyotulia ndo yenye kina kirefu...

Bwana Tae ni mwanaume mwenye maisha ya kimya asiye na marafiki wala watu wa karibu isipokuwa kwa binti mmoja mdogo aitwaye So-mi anayeishi jirani. Binti huyo anaishi na mama yake teja ambaye anafanya kazi klabu ya usiku.

Mahusiano ya bwana Tae na binti huyu yalisababishwa na mtoto huyo hukaa na bwana Tae pale ambapo mama yake anaporudi nyumbani na wanaume anaolala nao. So kwa kiasi fulani, Tae ni kama vile anabeba jukumu la kumlelea mtoto huyu kwani kutokana na ulevi wa madawa wa mama, mtoto hapati malezi wala upendo stahiki wa mama yake. Ndivyo maisha yalivyokuwa.

Siku moja, mama huyo akiwa ameponzwa na mpenzi wake, anaiba kiasi kikubwa cha madawa yaliyokuwa yakifanyiwa mauzo hapo klabu. Anayatia kwenye mkoba wa kamera kisha anaenda kumpatia Tae amtunzie kama bondi, huku Tae akiwa hajui kama ndaniye kuna madawa.

Hiyo haikuwa shida.

Genge la madawa linaingia kazini kutafuta mali yao wakimtuhumu mama yake So-mi. Wanamkamata na kumtesa aseme madawa yalipo kiasi yabainika yapo kwa bwana Tae, muuza duka.

Hilo nalo halikuwa shida.

Shida inakuja pale ambapo genge hilo la madawa linapokanyaga waya kwa kumteka mtoto So-mi. Mtoto ambaye bwana Tae amejipatia jukumu la kumlinda na kumsaidia kwa njia yoyote ile. Sasa bwana Tae anaingia uwanjani kuwajuza wakulungwa rangi yake halisi.

Anafanya mambo yanayowaacha watu wakijiuliza bwana huyu ni nani haswa? Na nini kilimkumba akawapo dukani?

05. THE BLACK HOUSE

ee4b9b5954d79e1cda68ed652c5bd678.jpg

Hii ni aina ya zile movies zinazokula akili yako kadiri unavyoitazama, ama tuseme zinazokaba shingoni na kukunyima pumzi kadiri muda unavyoenda mbele.

Hii ni bonge ya 'psychological thriller' ingawa kuna baadhi ya watu hui-classify kama horror lakini si kihivyo. Ni movie ambayo kwa mbali inafanana na 'Drag me to Hell' lakini ikiwa na utofauti wake wa kipekee.

Ipo hivi, bwana mmoja anayefanya kazi kwenye kampuni ya bima, ikiwa ni siku yake ya kwanza kazini, anapokea simu akiulizwa kama bima yaweza kutolewa kwa mhusika endapo akijiua? Baada ya siku chache anapokea simu akihitajika kufika kwenye moja ya makazi ya mteja wao wa bima.

Anapofika huko anakaribishwa na mwanaume anayeongea naye kidogo kabla ya kumtaka aonane na kijana wake wa kiume. Afisa wa bima anapoingia chumbani anakutana na mwili wa kijana unaoning'inia kwenye kitanzi ukiwa tayari mfu!

Baada ya hapo, mwanaume huyu anahudhuria kwenye ofisi ya bima mara kwa mara akidai pesa ya bima iliyokuwa inalinda maisha ya mwanae. Afisa anamwambia awe mtulivu mpaka ripoti itoke, lakini katika hilo anakuwa akimtilia mashaka mzee huyu na kile kifo cha utata cha mwanae.

Baada ya muda anamlipa mzee huyu pesa yake ya bima, lakini anafanya makosa kwa kuingia mzigoni kumpeleleza mzee huyu akiwa anahisi kuwa ni michezo yake hii ya kufanya matukio kisha kukusanya pesa za bima… lakini afisa huyu anafanya hivi kutokana na historia fulani ilowahi kutokea kwenye familia yake hapo nyuma.

Safari hii anayoianza afisa huyu, inamdidimiza katika ulimwengu ambao hakuutarajia ama tuseme ni zaidi ya vile alivyokuwa anawazia.

06. THE SPY; Undercover Operation.

b853f5561747466aa2c4a6ec305f6621.jpg

Bwana Chul ni mtumishi wa usalama anayefanya kazi yake kwa usiri mkubwa sana kiasi kwamba hamna mtu yeyote wa karibu anayejua kazi yake, hata mkewe (Bibie Young) anayefanya kazi kama mhudumu wa shirika fulani la ndege ... mke anayelala naye kwenye kitanda kimoja hafahamu kitu!

Basi siku moja bwana Chul anamuaga mkewe kuwa anaenda Busan kibiashara lakini kiuhalisia bwana huyo alikuwa akielekea Thailand katika mji wa Bangkok. Huko kuna misheni kubwa sana inayogusa maslahi ya nchi yake moja kwa moja, misheni ambayo kwa namna yoyote ile inabidi iwe 'settled'.

Akiwa huko Bangkok, bwana Chul, katika namna ya ajabu, anapata kumwona mkewe ambaye alipaswa kuwapo nyumbani, Korea! Na mwanamke huyo hayuko peke yake bali na mwanaume mmoja mtanashati aitwaye Ryan!

Sasa kachero Chul anajikuta akiwa na kazi tatu za kufanya ndani ya Bangkok. Moja kupambania na kufanikisha misheni kubwa ya kitaifa, pili kujua ni nini mkewe anafanya Bangkok na tatu yule mwanaume aliye na mkewe, yaani Bwana Ryan, ni nani haswa! …

Kazi ipo.

...

Movies Na Stories
 
Nilivoona ni vimacho vidogo nikajua hamna muvi humo
Kwako. Lakini haohao unaoita vimacho vidogo ndo wamekomba Academy Awards mbele ya macho makubwa. Tena zaidi ya 3. Na kama wewe si mtu wa movies, let me enlighten you kwamba hamna yeyote anayewazidi hao unawapuuzia wewe kwenye genre ya thrillers na mysteries, sawa Uncle Sam?
 
Nina furaha nimerudi tena uwanjani hapa ikiwa ni toleo langu la saba sasa kuhusu movies mbalimbali. Ni matumaini yangu mko salama. Sasa Weekend ndo' hiyooo inasogea, wengine hatuna mambo ya clubs wala drinking, tunafanyaje? Tunakaaa ndani kutazama movies.

Bila kupoteza muda, tutazame movies ambazo waweza kuzipatia muda na bundle lako pasipo kujutia. Na endapo ukizipenda, nimekuwekea link ya channel ya Telegram ambapo waweza zipakua for free!

Kabla ya kuendelea let me declare my interest, mimi ni mpenzi sana wa movies za kaliba ya 'mysteries', 'thrillers' na 'horrors'.

01. BROKEN
View attachment 1566710

Bwana Sang ni mwanaume afanyaye kazi kiwandani. Alishampoteza mkewe kwasababu ya saratani na hivyo basi anaishi peke yake na mtoto wake wa kike kwa jina Soo-jin.

Siku moja jioni, mvua ikiwa inanyesha, maisha yake yanabadilika kabisa. Anarudi nyumbani na kukuta binti yake hayupo na kama haitoshi hapokei hata simu yake.

Akiwa anadhani pengine atakuwa kwa marafiki zake na hivyo basi atarejea si muda sana, bwana Sang anaendelea na mambo yake bila shaka. Lakini habari inakuja geuka pale anapopokea simu toka polisi akihitajika kufika mochwari kuutambua mwili wa binti yake!

Binti alibakwa na kuuawa.

Tangu siku hiyo bwana Sang akawa anaenda polisi akitumai kusikia watuhumiwa wamekamatwa na haki imefuata mkondo wake lakini haikuwa vivyo, kila ajapo anajikuta anarudishwa nyumbani akiambulia tu ahadi!

Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.

Siku moja bwana Sang anakuja pokea ujumbe kwenye simu akijuzwa watu wawili walioshiriki kwenye mauaji ya binti yake, na zaidi anapewa mpaka anwani ya wapi watu hao wanapopatikana. Sasa bwana Sang anaamua sasa hivi kutokushirikisha polisi, achukue sheria mkononi.

Kutokana na hayo anajikuta akiwa anasakwa na polisi (fugitive) huku yeye akiwa anasaka haki!

Lakini katika namna ya ajabu kabisa, mpelelezi wa kesi hii ya mauaji ya mtoto anakuja baini kitu ambacho hata nawe kitakuacha mdomo wazi kwa duwazo!

Kila mpelelezi huyo anapopangilia shahidi zake kumbaini muuaji wa binti, Soo-jin, anajikuta zikimuelekea baba yake mzazi! Yaani bwana Sang!

Shusha pumzi..

02. THE YELLOW SEA

View attachment 1566711

Bwana Nam ni mwanaume anayeendesha maisha yake kwa kuendesha taxi na pale anapokuwa hayupo kazini, basi hupenda kuhudhuria kwenye kumbi za kamari, matokeo yake anajikuta akiwa kwenye malimbikizo ya madeni makubwa yasiyolipika.

Mke wake anaelekea nchi nyingine, South Korea, kutafuta kazi akiahidi kutuma pesa nyumbani lakini muda unapita bwana Nam hapokei simu wala ujumbe wowote toka kwa mkewe. Anapata mashaka. Anafikiri huenda mkewe ameshapata bwana mwingine huko katika maisha mapya.

Kama hiyo haitoshi, anafukuzwa kazini na hata kale ka-pesa kake kadogo anakopata kanasombwa chote na wanaomdai tena huku ikiwa haitoshi kulipia hata robo ya deni!

Akiwa katika hali hiyo ya kuhitaji sana pesa, mkuu wa genge la wahuni na wahalifu anampatia kazi yenye pesa nono, dola alfu kumi za Marekani, punde tu atakapoitimiza. Ni kazi hatari sana. Lakini pia na pesa ni kubwa vilevile kiasi cha kumaliza matatizo yake yote.

Kazi hiyo ni kuingia ndani ya nchi ya South Korea kisha kumsaka na kumuua professor mmoja kwa njia ya kumgonga na gari!

Bwana Nam hana budi kuikubali. Anapewa kianzio cha dola mia tano, anazama nchini na kuanza kumfuatilia target wake huku pia akifanya jitihada za kumpata mkewe kwani naye yupo humohumo nchini alimokuja kufanya kazi yake dhalimu.

Sasa shida inakuja pale muda ulipofika wa Bwana Nam kufanya kazi, mambo ya ajabu yanatokea kiasi cha kushindwa kutimiza kazi alotumwa. Matokeo yake, polisi wanaanza kumsaka kama mtuhumiwa wa zoezi la mauaji!

Wakati huohuo na genge la wahalifu lililomtuma, na pia lenginewe, nayo yanamsaka kwa udi na uvumba yamtie mikononi!

Ukitazama filamu hii mpaka mwisho wake ndo' utajua ulikua hujui! …

Mke wa Nam yu wapi? Anafanya nini? Na Nini hatma ya Nam anayepambana na pande tatu tofauti?

03. RAMPANT

View attachment 1566703
Umeitazama na ukaipenda TRAIN TO BUSAN? Habari njema ni kwamba Part 2 yake imetoka kwa jina la PENINSULA: TRAIN TO BUSAN, humo mambo kama kawaida, ni kazi kazi!

Sasa mbali na hiyo, balaa likiwa limetokea town, kuna hii ambayo yenyewe version yake ni kipindi kile cha kale. Nchi ikiwa na utawala wa kifalme, ambapo humo kuna ugonjwa wa ajabu unazuka na kuwavaa watu na kuwafanya kuwa wanyama wenye kasi, nguvu na zaidi kiu ya damu! Wakiwa wanavamia na kuua watu nyakati za usiku.

Usiku si muda salama tena. Mbaya zaidi mpaka kwenye kasri ya mfalme.

Sasa humu, kisanga hiki kinamkabili bwana aitwaye Lee ambaye alikuwa mateka huko Uchina kwa takribani miaka 10. Bwana huyo ni mtoto wa mfalme lakini mwenye ujuzi mkubwa sana wa kupambana. Anaporejea nyumbani, anakuta hali si hali!

Nchi imechafuka. Hapakaliki.

Anaamua kubeba silaha kupambania usalama wa himaya ambayo sasa ipo mkononi mwa ndugu yake, wakipambana kufa na kupona dhidi ya jeshi la usiku kabla ya himaya nzima haijapotea.

04. THE MAN FROM NOWHERE

View attachment 1566704
Maji yaliyotulia ndo yenye kina kirefu...

Bwana Tae ni mwanaume mwenye maisha ya kimya asiye na marafiki wala watu wa karibu isipokuwa kwa binti mmoja mdogo aitwaye So-mi anayeishi jirani. Binti huyo anaishi na mama yake teja ambaye anafanya kazi klabu ya usiku.

Mahusiano ya bwana Tae na binti huyu yalisababishwa na mtoto huyo hukaa na bwana Tae pale ambapo mama yake anaporudi nyumbani na wanaume anaolala nao. So kwa kiasi fulani, Tae ni kama vile anabeba jukumu la kumlelea mtoto huyu kwani kutokana na ulevi wa madawa wa mama, mtoto hapati malezi wala upendo stahiki wa mama yake. Ndivyo maisha yalivyokuwa.

Siku moja, mama huyo akiwa ameponzwa na mpenzi wake, anaiba kiasi kikubwa cha madawa yaliyokuwa yakifanyiwa mauzo hapo klabu. Anayatia kwenye mkoba wa kamera kisha anaenda kumpatia Tae amtunzie kama bondi, huku Tae akiwa hajui kama ndaniye kuna madawa.

Hiyo haikuwa shida.

Genge la madawa linaingia kazini kutafuta mali yao wakimtuhumu mama yake So-mi. Wanamkamata na kumtesa aseme madawa yalipo kiasi yabainika yapo kwa bwana Tae, muuza duka.

Hilo nalo halikuwa shida.

Shida inakuja pale ambapo genge hilo la madawa linapokanyaga waya kwa kumteka mtoto So-mi. Mtoto ambaye bwana Tae amejipatia jukumu la kumlinda na kumsaidia kwa njia yoyote ile. Sasa bwana Tae anaingia uwanjani kuwajuza wakulungwa rangi yake halisi.

Anafanya mambo yanayowaacha watu wakijiuliza bwana huyu ni nani haswa? Na nini kilimkumba akawapo dukani?

05. THE BLACK HOUSE

View attachment 1566707

Hii ni aina ya zile movies zinazokula akili yako kadiri unavyoitazama, ama tuseme zinazokaba shingoni na kukunyima pumzi kadiri muda unavyoenda mbele.

Hii ni bonge ya 'psychological thriller' ingawa kuna baadhi ya watu hui-classify kama horror lakini si kihivyo. Ni movie ambayo kwa mbali inafanana na 'Drag me to Hell' lakini ikiwa na utofauti wake wa kipekee.

Ipo hivi, bwana mmoja anayefanya kazi kwenye kampuni ya bima, ikiwa ni siku yake ya kwanza kazini, anapokea simu akiulizwa kama bima yaweza kutolewa kwa mhusika endapo akijiua? Baada ya siku chache anapokea simu akihitajika kufika kwenye moja ya makazi ya mteja wao wa bima.

Anapofika huko anakaribishwa na mwanaume anayeongea naye kidogo kabla ya kumtaka aonane na kijana wake wa kiume. Afisa wa bima anapoingia chumbani anakutana na mwili wa kijana unaoning'inia kwenye kitanzi ukiwa tayari mfu!

Baada ya hapo, mwanaume huyu anahudhuria kwenye ofisi ya bima mara kwa mara akidai pesa ya bima iliyokuwa inalinda maisha ya mwanae. Afisa anamwambia awe mtulivu mpaka ripoti itoke, lakini katika hilo anakuwa akimtilia mashaka mzee huyu na kile kifo cha utata cha mwanae.

Baada ya muda anamlipa mzee huyu pesa yake ya bima, lakini anafanya makosa kwa kuingia mzigoni kumpeleleza mzee huyu akiwa anahisi kuwa ni michezo yake hii ya kufanya matukio kisha kukusanya pesa za bima… lakini afisa huyu anafanya hivi kutokana na historia fulani ilowahi kutokea kwenye familia yake hapo nyuma.

Safari hii anayoianza afisa huyu, inamdidimiza katika ulimwengu ambao hakuutarajia ama tuseme ni zaidi ya vile alivyokuwa anawazia.

06. THE SPY; Undercover Operation.

View attachment 1566708

Bwana Chul ni mtumishi wa usalama anayefanya kazi yake kwa usiri mkubwa sana kiasi kwamba hamna mtu yeyote wa karibu anayejua kazi yake, hata mkewe (Bibie Young) anayefanya kazi kama mhudumu wa shirika fulani la ndege ... mke anayelala naye kwenye kitanda kimoja hafahamu kitu!

Basi siku moja bwana Chul anamuaga mkewe kuwa anaenda Busan kibiashara lakini kiuhalisia bwana huyo alikuwa akielekea Thailand katika mji wa Bangkok. Huko kuna misheni kubwa sana inayogusa maslahi ya nchi yake moja kwa moja, misheni ambayo kwa namna yoyote ile inabidi iwe 'settled'.

Akiwa huko Bangkok, bwana Chul, katika namna ya ajabu, anapata kumwona mkewe ambaye alipaswa kuwapo nyumbani, Korea! Na mwanamke huyo hayuko peke yake bali na mwanaume mmoja mtanashati aitwaye Ryan!

Sasa kachero Chul anajikuta akiwa na kazi tatu za kufanya ndani ya Bangkok. Moja kupambania na kufanikisha misheni kubwa ya kitaifa, pili kujua ni nini mkewe anafanya Bangkok na tatu yule mwanaume aliye na mkewe, yaani Bwana Ryan, ni nani haswa! …

Kazi ipo.

...

Movies Na Stories
We jamaa unapenda movies kama nnazopenda mimi,
Action
Unpredictable ending
Mind games
Twisted plot
Emotianal.
Philosophical
Katika kazi moja.
Hapa kwenye list yako nimeona hiyo A man from nowhere.
Ntazitafuta hizi nyingine zote
 
Baba ndo mana asiyejua haya mambo hawezi elewa... twisted plots kama za The Yellow Sea, Oldboy, Hide and Seek, Mother n.k zina raha yake katika namna ya kufikiri and surprises.
 
Kwa wapendao great minds movies (akili kubwa) though ni za muda kidogo hapo nyuma lakini zinastahili kutazama..View attachment 1566724View attachment 1566726
Mkuu hizi zote nimeona, ziko poa sana nyingine hizi
Mmoja wa maproducer nnaowakubali sana (CHRISTOPHER NOLAN) alitengeneza hizi
1. Memento
2. Inception
3. TENET
Alitengeneza pia Batman Triology- hiyo haiingii kwenye hii orodha.

Movie nyingine zinazohitaji akili kuzielewa na zimetengenezwa kwa akili sana ni hizi
4. Predestination
5.60 seconds gone
6. Loopers
7. Primer
8. A beuatiful mind
9. Immitation game
10. Limitless
 
Memento na Inception ambayo ndani yupo Leonardo DiCaprio nimezitazama. Nitatoa muda wangu kuzisaka hizo zingine nikate kiu yangu.

Confession of Murder 2012

Memories of Murder 2002 pia worth a watch!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom