Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Tatizo la kukatika kwa umeme imekuwa kero katika maeneo mbalimbali ya nchi na lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa shirika la umeme Tanzania (Tanesco).
Maeneo mengi yamekuwa yakikumbwa na kero hiyo huku wahusika wakishindwa kutoa taarifa ya nini hasa kinachosababisha kero hiyo ya kukatika kwa umeme.
Hali hiyo inasababisha adha na kuhatarisha maisha na mali zetu kwasababu umeme unavyokatika na kurudi inakuwa ni usumbufu kwa watu na wakati mwingine vitu huweza kuungua.
Kwahivyo siku kama ya leo ya eid el-fitr na nyinginezo watu tunakuwa tuko mapumzikoni pia hutembelewa na ndugu jamaa na marafiki kwa kupeana pongezi kufurahi, haitakuwa jambo jema kukatakata umeme na kurudisha.
Tunawaomba Tanesco kuepusha kero ambazo hazina ulazima vinginevyo tafsiri yake ni hujuma kwa tabaka fulani.
Eid mubarak kwa waislamu wote kulu ammu waantum bikheir na kwa watanzania wote.. amani na upendo daima.