Leo ni siku ambayo kampeni nhini Tanzania zinaanza kuelekea uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 28 Oktoba 2020. Niwaombe wanasiasa wafanye kampeni za kistaarabu, ni wakati wao wa kuuza sera zao. watueleze ni namna gani wamejipanga kuendeleza na kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya nchi yetu na wananchi kwa ujumla.
Ni muda muafaka kwa wananchi kuwapima wagombea nani ni nani anafaa kutuongoza. Tuwapime kwa sera zao,najua wapo ambao tayari walikuwepo madarakani halafu wamekuja kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena wengine ni wapya kabisa,lkn kikubwa ni kuangalia wamebeba nini katika sera zao. Siyo muda muafaka wa kushabikia chama ni muafaka wa kuchagua mtu mwenye uwezo wa kutetea na kupambania maendeleleo ya watu na maeneo husika.
Vurugu na matusi havijengi na wala siyo ustaarabu , tunataka kampeni zenye viashiria vyote vya AMANI. Vyombo vya ulinzi na usalama naomba vifanye kazi yake kwa weledi pasipo upendeleo wa aina yoyote ile na TUME ya uchaguzi nayo ifanye kazi yake kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi pasipo kupendelea chama au mgombea yeyote.
Niwatakie Watanzania wote kila la heri kuelekea Uchaguzi Mkuu. MUNGU IBARIKI TANZANIA.