CHONDE CHONDE WABUNGE SIKUWATUMA KWENDA KUISIFIA SERIKALI BALI KUISIMAMIA..

Hashim bin Faustin

Senior Member
Jan 30, 2017
177
216
Kwa kweli nashindwa kuwaelewa Baadhi ya wabunge wetu, kwani utakuta Mbunge kasimama kuchangia bajeti ya wizara husika lakini cha kustajabisha ataanza na misifa na kumalizia na misifa , Je hiyo ndiyo kazi yako ?? Kwani siye tulio kuwepo huku mtaani Hatuoni mazuri ya JPM na Mawaziri wake ?? Kwani wewe ni Mbunge wa Serikali au Wananchi ??

Eti na mishipa inamtoka utasikia Rais Mzuri, Waziri Mkuu Mzuri , Mawaziri wazuri ebooo !! Kwani wewe ni Jaji wa Uzuri ?? Hujuwi kazi yako ?? Baada ya kutoa mawazo ya Kujenga na Kuboresha Nchi unabakia kutoa sifa tu.

Eti wanasifia Kwa kununua Ndege au Kukusanya kodi , kwani hizo Kodi zinalipwa na nani ?? Bila sisi walala hoi kulipa kodi zetu na michango yetu ya nssf hizo pesa za kununua Ndege angezipata wapi ?? Je angezitoa mfukoni kwake ? Naomba mjuwe Uzuri wa Rais wetu tunaujuwa sisi Wananchi kwani sisi ndiyo tulio mpa kazi ya Urais na sisi ndiyo tunalipa Kodi na yeye anatumia Kodi zetu kufanya anayo ya fanya.

Wewe Mbunge tumekupa kazi ya Kwenda Kusimamia na Kushauri siyo Kwenda kusifia sifia tu ndiyo maana mnazaraulikaa ovyo ovyo kwani hamjitambui kabisa. Eti mwengine nimemsikia eti anasema na kuwashauri wenzake wafanye ubia wa biashara Ebooo ...!! Kwa hiyo mshakuwa mabusiness woman na man ehee ?? Eti waungane pamoja wafungue kiwanda. !?? Amakweli akili ni Nywele kila mtu anazake.

Mimi napenda kusema ukweli bila kumumunya maneno na kusema kweli Baadhi ya wabunge ni vilaza na wanakula kodi zetu bure wanatakiwa wapigwe chini kabla ya 2020. Sisi huku mtaani tunahangaika kulipa Kodi ili Serikali ipate hela za Maendeleo wao kazi yao Kwenda kuimba Taarabu za kusifia.

Kunammoja nimemasikia analinganisha Nchi yetu ya Amani na Upendo Tanzania na Rwanda au Nchi za Uarabuni. Hajuwi hata historia ya Nchi yetu. Sisi ni watu wa Amani na tumedai uhuru wetu kwa Amani pia Nchi yetu haiongozwi kiimla/Kijeshi bali Viongozi wetu ni wasikivu kwa Wananchi na ndiyo utamaduni wetu. Hivyo anapotokea kiongozi wetu kwa njia moja au nyengine anateleza lazima tumkumbushe kwa busara bila woga au unafiki. MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU. Hivyo wewe Mbunge Acha kututisha na historia ya Burundi au Rwanda. Hii siyo Nchi ya Kijeshi.

NAWAOMBA WABUNGE WOTE MSHIRIKIANE KUISIMAMIA SERIKALI KWA NGUVU ZOTE ILI TUWEZE KULETA MAENDELEO YA KWELI. ACHENI UNAFIKI NA WOGA SEMENI KWELI DAIMA.
 
Hili la kulinganisha nchi yetu na Rwanda, Burundi au DRC ni kama wimbo wa kundi Fulani ili kutisha wananchi. Kweli mbunge unafikia kumwambia raia halali wa nchi yako kaimbe Burundi uone kama hujapotezwa? Unaomba kupewa urais siku 2 ili upoteze watakaokukosoa au hata kukutolea maneno usiyoyapenda? Halafu ndani ya bunge hilohilo kuna watu wanakupigia makofi kukusapoti? Tulifanya makosa sana kwenye suala la katiba mpya. Huyu hasitahili kumaliza miaka 5.
 
7d299c5f80980c623cad5a5dc905195f.jpg
 
Miaka 50 tangu kupata Uhuru, jimbo halina barabara, hakuna hospitali, huduma za elimu ni kituko, ajabu yake mbunge anasifu utawala.
Hata hivyo kipimo cha wanajimbo(wananchi) wanaojitambua ni pamoja na uwepo wa huduma bora za jamii.

Ukiona jimboni hakuna maendeleo huo ni utambulisho tosha kabisa wa namna wanajimbo walivo lala kifikra.

Uongozi wa hovyo huchangia maendeleo ya hovyo.
 
Back
Top Bottom