Chongolo akemea wanaosaka Ubunge

Chongolo akemea wanaosaka Ubunge

Shabani Ajaha

Member
Joined
Aug 18, 2021
Posts
78
Reaction score
60
CHONGOLO AKEMEA WANAOSAKA UBUNGE SASA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo kutafuta wapambe ili wawasaidia kwenye malengo yao ya Ubunge na udiwani kwa mwaka 2025.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Chama hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya CCM ili kuwadhibiti watu hao, kwani muda wa uchaguzi bado na sasa kila jimbo lina mbunge na kila kata kuna diwani hivyo ni vema kwa kila mwanachama kusubiri muda ufike na sio kuanza sasa wakati viongozi waliochaguliwa wanafanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 13 Julai, 2022 wakati akifungua kongamano la Mafunzo ya Uongozi kwa mabalozi wa mashina na viongozi wa matawi mkoa wa Dodoma.

#chongolokazini
#kaziinaendelea

IMG-20220713-WA0144.jpg
 
CHONGOLO AKEMEA WANAOSAKA UBUNGE SASA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo kutafuta wapambe ili wawasaidia kwenye malengo yao ya Ubunge na udiwani kwa mwaka 2025...
Mbona karibia Wabunge wote walipitishwa na mwendazake bila kupingwa,Sasa kwani wanajipitisha kwenye majimbo yapi? Maana hata walipita kwenye majimbo wananchi hawawajui,

si mliona wananchi wa Jimbo la Iringa mjini,walivyokuwa wanamshangaa yule Mbunge.
 
Back
Top Bottom