Chota Maarifa Mbalimbali Uboreshe Maisha Yako

emma115

Senior Member
Apr 28, 2012
135
167
Ndugu zangu watanzania,hivi sasa tunakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo mi nadhani tunahitaji kupata suluhisho lake.Lakini kupata suluhisho ni jambo gumu sana hasa ukizingatia tunakabiliwa na tatizo la uchambuzi na upembuzi wa mambo kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa watanzania walio wengi.

Lakini watu wengi wanadhani kuwa na elumu ni lazma ufike chuo kikuu, sio kweli,unaweza kufika chuo kikuu lakini bado ukawa hujaelimika. Sasa kutokana na tatizo hili nimeona nielezee kwa ufupi baadhi ya vitabu ambavyo ukivisoma utapata manufaa makubwa.

1. The 7 Habits Of Highly Effective People – Steven Convey
Hapa utajifunza tabia saba za watu wenye ushawishi mkubwa na mafanikio pia. Unataka kufikia mafanikio makubwa? Fanyia kazi tabia hizi saba.

2. Donald Trump - Never Give Up
Katika kitabu hiki bilionea mwekezaji kwenye majengo Donald Trump anatushirikisha mbinu alizotumia yeye kutoka kwenye madeni mpaka kufikia kuwa bilionea kwa kuwekeza kwenye majengo, tena bila hata ya kuanza na fedha zake mwenyewe.

3. Anthony Robbins - Time of Your Life
Ningekuw ana muda ningefanya hiki, ningefanya kile na kadhalika. Hizi ni kauli maarufu sana kwa watu wengi. Anthony Robbins anakuambia una muda mwingi kuliko unavyofikiri. Muda huo uko wapi?

4. Your Right To Be Rich – Napoleon Hill
Unafikiri wewe huna haki ya kuwa tajiri? Unakosea sana, haki yako ipo, sema hujaijua ili uweze kuidai na kuisimamia. Napoleon Hill anakupa haki yako kwenye kitabu hiki.

5. Rich Dad's Guide to Investing – Robert Kiyosaki
Kama mpaka sasa hujaanza kuwekeza, upo kwenye hatari kubwa. Kama utapita siku ya leo bila ya kujifunza kitu kuhusu uwekezaji na kukifanyia kazi, hakuna kitakachokusaidia wkenye dunia hii. Robert Kiyosaki anakupatia muongozo mzuri sana wa uwekezaji kwenye kitabu hiki

6. Guide to Becoming Rich – Robert Kiyosaki
Robert kiyosaki na hapa tena anaendelea kukupa mbinu nzuri za kuweza kufikia utajiri. Haihitaji uibe au udhulumu, haihitaji uende kwa mganga, bali inahitaji wewe kujua misingi na kuifuata, na utajiri unakuja wenyewe.

7. 177 Mental Toughness Secrets of the World Class – Steve Siebold
Kuna tofauti kubwa sana ya kimawazo kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa. Steve Siebold anakupa siri 177 za watu waliofanikiwa sana ambazo watu wasiofanikiwa hawazijui. Unataka kuzijua?

8. Lessons from the Richest Man Who Ever Lived - Steven K. Scott
Kitabu hiki kina masomo muhimu sana kuhusu maisha na mafanikio kutoka kwa mtu tajiri sana aliyewahi kuishi na pia mtu mwenye busara sana kuwahi kutokea. Huyu ni mfalme Selemani. Steven Scott amekuchambulia siri muhimu za maisha kutoka kwenye maandiko ya Mfalme Selemani, nakusihi sana, usiache kukitafuta kitabu hiki. Yaani ni tuisheni kamili ya maisha, sio mafanikio na utajiri tu.

9. Neil Cavuto - Your Money Or Your Life
Maisha ni kuchagua na kila unachochagua kila siku kinakupeleka kwenye umasikini au kwenye utajiri. Tafuta kitabu hiki ufanye maamuzi yatakayokupeleka kwenye utajiri.

10. Anthony Robbins - Power To Influence
Mafanikio yako kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla yatatokana na jinsi unavyoweza kushawishi wale watu ambao ni muhimu kwako. Utamshawishije mteja anunue? Utamshawishije boss akuongeze mshahara? Anthony Robbins anakupa mbinu hizo

11. Anthony Robbins - Personal Training System
Kutengeneza mkakati wa kubadili maisha yako sio kitu rahisi. Anthony anakupa mfumo mzuri utakaoweza kuutumia kujifunza na kubadili maisha yako.

12. David Bach-The Automatic Millionaire
David Batch anakupa siri ambazo zitakuwezesha wewe kufikia utajiri hata kama unapata kipato cha kawaida. Anakupa siri ambayo watu wengi wameitumia kufikia utajiri kwa kufuata misingi mizuri na kwa muda mrefu. Kama hutaki misukosuko ya kibiashara, unapenda kuendelea na kazi ya kuajiriwa lakini pia ufikie utajiri basi tafuta kitabu hiki.
 
Mada nzuri sana. Nitajitahidi angalau nisome nusu ya vitabu hivi mkuu. Asante sana kwa sababu elimu haina mwisho na wengi wetu tu mbumbumbu hasa kwenye masuala ya pesa na matumizi sahihi ya muda.

Angalizo: Usitegemee comments wala likes nyingi kwenye mada kama hii.
 
Heshima Mkuu!!

Frantz Fanon anasema "Tuendelee kuelimisha wananchi mpaka wajue wao ndiyo wenye nguvu ya kuleta mabadiliko na hakuna mtu yeyote mmoja anayeweza kuleta mabadiliko isipokuwa wao wenyewe".

You did the best ''Great thinker" ila kama una PDF za vitabu vyote hapo juu ulivyoviainisha ingekuwa vyema kushea nasi ili tukapate kulisha "Chakula cha Akili" ubongo wetu.

Nashauri tuzidi kusoma vitabu kadiri tuwezavyo ili tuzidi kupata maarifa mbalimbali.Albert Einstein aliwahi kusema "Once you stop learning,you start dying"

Reading Educate!!
 
Wabongo walivyo wavivu kusoma vitabu, labda uwasimulie.Shuleni walisoma ili wajibu mitihani na si vitabu bali walisoma vitini.
 
Back
Top Bottom