tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,517
- 21,544
Serikali imewanyima wananchi fursa ya kufuatilia mijadala ya wawakilishi (wabunge) wao kwa kuzuia matangazo yote yanayohusu mijadala bungeni. Mambo kama haya ndiyo yanasababisha serikali ya CCM kuchukiwa na wananchi na ndiyo yaliyopelekea serikali kutumia nguvu nyingi kupambana na UKAWA kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Kuna watu wanashabikia unyimivu huu wa taarifa kwa umma kwa sababu ya kutokujua. Wanadhani kwamba wanaokomolewa ni wapinzani. La hasha! Wanaokomolewa hapa ni wananchi, sio wapinzani. Wananchi wanayo haki ya kujua wawakilishi (wabunge) wao wanawawakilishaje bungeni. Hii ni haki yao ya msingi kabisa. Kuwanyima wananchi taarifa kwa kisingizio chochote kile ni kuvunja sheria za nchi kwa makusudi.
Serikali kuendelea kuwanyima wananchi taarifa zinazohusu wawakilishi wao kutazidi kuongeza chuki dhidi ya serikali. Watawala na wanachama watiifu waiokunywa maji ya bendera lazima wafahamu kwamba wananoa kisu kitakachotumika kuwanyoa wao wenyewe. Pia fahamu kwamba hata wanaCCM wanakosa taarifa pia na wengi wao hawapendi kunyimwa taarifa hizi muhimu kutoka kwa wawakilishi wao. Tumeshuhudia serikali zilizopita zikitoa uhuru wa habari kwa umma pasipo vikwazo vyovyote. Iweje hii Serikali ya Viwanda iwe ya kwanza kuwanyima wananchi taarifa. Kuna nini nyuma ya pazia?