Chuji amshukulu Basena kwa kurudisha kiwango chake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuji amshukulu Basena kwa kurudisha kiwango chake

Discussion in 'Sports' started by baraka boki, Jun 7, 2011.

 1. b

  baraka boki Senior Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  source;mwananchi
  Clara Alphonce
  KIUNGO wa Simba Athuman Idd 'Chuji' amemshukuru kocha Mosses Basena kwa kurudisha kiwango chake huku Basena akisema kuwa kikosi chake kiko tayari kuwavaa DC Motema pembeya Congo hapo Jumamosi.

  Kauli hiyo ya Chuji imekuja siku chache baada ya kuanza mazoezi na timu yake ya zamani Simba akitokea Yanga.Chuji alisema kuwa kwa sasa yuko fiti baada ya kukaa muda mrefu nje ya uwanja akisumbuliwa na nyama za paja.

  ''Nashukuru Mungu, kwa sasa niko fiti nimerudi katika hali yangu baada ya kupata mazoezi magumu kutoka kwa kocha wangu, Basena ambayo yamenisaidia kurudi katika hali yangu kwa muda mfupi'' alisema Chuji.

  Naye Basena ambaye timu yake inarejea leo kutoka Tanga, alisema kuwa kambi ya Tanga imemsaidia pia kwa kiasi fulani, wachezaji wenzake kumuelewa kutokmana na utulivu uliopo.

  Alisema kwa kiasi kikubwa anakaribia kumaliza programu yake ya mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo ya Jumamosi ambayo ni ngumu sana kwao.

  Chuji, kiungo wa zamani wa Taifa Stars, alisema nia yake ni kuhakikisha kuwa hawapotezi mchezo huo baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Wydad Casablanca na kushindwa kuingia robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Alisema Motema Pembe ni timu ngumu hivyo anatakiwa kuwa makini kuakikisha hawapotezi mchezo huo japo bado kunatatizo katika suala la safu ya ulinzi ambalo bado analifanyia kazi.Hata hivyo alisema kuwa bado kuwakosa baadhi ya wachezaji waliokuwa kwenye timu zao za Taifa nalo linamvuruka kwa kiasi furani programu zake za mazoezi kwani hawezi kujua kwa kiasi gani timu yake imeiva japo amesema kwa waliopo anaoina wako safi.

  Katika hatua nyingine Simba imemnasa beki wa kati kutoka Nigeria, Felix Amaechi ambaye alitua wiki iliyopita na tayari yuko Tanga.
   
Loading...