Chokoraa wengi Baba zao ni Wabunge?.

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
Mbunge wa Tarime (CHADEMA) Chacha Wangwe, kama kawa ametoa kimbwanga Bungeni kuwa watoto wengi wa mitaani baba zao ni wabunge.

Wangwe ambaye kila kukicha huwa anaibuka vimbweka vya aina
yake alitoa kali ambayo inaweza ikawa ya kweli hiyo alipokuwa akichangia katika kamati ya Wizara ya jinsia Wanawake na Watoto.

Alisema kuwa wasichana wengi hupewa mimba na waheshimiwa
wabunge na kuwatekeleza kwa hiyo akashauri adhabu yao iwe ni kuozeshwa na si kifunguo.

Wangwe ambaye ni maarufu kwa jina la mesege sent huenda hoja yake hiyo ikawa ya kweli any way ukweli ni upi?
 
Back
Top Bottom