Naona hujanielewa au labda ni mi sijakuelewa. Me sitaki kuongelea swala la nationality, my concern hapa ni citizenship. Na niseme tu naona unajikanganya, Unaposema mtu akitaka uraia wa Tanzania, na kama yeye ni mkenya itabidi aukane uraia wa Kenya. Ndio hasa ambacho si tunakitaka. We know these guys, bado hatujafikia hatua ya kuwa comfortable nao.
Na unaposema sheria ya inayopinga dual citizenship haimzuii mkenya kuwa na uraia wa Tanzania, me sielewi. Una maana kwamba mtu anaweza akaja Tanzania na kupata uraia bila kuukana uraia wa nchi yake. Kama ndio maana yako, basi nadhani unapaswa ku-revisit the facts.
Hivi chuki dhuidi ya wana diaspora na hasa toka kwa wanasiasa na watu wenye hali nzuri za kimaisha hapa nyumbani inatokana na nini?
Cha ajabu ni kuwa mawaziri na viongozi kadhaa wa serikali ya nchi hii watoto wao wana uraia wa nchi mbili mbili japo sheria hiyo haipo. Mfano Waziri wa mambo ya nchi za nje ambaye diaspora iko chini yake, Bw Bernard Membe, watoto wake ni raia wa Canada, Sisemi kuwa kuwa na uraia wa nje ni dhambi lakini ungetegemea kuwa alikuwa na uwezo wa kuwaandikisha wanae kuwa ni raia wa Tanzania lakini alikubali waandikishwe kuwa ni raiua wa Canada. Cha ajabu ni kuwa Mheshimiwa Membe amekjuwa kimya sana huku watanzania ambao wako Diaspora wakiendelea kusulubiwa na wanasiasa na vyombo vya habari hii inanipelekea kulizia kuwa hivi chuki na husda dhidi ya wana Disapora (ambao wengi wao ni watoto wa maskini) inatokana na nini hasa?
Hivi vyama vya siasa vina maoni gani kuhusu hili suala?
Mkuu you must have a crooked mind!Really? Mbona majibu yanatolewa kila siku lakini hamtaki kufungua masikio? Nikupe mfano mmoja tu. Kuna dada Mtanzania ambaye anafanya kazi NASA. Huwezi kupata kazi sehemu kama NASA kama hauna uraia wa Marekani. Huyu dada, ndugu zake WOTE wako Tanzania, lakini ilibidi apate kazi anayopenda na inayoendana na kisomo chake. Sasa, kama mtu huyu ambaye ana PhD ya aerospace engineering, Bongo arudi afanye kazi wapi? Je, na watoto wake ambao ni Watanzania-Wamarekani, nao ni "wasaliti" kama ambavyo mnajaribu kuwasulubu "waliojilipua"?
Sidhani kama Watanzania ni wajanja sana kuliko Wanyarwanda, Wakenya, Waganda, Waghana, na mataifa mengine sana ya Afrika ambao wanaruhusu uraia pacha. Kama kuna practical experience ya madhara ya uraia pacha, ningependa kusikia mfano. Vinginevyo hoja zinazotoka upande wa kupinga uraia pacha kama mada hii inayosema, zinaonekana kujaa uoga, chuki tu na husda, badala ya nondo za nguvu.
Mkuu you must have a crooked mind!
Huyo dada anaye fanya kazi NASA alitekwa nyara?
Hebu tuanzie hapo.
Do I have a crooked mind? Nah, far from it.
Mkuu, uliuliza swali - ngoja nirudie swali lako " Huo urai wa huko ughaibuni waliupata kwa minajili gani?", nikakupa jibu na mfano halisi. Lakini naona mwenzangu umeamua kuchanja mbunga kwenye personal attacks. Huyo dada hakutekwa, bali aliamua kufanya kazi anayoipenda, ambayo hawezi kuipata bila uraia wa Marekani na ni kazi ambayo Tanzania hakuna. Kama una hoja ya msingi ya kumlaani mtu kama huyu dada asipewe uraia pacha, ningependa kuisikia hiyo hoja yako. Ndiyo maana tuna mijadala kama hii ya wazi.