Chonde chonde serikali

Chonde chonde serikali

dindili

Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
50
Reaction score
21
Habari za wakati huu jamani tuiombe serikali ya jamhuri ya muungano was Tanzania hasa salamu hizi zimfikie mheshimiwa rais wetu mheshimiwa wetu doctor John pombe maghufuli alifanyie kazi hili suala kuzuia watu kuja huku nchi za falme za kiarabu hususani Oman mheshimiwa rais wetu mheshimiwa wetu doctor wetu mpigania haki za wanyonge tunakuomba Sana utusaidie nini kifanyike ili tuweze kujikimu kimaisha mfano uko hivi Mimi Nina watoto wanahitaji msaada wangu kimasomo mmoja kamaliza chuo kikuu lakin Hana kazi na mwengine kamaliza form 4 wapo tu hawana kazi nimehangaika Sana nimetembeza sambusa na maandazi ili nisomeshe wanangu lakin hawana kazi mpaka leo hii na mume wangu Hana kazi na mgonjwa wa macho ndipo nilipoamua kuja nchini Oman kutafuta riziki Sasa Ninamaliza mkataba wa pili yaani namaliza miaka 4 Sasa nafikiria kurudi nyumbani nitarudi vipi ikiwa Hali imekuwa ukija hata likizo hurusuwi kurudi na Mimi Nina mtoto Yuko boarding secondary anahitaji msaada wangu mama yangu anahitaji msaada wangu je baba yetu mpendwa unatusaidiaje sisi wanyonge maana tukisema tunateseka si kweli vituko vingine tunaanzisha sisi wafanyakaz na maajenti huwa wanatuangalia Kama nyumba umepata sio watu wema ajenti anakuchukua anakupeleka nyumba nyingine tunakuomba Sana Sana Sana baba yetu ulifanyie kazi mwenyewe hili suala hata nikisema nirudi niuze Tena maandaz hata kodi itanishinda ya mwez tunakuomba Sana Sana baba yetu kipenzi mwenyewe huruma na mapenzi kwa wananchi wako tusaidie tufungulie mipaka kwa mm binafis nakuomba utusaidie na kingine Kuna baadhi yetu tunakuja huku cku mbili mtu akisikia tu mume wake cjui kafanyaje huko basi anaanzisha fujo kwa mabos wake mheshimiwa rais hakuna binadamu aliekamilika tukija huku kufanya kazi basi tuwe na heshima hata Kama bosi umemzidi umri lazima ufuate sheria tusaidie baba tufungulie njia tuna Nia ya kutafuta na wengine wakichoka kazi wanajifanya vichaa ili warudishwe hili nalo liangaliwe mheshimiwa rais tunakuomba Sana baba yetu tuangalie kwa jicho la huruma wengi tunakuwa waongo ukifika huku hununui sabuni Wala nguo unahudumiwa Kama familia moja nakuomba Sana Asante naamin utatusaidia kadiri ya uwezo wako shukurani
 
Sijaelewa kitu hapa!!!

Naona baba nyingi tu, sijaelewa kinachohitajika hapa kutoka kwa baba, ngoja nikae pembeni nisubiri wenzangu huwenda wapo walioelewa
 
Umekurupuka kitandani sijui ulikuwa unaota ndoto za kichawi,hujapiga hata mswaki kurupu huyo ukakamata kimeo chako na kupost taka zako hapa,shubaaaamit.

Hakuna aya,hakuna koma,hakuna nukta na pia hakuna mantiki.
 
Umeandika hovyo sana, nimejitahidi kusoma, hamu ya kuendelea kusoma imekata njiani.
 
Ulimkimbia mmeo ukakimbilia huko uarabuni maisha yamekugeuza unaomba kurudi ndo ukome sasa,tunaogopa waweza kuwa Al-Qaeda wewe si bure
 
Me sijaelewa unahitaji msaada gani?
 
Ulimkimbia mmeo ukakimbilia huko uarabuni maisha yamekugeuza unaomba kurudi ndo ukome sasa,tunaogopa waweza kuwa Al-Qaeda wewe si bure
Mkuu. Hujamuelewa anachoomba kwa Mhe. Rais ni akija Bongo, aruhusiwe kurejea kazini kwake,
Inaonekana kuna zuio la kurejea nje pindi wanapofika Nchini
 
Me sijaelewa unahitaji msaada gani?
Nimemuelewa hivi
Anamuomba Raisi awaruhusu kurejea ktk vibarua vyao pindi wanapokuja rikizo, inaonekana kuna Zuio limewekwa na Serkal la kurudi Oman pindi wanapofika Tz
 
Sawa kabisa
Nimemuelewa hivi
Anamuomba Raisi awaruhusu kurejea ktk vibarua vyao pindi wanapokuja rikizo, inaonekana kuna Zuio limewekwa na Serkal la kurudi Oman pindi wanapofika Tz
 
Dah ningekuwa kwenye mtihani ningeambulia sifuri kabisa...labda kwa kuwa ujumbe unauelekeza kwa Dr mwenye PhD yake ataelewa.....
 
Back
Top Bottom