Sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizokamatwa nyumbani kwa Billionea huyo.
Moja ya tukio ambalo limewatikisa polisi baada ya kumkamata Mharami Mohamed Abadallah Chonji ni kumkuta na sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kufanya upekuzi wa kina nyumbani kwake Magomeni Kondoa, jijini Dar.
Sare hizo zinafanana kwa sehemu kubwa na zile zilizomwingiza Mbongo Fleva, Nasibu Abdul Diamond kwenye mzozo na jeshi hilo.
Mbali na sare kwa maana ya mavazi, pia mtuhumiwa huyo alikutwa na viatu vya jeshi hilo maarufu kwa jina la buti nazo zikiwa mpya!
Katika hali iliyowatia shaka zaidi askari ni pale Mharami alipopekuliwa zaidi na kukutwa na bastola ambayo jeshi la polisi halijaitolea ufafanuzi inaitwaje na ilitengenezwa nchi gani!
Vitu vingine vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo ni jiko dogo la gesi na gundi ya plastiki, vyote vinaaminiwa kutumika wakati wa kutengeneza kete za unga tayari kwa kusafirisha.
Mkuu ushahidi unao? Kama upo tushilikiane na polisi juu ya jambo jili.na idd azan pia asiachwe.
Mkuu ushahidi unao? Kama upo tushilikiane na polisi juu ya jambo jili.
kumbe polisi wakiacha rushwa kazi inafanyika
a basket of fruitsWhat do you see?
Kwako wewe kigogo ni MTU wa na na gani???!!!! Umeambiwa huyu ni boss wa mateja, unadhani ni Nani zaidi yake???!!!!. Sema tu huyu amekamatwa sababu amemdhuru mwenzake physically, ni kisasi na huyu hachomoki. Orodha ya akina papa msofe waliodhani wako juu ya sheria inazidi kuwa ndefuhuyo wamemkomesha maana aliingikia anga za mtu
hawana
lolote zuga tu hatuna imani na nyinyi mpaka wakamatwe vigogo
Sasa kama hatujaambiwa inaitwaje na imetengenezwa wapi ni nini kinachofanya hali hiyo iwatie "shaka zaidi"? In other words, nini cha ajabu??? Na umejuaje imewatia polisi "shaka zaidi" wakati wamekataa kukwambia ni bastola gani na imetengenezwa wapi? In other words, waliposema bastola hii inatutia shaka zaidi, walisema ni kwa nini????? Hahahaha... waandishi wa Tanzania banaKatika hali iliyowatia shaka zaidi askari ni pale Mharami alipopekuliwa zaidi na kukutwa na bastola ambayo jeshi la polisi halijaitolea ufafanuzi inaitwaje na ilitengenezwa nchi gani!